Visa Vya Mama Wenye Nyumaba

Visa Vya Mama Wenye Nyumaba

hyo ni moja ya tabia za wanyakusa na sizipend Mungu aniepushie mbali!
 
Nilipokuwa nimepanga, bibi mwenye nyumba msela sana.

Sikuwahi kusikia zamu ya kudeki chooni, kufagia nje wala usafi wa aina yeyote.

Umeme unatumia utakavyo hadi kupikia jiko la umeme na tulikuwa wanaume wote kwahyo matumizi ya umeme ni babu kubwa ukichangia tulikuwa tunalipia 15,000 kwa mwezi ku-cover umeme, maji na usafi.

Mpenzi wako akija hana soo wala nini, yani ilikuwa raha sana. Sahivi nimehama nimemweka ndugu yangu pale na akitoka atamuweka mwingine.

Yule bibi nampenda sana, alitulea kama wanawe.
Naomba uniweke mimi mkuu
 
Habari Jaleleno MMU

Leo naomba tushee hizi kero za mama wenye nyumba kwa sisi tunaoishi nyumba za kupanga.
Ukienda kupanga bora muhusika awe Baba mwenye nyumba wengi hawana matatizo kama hawa mama zetu.
Mimi kipindi nasoma nilipanga kwenye nyumba ya Mama moja wa Kinyakyusa,Yule mama alikuwa hatari kwa mdomo,Nilijitahidi kumkwepa na kuwa busy cha ajabu siku mkikutana, We binti mbona sikuoni jikoni ukipika? utaniharibia ukuta wangu hii nyumba nilijenga mimi hii sio huyu babako(mumewe).
Haitoshi ikija bili ya maji toooobaaa!!!! ugomvi,anakuambia wewe mwenye kichumba kimoja ndo unamatumizi makubwa ya maji,Yaani ilikuwa ugomvi.
Nje kulikuwa na mti wa mapera msimu wa mapera ukianza anatoa kiti nje analinda mapera,ukipita anaanza kuimba taarabu mara mdundiko sijui..
Mpaka siku naondoka ilibidi niondoke kama mwizi ile nyumba asijue naondoka ,lakini nilimkomoa kama mwezi haujaisha nilitumia kupika kande jiko la umeme,maji ya kuoga,chooni nikamkomesha kuweka dekio chini kuacha maji yanatirika,na choo nikachukua gunia nikakandamiza.
Yule mama sitamsahau,mdomo wake alikuwa anamfokea mumewe hata nje ya uwanja,wapangaji nyumba yake walikuwa wanashindwa kukaa domo la mama mwenye hausi..

Hebu tupeane za mama mwenye nyumba wako huko kwa sisi tusiojenga.


ulitaka awe mwanaume ili akusamehe kulipa kodi baadhi ya miezi???
Usipende vya bure
 
ulitaka awe mwanaume ili akusamehe kulipa kodi baadhi ya miezi???
Usipende vya bure

Umenisikitisha sana na hiyo comment ambayo umeandika bila kufikiri vizuri
 
Narudia tena... Una roho ya shetani. Kwa kuwa shetani ndie mtu wa visasi. Hukuwa na sababu ya kufanya yote hayo ili kulipia ubaya aliokufanyia.

bibiwe hujalazimishwa kucomment hapa
 
Wakati mwengine inabidi kuwapa adhabu ya kutembea na waume zao na sisi wanaume inabibi kumtongoza

hiyo sio vizuri, unaweza ukajikuta unajikomesha mwenyewe
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom