visasi, visirani, hasira kuikwamisha Tanzania ya viwanda

falcon mombasa

JF-Expert Member
Mar 5, 2015
9,189
9,298
wakuu hadi sasa hali ndio kama mnavyoiona, visasi na visirani ndio vimetawala serikali ya awamu hii ya tano.
nimetoka kudokezwa hapo lumumba kuwa ni kweli kuna baadhi ya wanalumumba wenye nyadhifa kwenye chama na serikali wameanza kampeni za chini kwa chini kusaka urais 2020.
hii inatokana na wanalumumba wengi kujikuta wanaongozwa kibabe na mtu mmoja. kumbe wanalumumba wengi walitegemea serikali ambayo watakaa na kushauriana nayo badala yake kila kitu kinapelekwa kiubabe. mbaya zaidi chama cha mapinduzi kwa sasa hakina pesa sababu wadhamin wake wakubwa wote wako kwenye sintofahamu na muheshimiwa. Lakini pia kwa mtazamo wa kawaida ni dhahiri nchi ilipofikia sasa kila siku ni madai ambayo chanzo chake ni visasi visirani hasira za mheshimiwa dhidi ya watu aliowahi kushirikiana nao kabla ya hapa. mtazamo wangu nionavyo ile ahadi ya kuwa na Tanzania ya viwanda itaendelea kutekelezwa na mataifa mengine huku tanzania ikiendelea kulipa visasi. chuki visasi visirani ni adui wa maendeleo ni muhimu watanzania waamke waungane wapige vita vitu hivyo.
 
Back
Top Bottom