virusi vya au virusi ya / za??? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

virusi vya au virusi ya / za???

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by Kipala, Sep 28, 2010.

 1. Kipala

  Kipala JF-Expert Member

  #1
  Sep 28, 2010
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 3,537
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  Jamani neno "virusi" limeingia katika lugha.
  Wengu huandika "Virusi vya UKIMWI", "virusi vya kompyuta".

  Lakini hii ina matata. Nimeshaona watu wanaoandika "virusi vya kompyuta ni hatari; wiki iliyopita kirusi kipya..."
  Hii inaonyesha udhaifu wa kawaida hii;: namna gani kutofautisha kati ya virusi 1 (virusi kimoja? virusi vimoja ????) na virusi 100 (virusi vingi?).

  Mimi naona afadhali tukubaliane "virusi" ni neno la Kilatini kilichoingia hapa kupitia Kiingereza na kama maneno yale mengi tuseme
  virusi ya kompyuta, virusi ya UKIMWI kama ni 1

  virusi za kompyuta nyingi ....

  Mnaonaje ?
   
 2. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #2
  Sep 29, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  Kipala umekuja kujiunga na Lugha, na mambo ya Dini na imani umekimbia nenda kanisani ukafundishe Yesu Mwana wa Mungu Yesu Mwokozi wetu tuache hapa Kipala chako kinafanya kazi kweli kweli.

  Neno hilo Virus vya Computer au Virusi vya ukimwi liache kama kawaida enategemea mtu atakavyo litumia hilo neno la Virusi vya Computer au Virusi vya ukimwi, unajuwa kirusi kimoja cha Computer kinazaa virusi vingi ndani ya hiyo Computer? kaulize kule Technology & Science Forum kaulize hilo swali utapata jibu lake.

  Hakuna ubaya wowote kusema kuwa Computer yangu imevamiwa na Virusi ndani yake. Au kusema kuwa Mtu fulani ana Virusi vya Ukimwi ni sawa saw tu na kusema kuwa Computer yangu imevamiwa na kirusi haifanyi kazi.
   
 3. Kipala

  Kipala JF-Expert Member

  #3
  Sep 29, 2010
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 3,537
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  Asante kwa kutupa mahubiri ya kidini hata hapa. Usiwe na wasiwasi, kuna uwezekano ya kwamba nimekutangulia kidogo hapa lugha (sifiki mara nyingi)

  Sasa tuache uchungu.
  Naomba nisaidie: nikielewa vema unasema umoja ni Kirusi na uwingi ni Virusi . Nimeelewa sawa?

  Lakini
  a) Kirusi ni lugha. Tutofautishe kivipi?
  b) Neno la nje ambalo limepokelewa katika Kiswahili ni "virus", siyo "kirus".
  c) unasema ni sawa kuandika "Mtu fulani ana Virusi vya Ukimwi". Je hii inataka kusema ameambukizwa na virusi 1 au vingi/nyingi?

  Kuna sababu gani kutumia "virusi" tofauti na "video" ?
   
 4. w

  wikama Member

  #4
  Nov 8, 2010
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 83
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  navyojua katika lugha ukianza na Vi - basi wingi wake ni vya na ukianza na Ki- inaenda na cha-, mfano kiti wingi wake ni viti, kwa kuwa neno la virusi ni kingereza yaani VIRUS, linatumika katika kiswahili basi lifuate kanuni za kiswahili yaani ni virusi vya ukimwi na siyo virusi ya ukimwi kikiwa kimoja kirusi cha ukimwi nadhani hii itasaidia .
   
 5. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #5
  Nov 8, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  Umeshaleta Topic mpya Neno Video ni neno la Kiingereza hakuna kwa kiswahili Tafsiri ya neno Video litakwenda hivyo hivyo Video tu.na neno Virus ni neno la kiingereza tunaweza kusema kwa lugha yetu ya kiswahili kuwa ni Virusi kwa wingi tu au Kirusi kwa umoja hakuna matatizo itategemea vile utakavyotumia wewe .
  Mkuu nakubaliana na wewe kwa lugha yetu ya kiswahili ukianza na herufi ya (Vi) basi ina maanisha ni wingi wa kitu aidha chakula au kitu chochote chenye kuwa na wingi ndio maana tukatumia herufi ya (Vi) kwa mfano chakula ni umoja wingi wake ni vyakula, chombo ni kimoja vyombo ni vingi,Kisahani ni kimoja Visahani ni zaidi ya kimoja. Hiyo ni baadhi ya mifano michache tu niliyokutolea ipo mingi tu asante mkuu wikama kwa ufafanuzi wako mzuri.
   
