Visanga vya ukweli na uwazi baaina ya mimi na wachungaji

Visanga vya ukweli na uwazi baaina ya mimi na wachungaji

Dogoli kinyamkela

JF-Expert Member
Joined
Nov 21, 2024
Posts
2,144
Reaction score
3,459
MIMI: Maandiko yanaonesha kuwa
Adam alikuwa na watoto
‎wawili:
1769166839655.jpg
‎Kaini na Habili.

CARDINAL: ndio, Alikuwa na Watoto
wawili.

MIMI: Hakuna moto mwingine
anayetajwa kuwa
‎alijichomeka katikati ya hao
‎wawili!

CARDINAL: Haswaa, walizaliwa wawili.
Kaini ndo mkubwa, Habili
‎ndo mdogo.

MIMI: Kaini alimuua ndugu yake
akiwa mtoto ama mtu mzima?

CARDINAL: Akiwa mtu mzima. Kwa
mazingira yanayoelezewa,
‎alikuwa mtu mzima..

MIMI: Je Baada ya kumuua Habili,
Adam alikaa muda gani hadi
‎kupata Mtoto mwingine?

CARDINAL: Baada ya kifo cha Habili,
Adam alikaa miaka 130 ndipo
‎akamzaa mwana mwingine
‎mwenye sura na muonekano
‎wa Adam, akamuita SETH.

MIMI: Kwa miaka 130, imeandikwa
kuwa adam alikuwa na binti
‎yeyote kabla ya kuzaliwa kwa
‎Seth?

CARDINAL: Hapana, haikuandikwa, ila
kumbuka kuwa wanawake
‎walikuwa Hawahesabiwi
‎kipindi hiko? Kwa hiyo,
‎inawezekana hapo katikati
‎Alikuwa anapata tubinti, ila
‎baada ya miaka 130 ndipo
‎akapata mwana wa kiume!

MIMI: Hebu nisomee mwanzo 5:4.

CARDINAL: Maandiko yanasema:
Mwanzo 5:4
[4]Siku za Adamu baada ya
‎kumzaa Sethi zilikuwa miaka
‎mia nane, akazaa wana,
‎waume na wake.

MIMI: Mbona umesema kuwa mabinti
walikuwa hawahesabiwi?
‎Umeona mabinti walitajwa?

CARDINAL: Ndio naona.

MIMI: Wametajwa kuwa walizaliwa
baada ya Seth kuzaliwa ama
‎kabla ya Seth kuzaliwa?

CARDINAL: Ni baada ya Seth kuzaliwa.

MIMI: Ilikuwa imepita miaka mingapi
tangu Kifo cha habili hadi
‎kuzaliwa kwa Seth?

CARDINAL: Kwa Mujibu wa Simulizi za
Biblia ni kuwa baada ya kifo
‎cha Habili, Adam alikaa miaka
‎130, ndipo akampata Seth.

MIMI: Na mabinti wakazaliwa baada
ya miaka 130, sivyo?

CARDINAL: Ndio, tukifuata kihalali
maandiko, Walizaliwa baada
‎ya hiyo miaka..

MIMI: Unataka kuniambia kuwa kwa
muda wa miaka 130 kaini
‎alikuwa Hana hata kadem?
‎Unamaanisha alienda kukaa
‎mwituni akila nyeto tu bila
‎hata katoto ka elfu mbili?

CARDINAL: Dah, hili swali ni zito, ila
kiukweli inaonesha wazi kuwa
‎kulikuwa na jamii nyingine ya
‎watu. Maandiko yanaonesha
‎dhahiri kuwa baada ya
‎kuondoka pale, alienda nchi
‎Ya Nod ( ugenini) mahala
‎ambapo huko alipata mke na
‎kuzaa watoto. Hii ilifanyika
‎ndani ya miaka 130, na si
‎baada.

MIMI: Hii jamii ilitoka wapi?

