Vipi nipate kamusi?

Bakari China

JF-Expert Member
Jun 12, 2019
251
583
Habari wakuu mimi ni mwanafunzi kujifunza Kiswahili nchini China. Mimi nahitaji kamusi za Kiswahili lakini nimeshapata moja tu.

Maswali matatu:

La kwanza: huko Tanzania watoto wa shule za msingi hutumia kamusi gani?(kwa sababu nina msingi wa Kiswahili tu) na baada nijifunze zaidi nahitaji kamusi gani kwa watu wazima?

La pili: najua Kiingereza kidogo, kwa hivyo kamusi za Kiswahili~Kiswahili, za Kiingereza~Kiswahili, za Kiswahili~Kiingereza nazihitaji zote. zipi nazihitaji kabisa, mwasemaje? (Ikiwa na kamusi za Kiswahili~Kichina&Kichina~Kiswahili itakuwa vizuri sana)

La tatu: vipi naweza kupata kamusi hizi? kwenye mtandao wa China sijaiona kamusi yoyote ya Kiswahili. Tafadhali nipe tovuti kadhaa km. AMAZON ya TANZANIA, ili nipate njia ya kupata kamusi
shukran nyingi kabisa
 
Nitajaribu kuulizia.unaweza kutumia kamusi ya English-kiswahili nafikiri ndio Bora kwako.Nitauliza katika Chuo kikuu kimoja huwa wanasoma kichina labda unaweza kupata kiswahili- kichina.

Tanzania hakuna Duka la Amazon. Unaweza mwambia mtu akununulie halafu atakutumia uchina Kwa Posta au EMS.
 
Back
Top Bottom