Vipindi hivi maalum vinalipiwa na nani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vipindi hivi maalum vinalipiwa na nani?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Muangila, Mar 14, 2011.

 1. Muangila

  Muangila JF-Expert Member

  #1
  Mar 14, 2011
  Joined: Feb 24, 2010
  Messages: 1,854
  Likes Received: 196
  Trophy Points: 160
  Wana JF toka maandamano ya CDM yaanze kumekuwepo na vipindi maalum kwenye TV hapa kwetu wakiwahoji viongozi mbalimbali wa CCM na serikari kuhusu maandamano na wameutumia muda huo zaidi kukishambulia CDM kwa maneno makali ukiwemo na upotoshaji.Sasa naomba kujua je hivi vipindi vinalipiwa au ni bure kama ni bure kwa nini Television zetu hawawaiti CDM ili nao wawahoji ili kuweka uwiano wa taarifa hizi
  NAWASILISHA...!
   
 2. Technician

  Technician JF-Expert Member

  #2
  Mar 14, 2011
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 843
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kwani hujamsikia Askofu Pengo amelalamika kuwa watu wameshafungwa mdomo si kwa wanasiasa tu bali hata vyombo vya habari na wametishiwa kuuwawa endapo wataendelea kukikosoa chama Tawala thithiem.

  BIG UP ASKOFU PENGO KWA KUSEMA UKWELI HATA KAMA UNAUMA.
   
 3. emmathy

  emmathy Senior Member

  #3
  Mar 14, 2011
  Joined: Sep 22, 2010
  Messages: 146
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  media coverage wanayoipata ccm na serikali haiwez badilisha mawazo ya watu mana moyo,akili,nafsi ndio vilivyobadilika kutokana na maovu na ufisadi si macho na masikio yaliyobadilika kutokana na kuangalia tv dhidi ya propaganda za ccm.
  The need for change stil active in our mind
   
 4. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #4
  Mar 14, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Moja ya matatizo makubwa yanayolikabili taifa letu ni ubinafsi; watu wengi wanao ongoza taasisi na mashirika nyeti ya umma, wameamua kuweka taaluma zao kando na kucheza ngoma inayopigwa na watawala, kama njia ya kulinda maslahi yao binafsi. Jambo ambalo pengine wanashindwa kulielewa, ni kwamba mwisho wa yote hayo hawawasaidii hata kidogo watawala hao, maana watu wakisha ngamua kuwa chombo fulani ni kipaza sauti cha watawala wanakipuuzia. Hivyo ndivyo ilivyo kwa baadhi ya magazeti na vituo vya redio na luninga.
   
 5. k

  kilolambwani JF-Expert Member

  #5
  Mar 14, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 395
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Msihangaike na hivyo vipindi kwani hakuna watu wa maana wanaovisikiliza. Wanasikiliza wenyewe ccm tu.
   
 6. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #6
  Mar 14, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,767
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Hata mimi vipindi hivyo vinanishangaza saana na kwanini ni maaalumu umaalum wake upo wapi???? Ccm bwana!
   
 7. l

  lyimoc Senior Member

  #7
  Mar 14, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 140
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wafanye vyovyote vile ngoma yao ni yakitoto haiwezi kukesha .waongee kwenye tv hata masaa24 tumewachoka
   
 8. K

  KipimaPembe JF-Expert Member

  #8
  Mar 14, 2011
  Joined: Aug 5, 2007
  Messages: 1,287
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Hao hao viongozi wanaoenda kuhojiwa na kurusha makombora ya maneno kwa Chadema ndo viongozi ambao wananchi wengi hawana imani nao, na kusema ukweli wanachokisema wananchi wengi wanatarajia waseme vile. Tatizo ni kuwa hao wanaoongea wengi taswira zao kwa wananchi ni Chafu. Wananchi wanajua kuwa wanajikosha tu.

  Haiwezekani viongozi wa serikali wafanye kazi za kiserikali na kazi za chama wakati mmoja bila kuleta mgongano wa kimaslahi. Mara nyingi wamekuwa wakitumia nafasi zao kama viongozi wa umma kujaribu kuitetea CCM. Ni jambo lililo wazi kuwa kazi wanazofanya ni kazi ya Chama chao kwani wanajaribu kuchapa siasa kwa kutumia nafasi zao kama viongozi wa serikali.

  Kuhusu media, viongozi wale wameshajifunza baada ya kuona yaliyompata Tido Mhando. Ingawa alijitahidi sana kucheza ngoma ya usaniii wa CCM bado kiwango chake cha Taaluma na weledi vilimfanya ajizuie kufanya upendeleo wa wazi wazi kwani kwa kufanya hivyo ilikuwa kuchafua rekodi yake ya utendaji. Kama vile Mzee Six kule bungeni alivyokuwa akijitahidi sana kukibeba CCM lakini ikawa inafikia mahali anashindwa kutokan na kiwango chake cha utalaam na weledi.

  Ndo maana imefikia mahali tunaamini kuwa ili uweze kufanikiwa katika serikali hii na chama chake ni lazima uwe mbabaishaji wa wazi wazi tena asiye na shaka (mediocre). Ukiwa na kakiwango fulani ka weledi na utaalam na ukavitumia, dhahiri kabisa utaonekana kwenda tofauti na mwenendo wa chama na serikali yake na utakuwa huna nafasi humu. Kitu hiki ndo kinazidi kuwajenga wapinzani wa CCM kwani kusema ukweli inaonekana kabisa CCM ina viwango vya kikwake vya kupima uwezo wa watu.

  Sasa wakiendelea kujaza mapropaganda ya chama kwenye media ambazo zilikuwa zimeshaanza kujirudishia hadhi yake matokeo yake ni kuziua kabisa hizo media na hicho wanachokitarajia watakikosa kabisa. Kutetea uozo na kuendekeza propaganda chafu kwenye media za umma hakutasaidia zaidi sana ni kuzifanya media hizo zishindwe kuaminika na watu walio wengi. Vinginevyo huwa inafikia wakati kuwa palipo na ukweli UWONGO HUJITENGA.

  Kwa mfano hizi kaulizo zilizojaa midomoni mwa viongozi wengi kuwa maandamano ya Chadema yalikuwa na lengo la kuanzisha vurugu, kila mtu anaona ni ujuha kwani kote yalikofanyika; yaliisha salama bila vurugu zozote watu wakirudi nyumbani kwao salama. Sasa hizo vurugu ambazo wanatumia muda wao mwingi kuzihubiri ni zipi? Zilizotokea Arusha, kwenye mahakama ya maoni ya watu, ni wazi CCM walipoteza kwani vurugu zile zinaonekana kabisa zilikuwa za polisi. Kwa hiyo hata wakitumia media za umma kujieleza sana, haiachi shaka, kuwa wana matatizo. Kwa sababu badala ya kujieleza na kujibu hoja na kueleza ukweli wa mambo ambao wananchi wanaujua, wamejikita katika propaganda.

  Hiyo inakula kwao zaidi kuliko wanavyodhani. Kuwa na media na kuzitumia sana si chanzo cha mafanikio. Mafanikio hutokana na jinsi unavyozitumia media kujenga hoja zinazojisimamia zenyewe, badala ya kulazimisha hoja.
   
Loading...