 6. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #6
  Nov 8, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,193
  Trophy Points: 280
  Nani nguli wa ngeli ?

  Virusi vya, kama vinywaji vya. Kirusi cha, kama kinywaji cha.

  Kama unaweza kukikamata kirusi kimoja, then unasema Kirusi cha, kama unamaana ya aina moja ya kirusi, pia unaweza kusema kirusi cha HIV kama unavyoweza kusema kinywaji cha pepsi. Pia unaweza kusema virusi vya HIV. Lakini kamwezi huwezi kusema virusi cha HIV, haitakuwa sahihi kwa kufuatisha ngeli za kiswahili.

  Usichanganye vi ya Kiswahili na ya kiingereza, katika kiingereza hawa wadudu wanaitwa virus, jina linaanza na vi, katika kiswahili vi inaashiria wingi, na kimoja hakiwezi kuitwa virusi cha, kinaitwa kirusi cha kwa kufuatisha ngeli za Kiswahili.

  Hili ni somo la ngeli za Kiswahili, darasa la nne enzi hizo kama sijakosea, sijui kama wanafundisha bado siku hizi.
   
 7. Kipala

  Kipala JF-Expert Member

  #7
  Nov 10, 2010
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 3,537
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  Asante nimeelewa hoja lako.
  Lakini naomba jibu swali linalofuata:
  Je tukitazama filamu nyingi za video tunatazama pia filamu 1 ya kideo?

  Nadhani hatuwezi, tunasema video moja, video nyingi si vingi; video ndefu si virefu n.k.

  Sasa video sawa na virus ni maneno ya kigeni yaliyopokelewa katika Kiswahili. Mara nyingi maneno haya yanafika katika ngeli ya n-n (i-zi).

  Si lazima, maana kuna njia nyingi za "kuswahilisha" neno la kigeni (kama dokta - madokta si wadokta wala dokta wengi).

  Ila tu kwa "virusi" - naona ugumu kwa sababu "Kirusi" ni lugha.

  Kwa sababu gani virusi iwe tofauti na video? Kwa nini tusiseme virusi moja - virusi nyingi ?
   
 8. Gurta

  Gurta JF-Expert Member

  #8
  Nov 11, 2010
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 2,246
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Mhe Kipala,

  Kuna kitu kwenye lugha yoyote kinaitwa 'upatanisho wa kisarufi.' Hebu tuichambue hii kwa mfano:

  Tuchukue neno la kiIngereza 'mine' katika maana ya 'umiliki' na sio mgodi au bomu. Neno hili kwa kiSwahili lnaweza kutafsiriwa kama 'YANGU, CHANGU, WANGU au LANGU' kulingana na linatumika na nomino gani.
  • Gari langu.
  • Saa yangu.
  • Mke wangu. n.k.
  Haitapata kutokea mtu akasema 'Mke changu.' Kwa sababu 'changu' haipatani kisarufi na 'mke'.

  Turudi kwenye 'VIRUSI' kwanza tukubaliane kwamba neno hili limetoholewa kutoka KiIngereza ambao nao pia wamelitohoa. Baada ya neno kutoholewa kwenda katika lugha fulani, halina budi pia kufuata taratibu za lugha ile. Sasa ili kuleta huo upatano wa kisarufi kikiwa kimoja kitaitwa 'kirusi' ambao wingi wake ni 'virusi'
   
 9. Gurta

  Gurta JF-Expert Member

  #9
  Nov 11, 2010
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 2,246
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Kirusi (n)
  1. lugha yenye asili ya KiSlaviki katika familia ya Indo-European inayozungumza na watu wa Urusi, Belarus, Ukraine, Kazakhstan na Kyrgyzstan na mataifa mengine jirani
  2. umoja wa 'virusi'
   
 10. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #10
  Nov 11, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,193
  Trophy Points: 280
  Ukisema "nimeelewa hoja lako" unakosea, hoja inaenda na yako, hivyo "nimeelewa hoja yako".

  1. I doubt "video" ni neno la Kiswahili, mimi najua filamu ni neno la kiswahili.

  2. Hata kama "video" ni neno la kiswahili kwa maana ya kwamba limetoholewa rasmi, kila lugha ina rules na exceptions, kwa hiyo huwezi kutumia exception moja kutaka kuhalalisha kuvunja rules zote.

  Kwa mfano, kiingereza kina rule ya kind, kinder, kindest kuonyesha intensity ya kitu unaweka er na est mwisho wa neno.

  Lakini kuna exceptions, hatusemi beautiful, beautifuler, beautifulest, tunasema beautiful, more beautiful, most beautiful.

