Vita dhidi ya ushoga: Waziri Gwajima amechagua silaha kali au butu?

Vita dhidi ya ushoga: Waziri Gwajima amechagua silaha kali au butu?

Kwenye katiba mpya tunaweka sheria ya mashoga na mabasha zao na wasagaji wanyongwe mpaka kufa. Uone kama kuna mtu atasogeza trako kwa mwenzie
Hahaha,
Shida ni kuwa mchakato wa Katiba mpya ukiongozwa na ccm, matakwa, mapendekezo na matamanio ya wananchi hayatakuwa na nafasi. Ile Rasimu ya Katiba ya Warioba imesheheni maoni na matamanio ya umma wa wananchi wengi, lakini wahuni hawaitaki !!
 
Ushoga unaongezeka mitandaoni
Mimi huku mitaani sioni mashoga, ila nikija JF nakuta malalamiko juu ya ushoga in real life. Binafsi sijawahi kuwaona mashoga in real life lakini nawaonaga mitandaoni wanavyojadiliwa
Wewe kutowaona mitaani haimaanishi kuwa hawapo, pengine shughuli zako zinakunyima nafasi ya kuchangamana na watu au wewe sio mtu wa kujichanganya

Mtaani wapo tena hali ni mbaya kuanzia kwa watoto wadogo wa shule ( hili kundi linatisha zaidi, ongea na walimu utayajua mengi) hadi vijana mtaani na wengine wamejificha kwenye vivuli vya watoto.

Wapo waliobahatika kupata watoto mapema (wale wenye uwezo wa kushiriki na mwanamke) hawa utawaonea huruma wakiwa wanajitetea kwa kigezo cha watoto na kwa namna kubwa hawa ndio hutumika zaidi kutengeneza mashoga wengine kwasababu wanaouwezo wa kuwageuza wenzao. Hii ni project iliyokaa kimkakati muulize Mwakyembe kwanini harakati zake zilizimika ghafla?
 
Hahaha,
Shida ni kuwa mchakato wa Katiba mpya ukiongozwa na ccm, matakwa, mapendekezo na matamanio ya wananchi hayatakuwa na nafasi. Ile Rasimu ya Katiba ya Warioba imesheheni maoni ya wananchi lakini wahuni hawaitaki !!
Na ndomaana wanatuletea tujadiliane mambo ya kichoko ili kuzuia msishushe nondo kama hizi. well said
 
Wewe utafanya lolote ili mjadala wako wa ushoga uweze kujadiliwa na kupewa kipaumbele bila kujali uhalisia.
Kama umepitia comments zangu hapo juu, mimi napinga mijadala kama hii. Naona wanatuletea haya mambo ili tusizungumzie vitu vya msingi. Huyo waziri wenu analeta kiki tu, Tulisha fika kuongelea katiba mpya, wewe ndo umeturudisha nyuma tena.
 
Kama kuna jambo linakera watu wenye akili timamu ni kuona mashoga wanazidi kuongezeka katika jamii lakini pia agenda yao kupenya kirahisi sana na kubebwa na watu mashuhuri

Hivi karibuni ushoga umezungumzwa sana. Ukifuatilia mijadala unaweza kupandisha kisukari kama unaroho nyepesi kwa namna baadhi ya watu mashuhuri wanavyolichukulia jambo hili hasa hasa wanawake, japo swali pekee la msingi ambalo kwa asilimia kubwa linaonekana kuwakera linaulizwa na wanaume la "kama wao wangependa watoto wao wawe kama hao wanao watetea". Wakiambiwa hivi wanakasirika ukijuiliza wanakasirika nini wakati huo huo wanawatetea unashindwa kuelewa

Binafsi naelewa ukubwa wa swala la ushoga. Kwa uzoefu wangu uliotokana na kuchangamana na vijana umeniwezesha kujua kwanini hao wanaojianika mitandaoni wanapata wapi ujasiri

Hawa wapuuzi wako kimkakati sana. Kiufupi wameshatuweka mateka katika hili swala na tusipochagua siraha makini tutaendelea kuwatumikia kwa kuwasaidia ku "push" agenda yao huku tukidhani tunapambana nao

Tusichoelewa ni kwamba mashoga wenyewe pamoja na "mashoga" zao wanapenda wajadiliwe (kama hivi). Hili kwao tayari ni ushindi hivyo siraha yoyote inayowaleta kwenye jamii inakuwa butu tayari

