Nmeguswa sana hii maada. Sitamsahau ex wangu tulipendana sana tulipitia hali ngumu naye alinivumilia na nilimvumilia alinifariji kila ninapokumbwa na matatizo alijivika matatizo yangu yakawa yake. Lah hasha! Safar ya maisha ni kiza kinene unajua unapotoka lakn hupajui unapoenda. Niliweza kusafir mikoa ili nikamuone na kumjulia hali na yeye aliweza kujitoa kwa ila hali ili tu mambo yaende sawa.
Siku uhusiano wetu unavunjika alitoa machoz hadharan kama kapatwa na msiba. Naweza kujiita mzembe kwa kushindwa kulinusuru penzi na kusikia maneno ya watu. Japo palikuwa na vielelezo lakn nilishndwa hata kutoa nafasi ya msamaha, hasira hasara.....
Nakumbuka neno alilonambia Mungu anasamehe lakn ww mwanadam ni nani hasa hutaki kusamehe? Japo kwasasa yeye ni mke wa mtu lakn bado ananilaumu kwa kushindwa kunusuru penzi....
Pamoja na kuwa kila mtu ana hamsini zake lakn tunasaidiana kwa kila linalowezekana.
Sitokuja kumsahau my ex wangu, kutokuwa pamoja limekuwa pengo kubwa