Visambuzi na haki ya msingi ya kupata habari

Visambuzi na haki ya msingi ya kupata habari

barafu

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2013
Posts
6,739
Reaction score
32,945
Mwezi December 2012 Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Mamlaka ya Usimamizi /Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA) ilizima rasmi mitambo ya analogia na kuwasha ile ya digitali.

Kulikuwa na ahadi nyingi na matumaini kwa wananchi kuwa digitali italeta ufanisi mkubwa na kuondoa adha katika sekta ya mawasiliano na upashanaji habari. Tulihaidiwa kuwa kodi itaondolewa katika visambuzi ili kutoa nafasi kwa kila raia kupata haki ya msingi ya kupata habari kwa kununua visambuzi kwa bei nafuu.

Miezi karibu nane sasa imepita, lakini hali ya upatikanaji wa habari kwa mfumo wa digitali umekuwa ni mgumu sana. Visambuzi tulivyoambiwa vitauzwa kati ya Tsh 30,000 hadi Tsh. 35,000 sasa vipo bei juu mara mbili yake, hii imesababisha watu wengi kukosa mawasiliano ya kupata habari.

Signal ya visambuzi kama vya Startimes kampuni mshirika na TBC zimekuwa zikisumbua na kusababisha kukwama au kupotea kabisa kwa upatikanaji wa habari kwa ujumbe wa "bad signal". Maeneo mengi vimekuwa vikithibitika kushindwa hata kwa matumizi ya "antenna", hali hii inaondoa haki ya msingi ya raia kupata habari.

Tofauti ya matarajio ya wengi baadhi ya mikondo hewa (channel) ambayo huonyeshwa bure, baadhi ya watoa huduma hao wa visambuzi wamewatoza wateja wao. Kuna mikondo hewa ambayo wamiliki wameanzisha kwa lengo la kutoa habari bure, wasambazaji wa visambuzi wamezifanya kuwa za kulipia na hivyo kupokonya haki ya msingi ya raia

Mikondo hewa kama IQRAA TV ambayo hutoa elimu ya dini ya kiislamu, EWTN ambayo hutoa misa na mambo ya wakatoliki, kuna nyingine Seventh Adventist na Emmanuel Tv. Msingi wake si biashara bali ni huduma za kiroho na hutolewa bure lakini Startimes wanatoza wateja wao kitu ambacho wanawanyima haki ya msingi ya habari na upashanaji.

Mikondo hewa mingine kama "The citizen" na nyingine ya Iran inayorushwa kwa lugha ya kiingereza ni mfano wa ambazo zilipaswa kuwa bila malipo, ukimya wa serikali, mamlaka husika na utapeli wa makampuni ya visambuzi vinapelekea raia kukosa haki yao ya habari.

Mpaka sasa ni kama hakuna lilio bora litokanalo na digitali zaidi kero na wizi wa haki ya msingi ya kupata habari, viongozi husika wamelala, wengine wanasemwa kuwa na ubia na makampuni ya visambuzi. Tunaomba wizara husika ikumbuke ahadi zake, iliahidi kuwa ulimwengu wa digitali utamfanya raia apate huduma nzuri na kwa upana lakini imekuwa kinyume chake.

Jambo hili lipatiwe ufafanuzi/ufumbuzi nasi tupate haki ya msingi ya kupata habari, maana digitali sasa imekuwa kama keroo. No signal!!! No Signal!!!

Lini sasa itakuwa "Yes Signal!!"
 
Nasikitika Startimes wamekuwa wakinikatia chanell zote mwezi ukiisha bila kuacha chanel za local kulingana na taratibu nawamekuwa wakinifanyi hivyo tangu January 2016 kila Mwezi wanakata Chanel zote wananiachia TBC na TV1 basi.. Yaan sijui nani mwingine anayetakiwa kukemea hili kama siyo TCRA, tunalipa Kodi ili hawa TCRA wapate mishahara ila wanatuacha Tunaumia kwenye nchi yetu wenyewe zidi ya wageni hawa wakichina..

Yaan kila mwezi nakatiwa Chanel Zote za local, nimefuatilia Startimes majibu yao nidharau tupu tena wanajiamini kweli kinaaliyenijibu kwenye simu kuwa nifanyechochote nikitaka ila lazima nilipie..

Hii nifedhea

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nadhani ni wote mkuu maana Mimi Nina azam dstv na startimes hawa wote vikiisha ni TBC one na TV one sijui kwanini hizo wakati local Chanel zote ilibidi ziwe bure


Ila wanachoniudhi star times ikibaki wiki lazima scratch zianze



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acha ubahili lipia Decorder.

Hapa kazi tu
Watu kama nyinyi ndio msiyo jua haki zenu umnakuwa bendera fuata upepo.. Yaan chanel za antena ambazo zina minara straight kutoka kwa service provider kama clouds TV, ITV, na Chanel ten startv na wwngine wote ambao sheria inatutakA tuzipate bure wewe inasema nilipie,? Hatakama ningekuwa milionea mm vip raia wenye kipato kidogo uko mitaani nani anawasemea??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom