Vita kali inayoendelea Hollywood

Vita kali inayoendelea Hollywood

Chilojnr

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2012
Posts
308
Reaction score
1,354
VITA KALI INAYOENDELEA HOLLYWOOD

Ukifika pale Marekani, sehemu moja iitwayo Hollywood, utakutana na vita moja kali sana kwenye masuala ya filamu, hivi vita ni za makundi matatu, ila kundi moja linaonekana kuchemka mapema sana.

Hii vita kabla ya kuanza miaka ya 2000, hapo mwanzoni kulikuwa na kundi moja tu ambalo lilionekana kuwa tishio, kundi hili lilitwa DC.

Kwa miaka ya nyuma sana mpaka ile ya 90, DC alikuwa juu sana kwenye upande wa kutengeneza filamu bora na kali. Yeye aliwashikilia zaidi characters wake wawili, Superman na Batman, na kwa kupitia hao, walitengeneza jina kubwa sana na kuwapa pesa.

Kwenye miaka hiyo ya 90 wakati nikifuatilia, nilikuwa najiuliza tu, hivi itakuwaje siku Batman na Superman wakawa kwenye muvi moja? Itanogaje aisee!

Miaka ikakatika mpaka pale ambapo Stan Lee (Mwanaume wa shoka) alipoamua kumleta Spiderman kwenye filamu, hiyo ni kutoka kwenye kampuni ya Marvel. Kumbuka kipindi ha nyuma alikuwa akionekana kwenye vitabu vya comic tu.

Kuanzia hapo, watu sasa wakawa bize na huyo Spiderman, mzee wa kuruka maghorofa. Hapo nataka nikukumbushe tu kwamba kwenye vita vya watu hao wawili, yaani DC na Marvel, kuna mmoja akapenya na yeye kutaka vita, hii si kampuni bali jeshi la mtu mmoja aliyeitwa James Cameron.

Ngoja nikutonye kidogo kwanza. Huyu James Cameron, mwaka 1997 aliandaa muvi yake iitwayo Titanic, muvi ikawa nzuri na kwenye majumba ya sinema ikafanya vizuri sana kwa kuingizia kiasi kikubwa cha pesa zaidi ya muvi yoyote ile duniani.

Jamaa akashikilia usukani, kwenye vita hii ni kama hakuwepo na hata DC hawakumfikiria sana, wakaona mwamba kama amebahatisha hivi. Ilipofika mwaka 2009, jamaa akawapiga tena na kitu kizito usoni kwa kutoa muvi kali ya Avatar.

Hapa wakaona huyu mwamba yupo serious sasa kwani muvi hiyo ikaipiku Titanic na kukaa juu kwa filamu zilizoingiza pesa nyingi. Kwa maana hiyo, muvi ya kwanza ilikuwa ni Avatar, na ya pili ikawa Titanic.

Sasa miaka ilivyozidi kwenda mbele, DC ni kama walikuwa wakipoteza pumzi kwa sababu muunganiko wa stori zake haukuwa mzuri kabisa halafu kingine kilichowaangusha ni muonekano wa filamu zao, ni giza tu, yaani filamu zao zinaigizwa sana usiku kuliko mchana.

DC wakapunguza soko, wakati huo Marvel wakaja juu, wakapiga Captain America, Ironman, Spiderman, Thor, Guardian of Galaxy, Black Panther na nyinginezo, wakawa juu sana.

DC pamoja na ukongwe wake kwenye muvi, akapigwa chini. Sasa kitu kilichokuja kichwani mwa Stan Lee ni kuhakikisha muvi zao zinakuwa namba moja, ila watawezaje kumshusha James Cameron na Avatar yake?

Wakapiga muvi kama 22 hivi kuanzia mwaka 2008, muvi yao ya mwisho kabisa kwenye mfululizo huo ilikuwa ni Avenger Endgame. Walikamua sana, tena sana na hatimaye sasa, pamoja na figisufigusu zao za kibabe, wakafanikiwa kushika namba moja.

Kwa hiyo ikawa namba moja ni Avenger, namba mbili ni Avatar na namba tatu ni Titanic. Hapo kwanza James Cameron akatulia, akajifikiria weeee, akaona haiwezekani, akakumbuka mwaka 2009 wakati Avatar inatoka, haikuonyeshwa kwenye majumba ya sinema huko China, alichokifanya, akaichukua na kuionyesha huko mwaka 2019, ikapiga hela, akarudi tena namba moja.

