Visima vya Mzee Sabodo viko wapi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Visima vya Mzee Sabodo viko wapi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by FJM, May 9, 2011.

 1. F

  FJM JF-Expert Member

  #1
  May 9, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Mwishoni mwa mwaka jana tulimwona na kumsoma Mzee Sabodo kwenye vyombo mbalimbali vya habari kuwa ametoa msaada ili kufanikisha uchimbaji wa visima wa maji.

  Takribani visima 700 na kama sikosee ilikuwa walau kila Wilaya ipate kisima. Baadae kidogo Prof. Mwandosya alienda kumshukuru Mzee Sabodo kwa msaada wake na alipewa nyongeza ya visima 10 - hivi vikiwa mahsusi kwa eneo analotoka Mwandosya.

  Sasa, kuna mtu yeyote anajua nini kimefanyika?

  Kazi imeanza?

  Na kama imeanza vi wapi visima?

  Kama bado kwa kwanini?
   
 2. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #2
  May 9, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Wewe uko wapi?
  unatumia visima?
  maana usije kua una uliza viko wapi wakati huko uliko
  unatumia maji ya bomba 24/7,...
  walio ahidiwa wanajua mchakato ulipo fikia,..
  After all,sobodo hadaiwi na mtu kwamba akishindwa kuchimba atashitakiwa!

  Nilitegemea utauliza,meli alizo ahidi kikwete ziko wapi?
  kigoma imesha kuwa kama dubai?
  machinga complex nyingi dar ziko wapi?
  maisha bora yako wapi?

  Msimsumbue sobodo wa watu,akitaka atachimba asipotaka ataacha na
  hana deni!
   
 3. F

  FJM JF-Expert Member

  #3
  May 9, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145

  @ Speaker nimeuliza hili kwa sababu nina wasiwasi Prof. Mwandosya anaweza akawa anatekeleza kwa utashi wa kisiasa. Kwamba visima vinaweza kuchimbwa kwenye majimbo yanayoongozwa na ccm tu! upo hapo?
   
 4. t

  tufikiri Senior Member

  #4
  May 9, 2011
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 156
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mbona huhoji na zile alizowapa CDM wamefanya nini?
   
 5. F

  FJM JF-Expert Member

  #5
  May 9, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145

  Zilikuwa kusaidia elimu ya uraia nadhani hata wewe mwenyewe utakubali 'ILMU' inanoga i.e magamba na sasa watu wako Dodoma kwa semina elekezi. na bado!
   
 6. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #6
  May 9, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Mimi huwa nachoka kabisa nikiona kiongozi tena wa serikali anaongelea visima maeneo kama ya ilala, mwanza mjini ,bukoba ,musoma

  Yanii nikiona watu wa mjini wanaongela visima najiuliza wale wa mwanerumango singida na dodoma waongelee nini?
   
 7. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #7
  May 9, 2011
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,109
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Tuko mwezi wa tano tu baada ya yeye kuaidi sasa mnataka yeye aanze kuchimba bila mipango!!!. Vitu vinachukua muda hasa kama pesa ni ya mtu binafsi maana hataki pesa iende kwa mafisadi wa serikali tena. Anataka kusimamia mwenyewe visima!! Mpe muda ni pesa yake na atafanya kwa muda wake hili sio deni kwa mtu yeyote na Watanzania wengine mnatakiwa kujitolea badala ya kupiga domo siku nzima
   
 8. boma2000

  boma2000 JF-Expert Member

  #8
  May 10, 2011
  Joined: Oct 18, 2009
  Messages: 3,283
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  kwani hujui mbona jibu ni rahisi UFISADI
   
Loading...