Bartazar
JF-Expert Member
- Oct 4, 2011
- 1,049
- 571
Waswahili walisema ukistaajabu ya Musa utayaona ya Firauni...
Yametokea mji mdogo wa Ifakara mtaa wa Mlabani ambapo mgombea wa uenyekiti kwa tiketi ya CCM akitetea kiti chake alipelekewa jeneza akisubiriwa ajinyonge. Ilikuwa hivi...
Kabla ya uchaguzi alisikika akijigamba kuwa endapo angeshindwa uchaguzi ule angejinyonga. Maneno hayo kuingia masikioni mwa wnanchi, na wakasubiri kwa hamu utimilifu wa hiyo maneno. Siku ya siku uchaguzi huo..., watu wakachagua waliowachagua. Makokeo yalipotoka, mgombea huyu akaangukia pua, na akachaguliwa mgombea wa chadema.
Ndipo wana wa nchi walipokumbuka maneno ya mgombea huyo na kuamua kumrahisishia kazi. Wakachanga fedha kiasi cha sh. 101,100/=, wakanunua mbao na kuchonga jeneza, na kisha wakampelekea wakisubiri ajinyonge... Hadi leo jrnrza lipo hapo nyumbani kwake naye analitazama tu!