Vipimo vya kisima cha maji

Sendeu

Member
Jun 29, 2009
59
2
Wadau nimejenga kisima ili nivune maji ya mvua hapa hapa DSM naomba wenye ujuzi wanijuze hivi kisima cha urefu wa futi 14 na upana wa futi 8 kina ujazo wa lita ngap? Asanteni
 
tafuta eneo la chini la kisima zidisha kwa kimo, kisha libadilishe kuwa katika lita, acha uvivu.
 
Wadau nimejenga kisima ili nivune maji ya mvua hapa hapa DSM naomba wenye ujuzi wanijuze hivi kisima cha urefu wa futi 14 na upana wa futi 8 kina ujazo wa lita ngap? Asanteni
Cha duara au pembe nne(square/rectangular)? Huo 'urefu' umekusudia kusema 'kina'?

Kama ni square na kina ni ft 14 kitaingia lita kama 25,000. Na kama ni duara kwa kina hichohicho kitaingia lita kama 20,000.
 
Mbona vipimo havijakamilika?, ili upate volume lazima uwe na urefu x upana x kimo. Wewe hujatupa kimo, tutapataje volume?. Kweli hesabu ni somo gumu.
 
Umejenga kisima au umejenga tenki la kuhifadhi maji? Sijui kama unaweza "kujenga" kisima kwa vipimo hivyo - mimi nadhani umejenga sehemu au tenki la kuhifadhi maji manake kisima is a borehole or a well to draw water from na wewe unaongelea "kisima" cha kuharvest maji ya mvua?????

Watakusaidia wanaojua hesabu.....binafsi BAM zero!!!
 
Waliokimbia hesabu shuleni utawajua tuu!
We Bongolala leo umenichekesha kwelikweli du hapo kwenye red, hapa JF inabidi kuingia taratibu la sivyo utaonekana zumbukuku ,umenikumbusha nilipokuwa sekondari jamaa walivyokuwa wanazipiga chenga hesabu ,utawsikia uansheria hauna hesabu,mweh kumbe hesabu ni kitu chochote ,hesabu ni maisha.Jamani inabidi hata watoto wetu tujitahidi kuwazoesha wapende somo la hisabati,hilo ndio somo mama wa masomo yote
 
Wadau nashukuru kwa maoni,ushauri na elimu tenki nililojenga ni la duara kina chake ni futi 14 na upana wake ni futi 8 so from up to down futi zinalingana na upana vile vile the same futi 8 from up to down so please nipeni vipimo vya kitaalamu regardless kuwa mtu unajua au hujui hesabu kubwa hapa ni elimu kwa wana JF wote nataka kujua exactly lita zitakazoingia kwny kisima/tenk husika
 
formula :pI*radius squared*height
halafu jibu la hapo unaliconvert kutoka cubic feet kwenda kuwa litres

3.142*4*4*14=703.8
then
703.8 cubic feet = 19929.7 which is almost 20,000 litres
 
Huyu jamaa kweli hisabati hawezi amejitahidi kufafanua vipimo eti anasema tank ni la duara lakini upana ni futi 8. Hivi duara tuna upana? au kipenyo? hayo ndo madhara ya kukimbilia uandishi wa habari! hesabu ya shule ya msingi tu inakutoa jasho. vipi sasa ingekuwa chi-square?
 
$
Mbona vipimo havijakamilika?, ili upate volume lazima uwe na urefu x upana x kimo. Wewe hujatupa kimo, tutapataje volume?. Kweli hesabu ni somo gumu.

Wacha kikariri wewe,
Kama ni cha duara huo urefu na upana utatoka wapi??
 
Back
Top Bottom