Virusi katika ndoa

Virusi katika ndoa

Valentina

R I P
Joined
Oct 12, 2013
Posts
24,688
Reaction score
28,834
Maneno haya siyo yangu nimekopi na kupest. Ila naamini utakota mojawapo katika haya.
Maneno yenyewe ni haya yafuatayo;

Virusi vya ugonjwa wa kichaa cha Ndoa vinatoka wapi?

Virusi hivyo hatarishi vinatoka katika maeneo makuu matatu;

Eneo la kwanza: tabia ya kumhisi vibaya mumeo.

Eneo la pili: Mke kutotaka kutimiza wajibu wake kama mke. Mke kutotaka kuwa mjenzi wa ndoa. " Mwanamke mpumbavu ataibomoa nyumba yake kwa mikono yake mwenyewe.

Eneo la tatu: Mke kutojiamini kama yeye ni chaguo halali la mumewe.
Ukishakuwa na virusi hivi katika maeneo haya matatu, lazima utaaupata ugonjwa huu ambao dalili zake sasa ndizo zitakufanya uutambue una ugonjwa huo. Na haraka sana lazima uchukue tahadhari ama tiba sahihi

Ugonjwa huo dalili zake- ni:


1. Kuwa hasira kila mara kwa mumeo.

2. Wivu uliokirhiri

3. Kumchukia mumeo bila sababu, Yaani hana jema kwako.

4. Kuwa na chuki na wasichana warembo barabarani,kumtukana au kupigana na mwanamke yeyote ambaye,utahisi,- ama utaambiwa kwamba ana mahusiano ya mapenzi na mumeo.

5. Kununa hovyo, kiburi na majibu mabaya kwa mumeo.

6. Kila aliyekaribu na mumeo kumchukia. Especiall ndugu zake, marafiki zake. Ole wa mwanamke anayemsogelea.

7. Kuanza kujichukia mwenyewe na kutojipenda.

8. Kuanza kueleza matatizo ya mumeo kila mahali 9. Kuwaza kuondoka na kuvunja ndoa.

10. Kushika simu ya mume kwa kujiiba na kuchunguza msg au simu zilizoingia na kutoka

11. Kuanza kumchunguza mumeo kwa kuweka maspay ama wewe mwenyewe.

12. Kuchukia watoto wako wa kuwazaa mwenyewe. Licha ya wakufikia.

13. Kutamani Kuua ama kujiua.

Dalili za ugonjwa huo ni mbaya sana, na zinakukosesha furaha na kujiamini. Muda wote unakuwa mwanamke wa kujifikiria vibaya na kushidwa tu.

Unapogundua una dalili za ugonjwa huo, tafadhali anza kukabiliana na baadhi ya dalili hizo kabla hazijawa sugu. Zinapokuwa sugu utazalisha hatari zaidi na hasara.

Ugonjwa huu unatibika, na tiba yake inakuhitaji wewe mwenyewe kujituma na kuanza tiba hiyo.

TIBA YA UGONJWA WA KICHAA CHA NDOA:
1. Lazima usamehe kwa kumaanisha kwa unayoyajua na usiyoyajua.

2. Lazima uanze kuishi kwa kuaminiana na mumeo.

3. Timiza wajibu wako Kama mwanamke usipende kuagiza watoto/house girl kumuhudumia mumeo

4. Ujiamini kwamba wewe ni chaguo halali la mumeo , ili ikupe kujiamini na kujipenda(kutingisha mgongo)

5. Haraka sana anza kufunga chumba chako, kwa Kumheshimu mumeo, kumthamini na kumstahi.

6. Maombi ni jambo la msingi sana na manufaa, nilazima umuombee mumeo nafamilia yako kwa kumaanisha.
Unapokuwa na Kichaa cha Ndoa ni vigumu sana kuwa na maendeleo kwenye familia, na maisha kwa ujumla, yaani hata uchumi utayumba sana, kwani muda mwingi utakuwa na hasira.

Hivyo ni vyema sana kuhakikisha unakuwa makini kwa kuchukua tahadhari hizo 6 ili kukabiliana na ugonjwa wa Kichaa cha ndoa, ama la basi kama tayari dalili hizo unazo uweze kujitibu.
 
'Valentina' katika ubora wake...mkuu binafsi jana kuna mtafaruku umetokea japo nimefanikiwa kusolve ila nimepunguza upendo kwa kiwango fulani till nione ameimprove nimrudishie nyota niliyompoka!
 
Last edited by a moderator:
'Valentina' katika ubora wake...mkuu binafsi jana kuna mtafaruku umetokea japo nimefanikiwa kusolve ila nimepunguza upendo kwa kiwango fulani till nione ameimprove nimrudishie nyota niliyompoka!

Mweeh nini shida na wifi yangu tena
 
Last edited by a moderator:
Kweli Kabisa.. I agree with you. Napenda kujifunza.. This z for both Man n Women Us. Jifunze Itakusaidia. Sio kwakua Wameandikiwa Wanawake eti Sisi wanaume haituhusu.. No! Jaribu pia kuubadili ujumbe Uone kama ni Wako pia Mwanaume utagundua una weakness kadhaa pale ambazo pia wewe Unazo ni kujifunza na Kubadilika Kuboresha Mahusiano Yenu.
 
Back
Top Bottom