Shuleni siku hizi kuna watoto wengi mashoga! Cha ajabu hao watoto wakibahatika kujulikana mara nyingi taarifa zinatoka kwa watoto wenzao, kisha Walimu huwataarifu wazazi, wazazi wakiwa waelewa wanalipeleka kwa watu wa ustawi, likifika ustawi polisi nao huingia kati na hatua ya mwisho huwa ni kupelekwa hospitali kupata uthibitisho wa kitabibu baada ya hapo file linarudishwa kabatini kwa kujipa matumaini ya kumnasihi na kumfuatilia mtoto kisha mtoto anarudi shule kuendelea na masomo kwa "matumaini" kwamba ameshauriwa na sasa ataacha tabia hiyo, mtoto anamaliza shule anaingia mtaani au wengine wanaendelea na masomo ya juu na hatimaye wengine wanaingia maofisini kulitumikia Taifa

Kosa kubwa sana lipo hapa kwenye kuweka haya "matumaini" ya kuwa unasihi aliopewa umembadilisha bila kujiridhisha na hapa ndipo tunapotakiwa kuchagua siraha sahihi kwasababu wapo kweli wanaobadilika lakini wapo wengi wanabaki vile vile

Hawa wanaojianika mitandaoni ukifuatilia kwa undani utakuta shule aliyosoma walikwisha mgundua mapema tu na uongozi wa shule ulifuata hatua zote nilizozieleza hapo juu lakini mtoto aliporudi shuleni kuendelea na masomo hizo mamlaka zilijiaminisha kuwa amebadilika pasipo kuwa na uhakika

Ni kweli kabisa kesi nyingi sana za kuwaharibu watoto wa kiume kwa kuwafira ( hili ndilo neno sahihi, anayefanywa kinyume na maumbile ni mwanamke, mwanaume akifanyiwa inaitwa ufiraji! Hapa pia kuna kosa linafanyika kwa kivuli cha kupunguza ukali wa maneno kitu ambacho sio sahihi, dhambi haitakiwi kuonewa aibu inapokemewa).

Kesi nyingi unakuta chimbuko lake liko ndani ya wanafamilia. Kama sio kaka atakuwa mjomba, Baba mdogo au ndugu wa karibu na mara kadhaa utakutana na kijana wa jirani, "ma anko" wa mashuleni au sehemu za ibada hali inayopelekea familia kushindwa kufanya maamuzi sahihi ya kisheria kushughulika na huyu aliyemuharibu kwa mara ya kwanza na akaendelea kumzoesha kuona ni jambo la kawaida

Mara kadhaa nimeshuhudia kesi za aina hii za moja kwa moja ambapo mtoto anasimulia alikuwa akifanyiwa na kaka yake mkubwa, kisha akazoea halafu ikafikia hatua hawezi tena kufanya na kaka yake hivyo inabidi awashawishi watoto wengine wamfanyie.

Simulizi kama hizo ukija huku chini kwenye jamii hasa hasa shule za msingi na sekondari utakutana nazo nyingi mpaka utashangaa mwenyewe na utaumia zaidi utakaposikia mtoto wa miaka 12+ amekwishazoea kufirwa kiasi kwamba anafikia hatua ya "kuwatongoza" vijana kwa kujilengesha ili wamfanyie huo upuuzi na hawa vijana wanaofanya huo upuuzi wako mitaani

Kundi lingine la hawa mashoga liko kwenye hizi saloon za kike. Huko wamejazana wengi sana waliojificha kwenye kivuli cha kujipatia riziki kama hao wafanyabiashara anaopambana nao waziri Gwajima. Ukilichimba hili swala kisukari na presha havikuachi salama kwasababu hali ni mbaya sana. Hapo hatujaangazia kwenye hizi media house, wasanii, taasisi mbalimbali, vyama vya kijamii, serikalini na hata kwenye chama mojawapo kikubwa cha siasa

Ndiomaana ninapo muona waziri Gwajima anapambana na hawa watu mitandaoni najiuliza kama kweli hiyo siraha aliyoichagua itatuvusha kweli? Ni kweli hizi taarifa za huku yanakoanzia, huko mawizarani haziwafikii? Wamezifanyia tafiti kujua kwanini kila siku zinazidi kuongezeka badala ya kupungua?

Hawa watendaji wa huku chini linakoanzia wamewawezesha kiujuzi na kiuwezo kushughulika nalo ili wao wanapolidhibiti huko mitandaoni na hawa wachini walidhibiti lisiendelee kukua?

Uhalisia ulivyo, hawa mnaowaona wanawatetea huko mitandaoni watu kama hao ndio wanaolikwamisha kuthibitiwa pia huku chini

Waziri anapopamba na hao watu, ameshaweka mkakati madhubuti wa kushughulikia hoja za wanaompinga kwa maneno ya kuwafariji wahanga kama:-

"...acheni kuwasema vibaya hamjui kwanini wako hivyo; au kama ndivyo alivyozaliwa unataka yeye afanyeje? au unafikiri yeye amependa kuwa hivyo muacheni aishi anavyotaka au kwani wanaowafanya wao wamefanywa nini... na maneno mengine kedekede yanayowatia moyo wenye tabia hizo lakini yanayowakatisha tamaa wanaochukia na kupambana na ushoga?

Je, Waziri amejiuliza kwa undani hawa watu wanapata wapi ujasiri wa kujibizana naye mitandaoni? Katika hali tuliyonayo kwasasa, mtu mwenye viashiria vyote vya ushoga anawezaje kupata confidence ya kujibizana na waziri kimafumbo mafumbo mitandaoni bila back up! Waziri ana uhakika atazishinda hizo back up za hao watu?

Binafsi napata mashaka sana nikitazama kuanzia huku chini linakoanzia na namna mamlaka za huku chini zinavyoshughulika nalo kisha nikitazama huko juu lilivyo na linavyozidi kuwa kubwa na namna mamlaka za huko juu zinavyoshughulika nalo, wasiwasi wangu upo kwenye siraha zinazochaguliwa kama zina uwezo kweli wa kumuangamiza adui au zinakoleza moto pasipo mamlaka kujua na hatimaye kulifanya jambo lizidi kuwa kubwa?

Tuzisaidie mamlaka kuchagua siraha sahihi, wanaoangamia ni sisi kama Taifa
Wasalaam sana ndugu yetu @kiranjawajamii.
Nakupongeza kwa andiko lako ambalo hakika ni jema na lina mashiko. Nami nikasema, acha nichangie mada hii. Awali ya yote, niseme hivi, kama mama mtu mzima kabisa na kiongozi, mmomonyoko wa maadili wa sura zote kama ilivyo kwa wengine wote nami unanikera sana maana ndani yake hakuna hata utukufu wa Mungu. Ndiyo maana Serikali pia inatekeleza programu za malezi na makuzi ambazo, zingine ziko kwenye eneo ninalosimamia.

Kuhusu vita hii eneo hili uliliandika, tafadhali jamii msiniachie hii vita na mkaipa jina kuwa ni vita yangu na kundi hili la mashoga na nyie mkajitoa mkadhani eti labda mimi nanufaika au napata hasara binafsi huku jamii mkiwa pembeni kutazama pambano.

Ijulikane kuwa, hii ni vita yetu sote mimi naratibu tu wadau wote mje uwanjani. Majukumu ya jamii yapo na ya kisheria yapo. Jamii ikijua wajibu wake kuwa ni kukataa kutoa ushirikiano kwenye harakati za wabomoa maadili basi tunashinda mapema. Hii hatua inaitwa social suctions. Huwezi jamii ikawa inawapa ushirikiano kwa kuwa promoti mambo yao mitandaoni na kuwaalika na kushiriki shughuli zao na kuacha kufanya malezi na makuzi sahihi kisha mtu akadhani eti waziri au Serikali peke yake itashinda. Tushirikiane.

Sauti yangu ionekane kuwa ni mwanzo wa wito wa wote kushirikiana kwenye kulinda maadili kila mmoja kwa nafasi yake. Pia, ni sauti ya Elimu ili ilibidi wahusika wabadilike, pia ni sauti ya kukumbusha kuwa pamoja na Sheria kuhitajika kufanya kazi bado tunao wajibu wa kuwasaidia watoke huko walikojiingiza au kuingizwa bila kupenda au kujua na kuzuia wengine kuingia huko.

Hivyo, njia zote tutumie kulinda na kuokoa jamii yetu. Naendelea kupokea maoni maana, kazi ni yetu sote na siyo ya mtu binafsi kwa manufaa yake peke yake.