CARDINAL: Nakuibia siri, ila usiende
kuhubiri huko tusije kosa
‎ waumini, maake nakufahamu.
‎ huwa hauna siri. Hili neno
Nod, ni neno linalomaanisha
‎kutangatanga, lakini hapo kale
‎lilimaanisha Nubia. Kwa hiyo,
‎ngozi nyeusi imekuwapo hata
‎kabla ya uumbaji wa huyu
‎Adam. Hata hivyo historia
‎yake imefukiwa fukiwa ili
‎isifahamike hadi leo.
‎Anadhani alitoka kwa Adam.
‎Ningependa Wanaotaka
‎kujuwa historia yao Wasome
‎hadithi za Dogon Kuhusu
‎chimbuko la mtu mweusi.

MIMI: Dah, unaonekana wewe ni
muungwana sana.
‎Ningekutana na Kina fulani
‎hapa, ningekuwa
‎nishatimuliwa. Je Unadhani
‎mwafrika, mzungu, muarabu,
‎mchina na Muhindi wana asili
‎moja?

CARDINAL: Hapana, hawana asili moja.
Hizo ni asili tofauti kabisa.

MIMI: kwanini?

CARDINAL: Tafiti zainasema kuwa Watu
wote asili yao ni Afrika. Ila hii
‎ni propaganda tu ili
‎waendelee kunyonya afrika.

MIMI: Kwanini?

CARDINAL: Chukuwa mfano huu: Mimi ni
mtu mweusi. Ninapatikana
‎afrika ya mashariki. Nina mke
‎wangu ni mweusi kabisa,
‎anapua fupi na kubwa kama
‎yangu. Tumezaa watoto 12,
‎waoto 2 wa kiume na wakike
‎wakachukuana ili kwenda
‎kuendeleza Uzao– wakaenda
‎Sweden ambapo hakuna jamii
‎nyingine nyeupe yenye pua
‎ndefu. Baada ya miaka 5000
‎( vizazi 200) wanazaa watoto
‎wenye pua ndefu, na ngozi
‎nyeupe. Hii inawezekana?

MIMI: Pengine, kutokana na
Mazingira ya kule.

CARDINAL: Makaburu wa Afrika kusini
wamekuja huku afrika mwaka
‎gani?

MIMI: Miaka ya 300-400 AD.

CARDINAL: Mbona hawajawa weusi? Ok,
watu wa Eritrea, wana muda
‎gani kule?

MIMI: Kwa hiyo unataka kusema nini
hapa cardinal?

CARDINAL: Ni lazima wanangu
watakapoenda Sweden,
‎wakutane na Race nyingine
‎yenye pua Ndefu na ngozi
‎nyeusi, ndipo watoto wao
‎watakapoanza kupata Wana
‎wenye pua Ndefu na Ngozi
‎nyeupe tofauti na race ya
‎wazazi wao ambayo miaka
‎nenda rudi hawatowahi kizaa
‎ngozi nyeupe wao kwa wao.

MIMI: Kwa hiyo kumbe Hizi ni race
tofauti kabisa?

CARDINAL: Ndio.. Wewe na mkeo ni
weusi wenye pua fupi. Hata
‎muende Norway, mkae miaka 1
‎Milion. Hatowahi kupatikana
‎mtu mwenye ngozi nyeupe na
‎pua ndefu.

MIMI: Mbona wazungu waseme kuwa
mtu wa kwanza alitoka afrika
‎mashariki? Mbona wadai kuwa
‎sote tuna asili moja, ilihali
‎waziwazi wanatubagua?

CARDINAL: Huo ni mpango mkakati ili
waendelee kunyonya afrika.
‎Lakini sisi na wao ni Race
‎tofauti kabisa. Wanajuwa
‎kuwa mwafrika akijuwa kuwa
‎yeye na wao ni maji na
‎mafuta– waafrika
‎watamtimua, hivyo anajitahidi
‎kuunganisha hizi race mbili
‎tofauti ili apate mwanya wa
‎kuendelea kula mema ya
‎afrika.

MIMI: saasa mbona wewe bado uko
huko?

CARDINAL: nazingatia maokoto ndugu
yangu😁
 
Back
Top Bottom