Kwa hiyo msimamo ukabadilika, 1 ikawa Avatar, 2 ikawa Avenger Endgame na 3 ikawa Titanic. Hapo bado vichwa vya watu wa Marvel havijatulia, vinamfikiria James Cameron kwani mwaka kesho, anakuja na Avatar 2, halafu atapiga kama nne mfululizo, swali wanalojiuliza, je, wataendelea kuwa namba mbili ama hizo Avatar zitakuja kuwashusha? Manake huyu mtu ameonekana kuwa hatari sana.

Badala ya Marvel kupigana vita na DC, wamekwishaona ni mdogo kwake sokoni, sasa vita vyake wanapambana na James Cameroon ambaye anaonekana kuwa hatari.

KUFELI KWA DC

Kuna sababu nyingi za kufeli kwa DC lakini mbili kubwa ni muvi zao kuwa na giza sana, hili limekuwa likilalamikiwa sana na watazamaji hata huko Marekani lakini la pili, filamu zake zimekuwa za kibabe sana, huwa hazina comedy hata kidogo.

Ili Marvel waiunuke, walichokifanya ni kupambana na udhaifu wa DC, filamu zao wakazirekodi zaidi mchana kuliko usiku lakini pia wakawa wanaweka comedy nyingi za kuwachekesha hata watoto.

Ukitazama muvi kama Spiderman, script zake huwa ni za vichekesho sana, halafu siku zote Spiderman huwa haui, na kama utakufa, basi utafia kwa uzembe wako lakini si yeye akupige mpaka akuue, unajua kwa nini? Ni kwa sababu wamewekeza sana kwa watoto.

Ukiachana na hayo, DC stori zake huwa hazina muunganiko mzuri, nitakwambia kwa sababu gani. Ukicheki muvi za Marvel, huwa zinaanzia mwanzo, yaani mtu alipopata uwezo wake, halafu na maisha yake ya mbele.

Tazama muvi kama Spiderman, tulianza kuona pale alipoanza kung’atwa na buibui, ikaendelea mbele, ila njoo kwa DC sasa.

Ukiacheki muvi ya Justice League ile ya kwanza, kuna superhero anaitwa Aquaman. Tulimuona, tukajiuliza huyu mchizi ni nani? Imekuwaje mpaka kuwa hapa? Yaani tukawa tunashangaa, halafu mwaka uliofuata, eti ndiyo wakatoa muvi ya Aquaman, yaani mwanzo wa maisha yake mpaka alipokuwa hivyo alivyo, yaani hawapo serious kwenye suala hilo, nadhani ni muda wa Zack Snyder kukaa chini na kujifikiria upya kwenye uandishi wa muvi za hawa majamaa.

Baada ya DC kugundua kwamba hawana characters ya comedy, hapo ndipo wakaamua kumleta Flash lakini cha ajabu sasa, napo hawajatuambia huyu flash alianzia wapi mpaka kuwa hivyo alivyo, guess what...eti baadaye ndipo watakapoitoa muvi ya Flash kuonyesha ameupata wapi uwezo huo aliokuwanao. Nadhani labda wameelezea kwenye series zake, ila sisi tunataka kuuona mwanzo wake kwenye muvi na si series.

DC wanarukaruka sana kwa sasa, wamepunguza ubora wao, kila muvi wanayoitoa, inaonekana kuwa si lolote, kidogo kwa muvi ya Joker walipiga hatua ndefu mbele.

Ila pamoja na hayo, characters wa DC wanapendwa sana duniani. Batman na Superman ni supehroes maarufu kuliko wote duniani, si ajabu kuona jana Neymar amechora nembo ya Batman kichwani, hawa jamaa ni maarufu sana ila sokoni, wanapigwa vibaya mno.

MARVEL WANAJIIMARISHA TENA

Nikwambie kitu ambacho inawezekana hukuwa unakijua. Ile muvi ya 22 ndiyo ilikuwa ni ya mwisho kwa waigizaji kama Ironman, nafasi ilivyochezwa na Robert Jr, Captain America, nafasi iliyochezwa na Chris Evans ambaye ndani ya muvi alionekana kuwa mzee, mwisho wake ukawa hapo.

