proxy
JF-Expert Member
- Jul 3, 2016
- 1,481
- 1,356
Nimejilimia kampunga kangu na nina viloba kama 8 hivi nimevipiga kwenye kitani 2 changu narudisha nyumbani ,sasa shida kuna jamaa hapa getini wanahitaji ushuru kwa gharama ya 4,000 kila roba,sasa naombeni kuuliza hivi hizi sheria za ushuru zikoje huwa zinaruhusu kumtoza mtu ushuru kwa viroba alivyojilimia mtu kwa ajili ya chakula? .Na kama inatakiwa ulipia ni kwa gharama gani kwa roba?Naomba kuwasilisha wakuu.