  Lakini ukweli kwamba kuna exception hii haumaanishi kwamba ile rule si valid. Linguistics is not a hard science with set constants and natural invariables like the speed of light in a vacuum.
   
 11. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #11
  Nov 11, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,193
  Trophy Points: 280
  Ukiangalia kwa undani utagundua neno "virus" halijatoholewa moja kwa moja kutoka Kiingereza na kuongezewa i ya mwisho kupewa sauti ya kiswahili tu, matamshi ya Kiingereza ni "vairas" na kiswahili ni lugha ya matamshi inayotohoa kwa matamshi kuliko maandiko, kwa hiyo kutohoa moja kwa moja kungekuwa "vairasi".

  Kwa hiyo, lilipotoholewa pia likaswahilishwa na kusilimishwa zaidi ya kupewa sauti ya Kiswahili tu, ndiyo maana hatusemi "vairasi".

  Kwa hiyo neno "virus" halijatoholewa kuwa "virusi" kama ambavyo maandishi yanaweza kutughilibu. Neno "virus" limetoholewa kuwa "kirusi". Neno hili wingi wake ndio umekuwa "virusi" kwa sababu wingi wa ki ni vi, kama vile wingi wa kijiji ulivyo vijiji.

  Kinachochanganya hapa ni kuona kwamba, wingi wa kirusi "virusi" unafanana na umoja wake katika kiingereza "virus".
   
 12. Kipala

  Kipala JF-Expert Member

  #12
  Nov 11, 2010
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 3,537
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  Asante sana kwa mchango - umeikuta wapi? Au umeitunga mwenyewe?
   
 13. Kipala

  Kipala JF-Expert Member

  #13
  Nov 11, 2010
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 3,537
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  Asante kwa kunisahihisha huko juu!

  Ila juu ya hii: una uhakika imechukuliwa kutoka Kiingereza? Mimi sidhani.

  Maana ndani ya Kiingereza maneno mengi sana yamepokelewa kutoka lugha nyingine.
  Hasa maneno ya kisayansi yana asili katika lugha za kale Kigiriki na Kilatini.
  Kiingereza mara nyingi inapinda matamshi ya maneno haya kutoka kwa kawaida ya kimataifa;)
  Mara nyingi si matamshi ya Kiingereza ya maneno ya kisayansi yaliyopokelewa katika Kiswahili.

  Mfano: Kiswahili sanifu ni "biolojia" si "baiyolojia". (hii ina faida nyingi ... - lingaisha Kamusi ya TUKI)

  Kwa hiyo nina wasiwasi kuhusu maelezo yako yanayohusu utaratibu wa kushughulika maneno yenye asili ya Kiingereza maana sidhani inafaa kwa mfano huu.
   
 14. k

  kakiige New Member

  #14
  Nov 24, 2010
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa maoni yangu kuna utata unaotokana na kutoholewa kwa neno virus kuwa virusi. Ile "vi" katika virusi sio yakuashiria wingi ila ni sehemu ya jina lile. Kipala asema kweli kuwa hakuna neno kam "Kirusi". Shida kuu nikupata wingi wa virusi moja ambapo naonelea iwe "Mavirusi mengi".
   
 15. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #15
  Nov 24, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Kwenye lugha ya kiswahili kuna maneno mengine haya wingi! mf: Maji, Virusi, bamia, mchele, unga n.k
   
 16. Kipala

  Kipala JF-Expert Member

  #16
  Nov 26, 2010
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 3,537
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  Una uhakika "Virusi" iko katika kundi hili cha maneno yanayojumlisha kiasi lakini hayawezi kuhesabu jambo?

  Maana maji ni jumla; tunaweza kuwa na maji mengi au kidogo, lakini hatuna maji 1,2,3 yaani hatuna umoja kilugha; badala yake tunaweza kuhesabu matone ya maji. Vivyo hivyo mchele: kilugha haina umoja, tunaweza kuhesabu aina au punje za mchele lakini haiwezekani kutaja mchele 1,2,3.

  Kwa virusi inawezekana kuzihesabu 1,2,3 (estimate of virusload).
   
 17. Charles1990

  Charles1990 JF-Expert Member

  #17
  Nov 26, 2010
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 222
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mtu asikudanganye,sana sana we nielimishe ila mwisho wa siku mi mchaga,nitakuambiaaa:Firusi fya kompyuuu we utamalizia kompyuta.Ndugu zangu watakuambia Vilusi wa kompyuta.
   
 18. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #18
  Nov 26, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Katika neno Virusi hakuna wingi wala umoja!
   
Loading...