Ukiachana na hao, waliwamaliza characters kama Vision, Black Widow. Kwa maana hiyo, wanachokifanya kwa sasa ni kuwaandaa characters wengine ambao watakuja kushika nafasi za wengine na kuanza kulisukuma gurudumu.

Umekwishaiona muvi ya Eternal sinema? Kama hujaiona, kaione, wale ni supeheroes wanaokuja kuchukua nafasi pale Avenger, kuna huyu Shang Chi naye anakuja kuchukua nafasi hapo, kuna Marbius naye pia anakuja, na wataungana na Venom, wote hao watakuja kuunda Avengers na kuwa tishio kama ilivyokuwa kipindi cha nyuma.

Kwa upande wa DC, bado wanajifikiria nini cha kufanya. Mwaka kesho wanakuja kumtambulisha character mpya kwenye muvi, anaitwa Black Adam, nafasi itakayochezwa na Dwayne Jonhson ‘The Rock’. Je, mwamba ataweza kuwarudisha juu kama ilivyokuwa miaka ya tisini?

Tusubiri.

Cha mwisho kumbuka muvi za Marvel zinarekodiwa na SONY, za DC zinarekodiwa na WARNER BROS na zile za James Cameron zinarekodiwa na 21 Century.

MWISHO.

Imeandikwa na Nyemo Chilongani.
 
"Ngoja nikutonye kidogo" ndo basi tena ukazamia!
 
Jamaaa katupiga kamba balaa sema bahati yake mwandishi hayupo humu ngoja nimuache. Ila kwa kuweka mambo sawa..
✔️Zack Snyder sio mwenye sauti kuu DC ni kiongozi kwenye upande wa creativity yaani DCEU. Warner bros ndio wenye sauti na ndio wanasababisha kufeli kwa DC kwakua hawampi full control ya creativity Zack Snyder. Na muvi za DC hua haziigizwi usiku bali ni tone Color tu walio ichagua DC ili kuweka radha tofauti.
✔️ Umempamba Stan Lee lakini ukae ukijua yeye hahusiki kwenye creativity ndio maana hua credited kama Executive producer/Creator
Creativity team ya Marvel inaundwa na Kevin Feige, Victoria Alonso,Lois despacito,Stephen Broussard, Nat Moore,Jonathan Schwartz,Trinh Tran,Bran Winderbaum na kipindi cha nyuma hasa phase 2 alikuwepo Josh whedon
✔️Mpango mzima wa muvi 22 kwa miaka kumi zenye storyline moja umeundwa na vichwa vitatu ambavyo ni Avi Arad, Sami Raim na Kevin Feige ambae ni Boss wa Marvel studios.

✔️ Paragraph yako ya mwiso ndio umeongea uongo mkubwa sana...Looh hadi aibu.
👉 Marvel ilikua haina hela kabisa miaka ya 90 huko so ilikua inauza baadhi ya characters wake ili kuendesha Kampuni. Mfano iliuza Spiderman na Venom kwa kampuni ya Sony, ikauza XMen na Fantastic four kwa 21th Fox yaani marvel inapata kitu kama asilimia 10% tu kwenye mauzo ya hao characters. Mwaka 99 Marvel ilitoa muvi ya Blade hii muvi iliuza kiasi chake na hii ndio pesa zilizopatikana ziliwezesha kuanzisha marvel studio mwaka 2007. Kama kawaida Disney ni wazee wa kunusa hela tu kama walivyoinusa kampuni ya Pixar animation wakaichukua hivyo basi mwaka 2009/10 Disney rasmi iliinunua Marvel studios so Marvel character wote wapo chini ya Disney. Hivyo Boss wa Marvel anapokea naelekezo kutoka kwa CEO wa Disney ambae ni Bob Igler. Disney wenyewe wanachohusika kwenye Marvel studio movies wanakua kama wasambazaji (Distributor)
Hivyo basi Marvel studios ni stand alone studio inayojitengenezea muvi zake hata Bob Igler hahusiki kwenye creativity yeye anapewa taarifa tu kama boss kama kuna promotion na pesa zinatakiwa yeye ndio ana issue

👉Mwaka 2019 rasmi kampuni ya Disney ilinunua kampuni ya 20th Fox na 21th Fox hii ina maana character wa marvel waliopo Fox kaa vile Deadpool,Xmen na Fantastic four wote wapo marvel/Disney. Sio hivyo tu Hata James Cameron yupo chini ya Disney maana muvi zake zote za Titanic na avatar zote zilikua fox sasa zinamilikiwa na Disney.

