Vita dhidi ya dawa za kulevya ianzie bungeni

Deo Meck Mbagi

JF-Expert Member
Apr 19, 2015
360
525
VITA YA DAWA IANZIE BUNGENI

Bunge ni mhimili muhimu sana kwa ustawi wa Taifa. Na ni jukwaa muhimu kwa niaba ya Watanzania wote.

Ila ni mara nyingi wabunge wametuhumiwa kupokea rushwa ili kupitisha agenda zisizo na faida kwa umma au kukwamisha mambo yenye maslahi kwa umma.

Wakati wa serikali ya awamu ya tatu, kulikuwa na maambukizi makubwa ya virusi vya UKIMWI, baada ya serikali kuunda TACAIDS kampeni mubashara iliendeshwa. Na moja kama njia za kuhamasisha umma ujitokeze kupima wabunge walitakiwa kuwa mfano na kupima.

Siku ilipofika waliojitokeza walikuwa ni mawaziri pekee, wabunge karibia wote walichimba. Baadae ilitolewa ripoti ya mawaziri walio positive na negative. Ikasaidia umma nao kuhamasika kupima.

Kuna mifano mingi ya operesheni ambazo ziliharibikia bungeni sio kwa maslahi ya umma bali ya watu wachache.

Watuhumiwa wa unga kama wahalifu wengine hawatumii taratibu fulani kufanya uchafu wao bali huangalia matokeo ya wanachohitaji, suala muhimu ni kufanikisha zoezi la kuwatia nguvuni vyovyote iwezekanavyo.

Katika vita ya dawa za kulevya iliyotangazwa na RC wa DAR, Ndugu Makonda tumeona jinsi baadhi ya wabunge walivyoichukulia personal na kutetea baadhi ya washukiwa, sio wote. Hivyo ni dhahiri sio suala la utaratibu bali watu wenye maslahi nao.

Kabla ya operesheni kuna watu walilalamika na kutoa picha za waathirika, sanasana wasanii wakilaumu serikali kuwa inashindwaje kuwakamata wauzaji wakati wateja wanajulikana?

Serikali ikafanyia kazi ushauri huo, ilipowataja wasanii walewale, watu walewale waliokuwa wameibua hoja hiyo wakabeza kuwa waliotajwa ni vidagaa na wanataka mapapa.

Wanaoshukiwa ni mapapa walipotajwa sasa ndipo MAPOVU ya OMMO grade 1 yalipoanzia bungeni hadi mtaani, huku watu wakibinafsisha tuhuma au kutajwa kwa mtu na taasisi yake, kiongozi wa timu akijificha kwa wanachama wake, Mchungaji kwa waumini na wanasiasa mwavuli wa chama.

Kama mnafikiri mapapa ni furu basi mtasubiri sana, tunashindwa kujua kwamba sote ni binadamu na yote yanawezekana, na hapa ndipo unagundua kwa uwezo huu mdogo tu wa kupambanua mambo na kuishia kuwa mashabiki nchi ina safari ndefu sana kuendelea.

Nikirudi bungeni ambapo ndipo kulipaswa kutoa Mwanga na kusaidia wananchi wa kawaida nako wamekuwa kama na uwezo wa chini sana either kwa uelewa au kwa maslahi yao na watu wanaowatetea.

Njia rahisi ya kupambana na madawa, na kweli wabunge kama hawahusiki kama watumiaji au wauzaji na kwa niaba ya kusaidia watu wanaowawakilisha na kama sehemu ya vita dhidi ya biashara ya madawa ya kulevya basi wapitishe azimio wabunge wote wapimwe kama wanatumia dawa za kulevya na watakaobainika wawataje wanaowauzia.

Kama sheria inavyosema, mahakama pekee ndio yenye uwezo wa kumtia mtu hatiani, nguvu kubwa ya kupinga inatia wasiwasi huenda unahusika au unawajua wahusika.

NB: WABUNGE WAWE WA KWANZA KUPIMWA, NDIO MSINGI MKUBWA WA HOJA YANGU.
Deo Meck
 
naunga Mknono asilimia Mia moja! Nimepata shaka mnoooo na Bunge hili! Maana povu lile halikuwa la kawaida! Hii ndio Tanzania?!??!?!?!?!?! Tulipofikia?!?!?!?!!?
 
baadhi ya wabunge waliwahi kusikika kuisifu bange na kuomba iruhusiwe kwani kwa maoni yao eti inatija kwenye uzalishaji mali, sasa ukiwa na wabunge wenye mawazo hayo vita dhidi ya madawa ita pata uungaji mkono kweli?
 
Dunia nzima inajulikana wale watenda madhambi au wafanyabiashara wakitaka kulinda mali au vitu vyao huwa wanapenda kuingilia bungeni ili kupata nafasi ya kuwa karibu na serikali japo bunge ni mihimili unaojitegemea lakini ni muhimili ambao watu wa serikali wanautumia sana

Na mapambano ya kweli huwa yanaanzishwa na serikali si Bunge hakuna mapambano ambayo alianzishwa na Bunge yakafanikiwa bila ya support ya serikali kwani Bunge kazi yao ni Kutunga sheria tu kazi ya kutafasiri sheria ni kazi ya mahakama kazi ya kutekeleza sheria ni Kazi ya serikali

So siwezi kushangaa leo Bunge kutetea wahalifu na wauza unga kwani ndio sehemu ambayo mtu yeyote anaweza kuingia tu akiwa na fedha ,hakuna vetting kama vile serikalini au mahakamani ukiona sehemu ambayo wanasema mtu yeyote tu anaweza ingia basi jiandae kupokea vilaza,majambazi,magaidi,wenye elimu,wasio na elimu na wote interview ni kushinda uchaguzi tu .hakuna cha vetting kujua hawa wanaoingia ni watu gani au wanajihusisha na nini kabla ya kuingia hapa ndo maana tunaona wakina Msukuma watu waliokuwa ............... wapo Bungeni leo
 
U kweli mtupu
 
baadhi ya wabunge waliwahi kusikika kuisifu bange na kuomba iruhusiwe kwani kwa maoni yao eti inatija kwenye uzalishaji mali, sasa ukiwa na wabunge wenye mawazo hayo vita dhidi ya madawa ita pata uungaji mkono kweli?

Mbunge mwingine alisema watumiaji sijui Wa uzaji ( sijumbuki vizuri) wamo ndani ya bunge kama akipata ridhaa yamwenyekiti awataje !! Cha kushangaza hakupewa ridhaa huyo!!!
 
baadhi ya wabunge waliwahi kusikika kuisifu bange na kuomba iruhusiwe kwani kwa maoni yao eti inatija kwenye uzalishaji mali, sasa ukiwa na wabunge wenye mawazo hayo vita dhidi ya madawa ita pata uungaji mkono kweli?

Tena ndiyo mpingaji mkubwa huyo Msukuma, ameacha hoja anamshambulia Makonda!! Kwa faida ya nani??!
 
Tena ndiyo mpingaji mkubwa huyo Msukuma, ameacha hoja anamshambulia Makonda!! Kwa faida ya nani??!
Shangaa, na uchaguzi ujao ninasikia atagombea na huenda akashinda,huko (bugando geita) mbunge mzuri ni yule anayeleta chumvi huwezi kumpa mtu kura hivi hivi kwani yeye anaenda kula vingapi huko bungeni,
 
Ianze bungen sambamba na ikulu, wafanyakaz wote wa ikulu wapimwe, wale w a jamii ya siri za intelijensia pamoja na wavaa kofia nyekundu, tuone, sio mnasakama bunge tu
 
Back
Top Bottom