AHSANTE SANA 👋
 
Kama umepitia comments zangu hapo juu, mimi napinga mijadala kama hii. Naona wanatuletea haya mambo ili tusizungumzie vitu vya msingi. Huyo waziri wenu analeta kiki tu, Tulisha fika kuongelea katiba mpya, wewe ndo umeturudisha nyuma tena.
Wewe Mimi kiki ya Nini? Hakuna kiki Mimi ilishanisaidia kufika hapa nilipo na siamini kwenye kiki ingawa wewe kwa kuwa umezoea hivyo, basi unadhani kila mmoja anatumiaga kiki. Namfanya kazi yangu na hiyo ya katiba nenda kwa Waziri wa katiba na Sheria maana wiki iliyopita tu katoa tamko la mwelekeo. Ahsante
 
Kabisa kwa asilimia kubwa ili hili swala lionekane limevaliwa njuga ni lazima kwanza viongozi serikalini waliwekee mjadala huko wao kwa wao waone kwanza kama wao wenyewe wako kitu kimoja? Miongoni mwao hakuna mapandikizi yaliyopandikizwa kukwamisha juhudi?

Huko watapata jibu sahihi litakaloonyesha picha halisi ya ukubwa wa tatizo litakalowasukuma kuliwekea nguvu kubwa ya kisheria vinginevyo kwa mwendo huu hatufiki badala yake wanaume wataanza kuoneana wivu
Katika vita hivi, wewe chukua nafasi yako kama mwanajamii. Kero zote ziko kila mtaa na jamii inaweza kabisa kusema hili hatutaki kwa mifumo ya kijamii bila hata kuvunja Sheria. Hili la jamii kusema sijui kaeni huko Serikalini mjiulize, ni hoja ya kudhani jukumu hili ni la Serikali tu na mifumo ya kijamii Haina nafasi. Huko Serikalini wanakuja watu waliotokana na jamii hii hii. Tubadilike
 
Wewe Mimi kiki ya Nini? Hakuna kiki Mimi ilishanisaidia kufika hapa nilipo na siamini kwenye kiki ingawa wewe kwa kuwa umezoea hivyo, basi unadhani kila mmoja anatumiaga kiki. Namfanya kazi yangu na hiyo ya katiba nenda kwa Waziri wa katiba na Sheria maana wiki iliyopita tu katoa tamko la mwelekeo. Ahsante
Tutafurahi sana kama juhudi zako zitazaa matunda, pale tutakapoona mkono wa sheria ukipita juu ya hawa watu na wakatoweka mitaani. Maana wamekua kero sana mpaka tunakosa namna Nzuri ya kuishi huko mitaani.
 
Tutafurahi sana kama juhudi zako zitazaa matunda, pale tutakapoona mkono wa sheria ukipita juu ya hawa watu na wakatoweka mitaani. Maana wamekua kero sana mpaka tunakosa namna Nzuri ya kuishi huko mitaani.
Mnaishi mitaa gani ambayo sisi wengine hatuyaoni hayo mambo ni nyie tu mnayaona??
 
Katika vita hivi, wewe chukua nafasi yako kama mwanajamii. Kero zote ziko kila mtaa na jamii inaweza kabisa kusema hili hatutaki kwa mifumo ya kijamii bila hata kuvunja Sheria. Hili la jamii kusema sijui kaeni huko Serikalini mjiulize, ni hoja ya kudhani jukumu hili ni la Serikali tu na mifumo ya kijamii Haina nafasi. Huko Serikalini wanakuja watu waliotokana na jamii hii hii. Tubadilike
Hakuna vita yoyote.
You can't solve a problem that doesn't exist.
 
Wewe Mimi kiki ya Nini? Hakuna kiki Mimi ilishanisaidia kufika hapa nilipo na siamini kwenye kiki ingawa wewe kwa kuwa umezoea hivyo, basi unadhani kila mmoja anatumiaga kiki. Namfanya kazi yangu na hiyo ya katiba nenda kwa Waziri wa katiba na Sheria maana wiki iliyopita tu katoa tamko la mwelekeo. Ahsante
Ushoga ni ukosefu wa maadili, kama nyie wenyewe viongozi mnaingia madarakani kwa kufanya mauaji ya kutisha, mnapata wapi nguvu ya kusema mnapinga ushoga? Kwanza mjiangalie mko madarakani kwa kufanya mauaji ya kiwango gani, hapo uwezo wenu wa kimaadili utakubalika. Si jitihada mbaya unafanya ili isionekane unachukua mshahara wa bure, lakini kuua ili ukae madarakani ni mbaya kuliko hata huo ushoga ambao wengi wanafanya kwa hiari. Inshort nyie ni wauaji mnaotaka kujifanya mna maadili.
 
Back
Top Bottom