✔️ WanaBros wao ni wamiliki na wasambazaji wa DC movies

Ngoja niishie hapa maana mwandishi halisi hyupo humu so ni kazi bure kukosoa✌️
 
marvel wako vizuri stori zao zinabamba hata movie unaangalia unaienjoy ila DC nawakubali wanashow za kibabe sana Ichek ile batman and superman

Ila kuishusha marvel ni kazi nguvu hawa jamaa wanajua nini wanafanya R.I.P Stan lee
 
Kwenye Bongo movie yenu kuna vita Gani?..
 
{Baada ya DC kugundua kwamba hawana characters ya comedy, hapo ndipo wakaamua kumleta Flash }

Hahah hivi hizi story umeleta ulikuwa unauhakika na unachokileta kweli au basi tu ufungue thread? Alafu nilichogundua wewe hujui chochote kuhusu comic books hasa za hao MARVEL na DC sababu characters wote wametoka kwenye vitabu mpaka kuwa kwenye screen. Nani alikuambia FLASH ni character wa comedy??😂😂
 
MTU ANAKUAMBIA ETI HAJUI THE FLASH ALITOKA WAPI WAKATI KWENYE ILE SERIE YAKE WANAELEZA VEMA KABISA

ACHA KUWACHAFUA DC KWA MAPENZI YAKO KWA MARVEL
 
Bro, unataka The Dark Knight/Prince of Gotham/King of the Night(in a good way), the fittest among humans, a man amongst gods, the greatest detective, god of knowledge(alipoketi kwenye mobius chair), man of principle, The Batman acheke ili iweye bro?!
Kuhusu weusi wa movies za dc inamaana hujawahi kusoma comics za dc hasahasa za batman au hata kuangalia animation za dc.

Detective Comics.
 
Jamaaa katupiga kamba balaa sema bahati yake mwandishi hayupo humu ngoja nimuache. Ila kwa kuweka mambo sawa..
Zack Snyder sio mwenye sauti kuu DC ni kiongozi kwenye upande wa creativity yaani DCEU. Warner bros ndio wenye sauti na ndio wanasababisha kufeli kwa DC kwakua hawampi full control ya creativity Zack Snyder. Na muvi za DC hua haziigizwi usiku bali ni tone Color tu walio ichagua DC ili kuweka radha tofauti.
Umempamba Stan Lee lakini ukae ukijua yeye hahusiki kwenye creativity ndio maana hua credited kama Executive producer/Creator
Creativity team ya Marvel inaundwa na Kevin Feige, Victoria Alonso,Lois despacito,Stephen Broussard, Nat Moore,Jonathan Schwartz,Trinh Tran,Bran Winderbaum na kipindi cha nyuma hasa phase 2 alikuwepo Josh whedon
Mpango mzima wa muvi 22 kwa miaka kumi zenye storyline moja umeundwa na vichwa vitatu ambavyo ni Avi Arad, Sami Raim na Kevin Feige ambae ni Boss wa Marvel studios.

Paragraph yako ya mwiso ndio umeongea uongo mkubwa sana...Looh hadi aibu.
Marvel ilikua haina hela kabisa miaka ya 90 huko so ilikua inauza baadhi ya characters wake ili kuendesha Kampuni. Mfano iliuza Spiderman na Venom kwa kampuni ya Sony, ikauza XMen na Fantastic four kwa 21th Fox yaani marvel inapata kitu kama asilimia 10% tu kwenye mauzo ya hao characters. Mwaka 99 Marvel ilitoa muvi ya Blade hii muvi iliuza kiasi chake na hii ndio pesa zilizopatikana ziliwezesha kuanzisha marvel studio mwaka 2007. Kama kawaida Disney ni wazee wa kunusa hela tu kama walivyoinusa kampuni ya Pixar animation wakaichukua hivyo basi mwaka 2009/10 Disney rasmi iliinunua Marvel studios so Marvel character wote wapo chini ya Disney. Hivyo Boss wa Marvel anapokea naelekezo kutoka kwa CEO wa Disney ambae ni Bob Igler. Disney wenyewe wanachohusika kwenye Marvel studio movies wanakua kama wasambazaji (Distributor)
Hivyo basi Marvel studios ni stand alone studio inayojitengenezea muvi zake hata Bob Igler hahusiki kwenye creativity yeye anapewa taarifa tu kama boss kama kuna promotion na pesa zinatakiwa yeye ndio ana issue

