VITA KALI TANZANIA- Ni ya Ukweli na Uongo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

VITA KALI TANZANIA- Ni ya Ukweli na Uongo

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mwanza_kwetu, Jul 29, 2011.

 1. m

  mwanza_kwetu JF-Expert Member

  #1
  Jul 29, 2011
  Joined: Mar 2, 2011
  Messages: 684
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Wandugu;

  Kwa kipindi sasa Tangu baada ya uchaguzi mengi yameonekana kwa macho; kubwa na ambalo mie nalitafsiri ni kuwa sasa kuna vita kali kati ya ukweli na uongo. Tumeona ufinyanzi wa matokeo na kumpa JK mamlaka kuendesha nchi kwa gharama yoyote ile (walijiandaa hata watu wafe potelea mbali);ahadi lukuki ambazoi hazikutekelezeka tangu 2005 mpaka leo na ahadi ambazo zinazidi kutolewa kila mkuu wa nchi akienda mikoani baada ya safari zake za nje ya nchi;Tangu mwanzo wa mwisho wa uchaguzi 2010 kwa kweli wenye haki na wasiopenda shari walikaa kimya pamoja na dhuluma zote zilizokuwa wazi; hatimaye ikazuka uzushi eti Dk Slaa atakoksa la kufanya; sasa ana mengi ya kufanya; wamekosa ya kusema; hatimaye tukaona haki zinavyofinyangwa angalia Tabora, Arusha, Tarime, Geita, Mbeya, Dar, Kahama, Shinyanga na sehemu zingine; sasa wabunge wameonekana hamna cha maana wanachofanya zaidi ya kukubali kila linalokuja na kuletwa na serikali. Maandamano eti yanaleta uvunjivu wa amani; imedhihirika serikali na vyombo vyake ndio vinavunja amani (refer mazishi ya marehemu watatu pale Arusha bila msaada wa askari)
  Kwa sasa watu wanadai mambo mengi; ikiwemo umeme; chakula (ukosefu ubunifu), miundombinu, ukosefu wa wa ajira, elimu isiyo na balance nk bado hayana majibu; sasa kila siku serikali na wabunge wake wanatumia uongo kuwalazimisha waamini kitu ambacho hakipo kabisa katika utaratibu wa kiserikali; sasa naamini ya kuwa Kweli siku zote nuru(chadema kwa sasa) haishindani na giza (CCM+serikali); mwisho wa siku naona wataona heri wafanye nini ila serikali iko hoi aibu kubwa sana kwa uongozi uliongia kwa kuaminiwa kutia aibu ya aina hii sijawahi kuona hata kidogo; ngoja tuone sisi tumetulia lakini Mungu mkuu anaonyesha njia kule tuendako na mwisho wa siku serikali ya CCM chali
  Karibuni
   
 2. yutong

  yutong JF-Expert Member

  #2
  Jul 29, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 1,604
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Mgonjwa akikaribia kufa huwa anaongea sana siku hiyo. Kama alikuwa hawezi kutembea atajitahidi kutembea angalau hatua moja ili ajiridhishe kuwa bado ni mzima. Angalia Magamba wanavyoongea ongea ovyo ali hali wanajijua kuwa wao ni wangonjwa mahututi. Hatutakubali kuibiwa kura zetu tena mwaka 2015
   
Loading...