Mwaka 2019 rasmi kampuni ya Disney ilinunua kampuni ya 20th Fox na 21th Fox hii ina maana character wa marvel waliopo Fox kaa vile Deadpool,Xmen na Fantastic four wote wapo marvel/Disney. Sio hivyo tu Hata James Cameron yupo chini ya Disney maana muvi zake zote za Titanic na avatar zote zilikua fox sasa zinamilikiwa na Disney.

WanaBros wao ni wamiliki na wasambazaji wa DC movies

Ngoja niishie hapa maana mwandishi halisi hyupo humu so ni kazi bure kukosoa

Phase iliyopita Joss Whedon alisema Avengers zile mbili specifically ya Pili ambayo ni Age of ultron ilimchosha haijawahi kutokea alikuwa anafanya kazi usiku mchana alichoka kiasi sio cha kawaida, mwili wote ulikuwa unamgomea mzee wa watu.

Eternals: Spoiler alert
Eternals post credit Imetoka sauti ambayo watu wanasema inasemekama kuwa ni ya Blade kwahiyo siku za usoni atakuja Black Night, Blade na Mutants watakuwa introduced pia ndani ya MCU maana copyrights kwa Fox ndio tushachukua hivyo binafsi naona DC wameshaachwa mbali sana

Hata hiyo Black adam ya DC itakuwa ni Flop tu, naweza nkawa sipo sahihi ila DCEU sikuhizi wamepoteana kbs
 
Phase iliyopita Joss Whedon alisema Avengers zile mbili specifically ya Pili ambayo ni Age of ultron ilimchosha haijawahi kutokea alikuwa anafanya kazi usiku mchana alichoka kiasi sio cha kawaida, mwili wote ulikuwa unamgomea mzee wa watu.
Phase iliyopita ilikua ni phase 3 now 4. Avge of ultron ipo phase 2
Joss whedon mwenyewe anasema yeye ni workholic akianza kazi kaanza ndio maana Cast ya Justice League akiwemo Josson momoa,Ray fisher, Gal gadot wamekua wakimtuhumu kua anawafanyia harassment wanapokua kwenye kuigiza.
But kwakweli Avangers an Ultron ni muvi amabazo Joss kazisuka vyema kuanzia directing hadi dialogue (screenplay)
Nadhani kinachomchosha ni kwakua hua anadirect na kuandika mwenyewe script
Phase 2 yote yeye alikua kama Consultant Director ndio maana kuanzia Thor dark world,Winter soldier,First avenger, Thor zote kuna mkono wake
Eternals: Spoiler alert
Eternals post credit scenes Imetoka sauti ambayo watu wanasema inasemekama kuwa ni ya Blade kwahiyo siku za usoni atakuja Black Night,
Hapana Ule upanga alioushika Dane Whitman kwenye Comics pia hua unatoa sauti na sio yeye pekee aliyewahi kuutumia. Wamefanya twisting kumu introduce Blade lakini pia mbona muvi ya balde ipo Kwenye development muda mrwfu tu sema tu kumyo Merhashala ali hakuna actors wengine waliokua confirmed. Btw naona instructions iliyomo kwenye eternal ni ya mdogo wake thanos pekee Eros starfox
Blade na Mutants watakuwa introduced pia ndani ya MCU maana copyrights kwa Fox ndio tushachukua hivyo binafsi naona DC wameshaachwa mbali sana
DC upande wa film inabidi wafanye transformation kubwa sana kuanzia huko kwenye parent company WB.
X men soon wanaingia MCU ndio maana mwendelezo wa Xmen movies umesitishwa ili character warudi nyumbani tumeanza na Deadpool na Fantastic 4
Hata hiyo Black adam itakuwa ni Flop tu, naweza nkawa sipo sahihi ila Dc sikuhizi wamepoteana kbs
Hua sipo excited na muvi za DC na sababu kuu ni Warner Bros ndio wanawavurugia creativity team ya Zack Snyder. Ngoja tuone labda inaweza kua much interesting kama Aquaman
 
Back
Top Bottom