Vipepeo Weusi: Mkakati Namba 0034 (Simulizi)

Vipepeo Weusi: Mkakati Namba 0034 (Simulizi)

No hii kuna mtoto nahisi anaitwa Grayson alizaliwa na utindio wa ubongo mama ake akawatelekeza akaja akapata ukimwi akamuambukiza mumewe, ,,.... aahghhhha nishaisahau,
ila ni family matter
Yani wewe bora mimi

Hakuna story ambayo haina family matters.
 
No hii kuna mtoto nahisi anaitwa Grayson alizaliwa na utindio wa ubongo mama ake akawatelekeza akaja akapata ukimwi akamuambukiza mumewe, ,,.... aahghhhha nishaisahau,
ila ni family matter
Hiyo ya greyson mwenye mtindio wa ubongo naikumbuka, alikua na dada yake anaitwa destiny, nadhan walikua wanakaa na bibi yao sijui! Greyson alikua ni genious, akachukuliwa na marekani akawa anadesign computers. Baadae tz wakatuma kikosi cha makomando kwende kumteka (wakiongozwa na komando buberwa ), wakamleta tz akawa anawafanyia kazi ile km america (ofisi yake ilikua under ground nje ya mji huko) america wakashtuka nao wakaja kumchukua tena. Sasa nimesahau mwanzo wake kabisa na mwisho wake, hata jina pia sikumbuki.
Aargh jamaa nae alikua na story nyingiii
 
Nimesubiri mpaka saiz sijala bado, mpira sikuenda kuangalia duu bado nasubiri episode 3
 
DAAAHH WAKUU SIJUI NISEMEJE.!! NAHISI THE BOARD WAMEDUKUA PC YANGU.! YANI NIMEANDIKA EPISODE YOTE, MIDA YA SAA KUMI NA MOJA NATAKA KUPOST SIJUI NIMEGUSA WAPI IKAYEYUKA YOTE KATIKA MAZINGIRA YA KUTATANISHA

USHUJAA NILIOUFANYA NASTAHILI HATA KIEPE YAI WALAHI.!! IMEBIDI NIANDIKE TENA UPYA YOTE, NENO KWA NENO.!! NA KWA HASIRA SASA LEO NAPOST EPISODE 3 ALAFU KESHO EPISODE 4.!! YANI BAMPA TO BAMPA KUWAKOMESHA THE BOARD

NDANI YA DAKIKA 10 EPISODE 3 INAKUWA HEWANI..

MNIWIE RADHI WAKU..!
 
DAAAHH WAKUU SIJUI NISEMEJE.!! NAHISI THE BOARD WAMEDUKUA PC YANGU.! YANI NIMEANDIKA EPISODE YOTE, MIDA YA SAA KUMI NA MOJA NATAKA KUPOST SIJUI NIMEGUSA WAPI IKAYEYUKA YOTE KATIKA MAZINGIRA YA KUTATANISHA

USHUJAA NILIOUFANYA NASTAHILI HATA KIEPE YAI WALAHI.!! IMEBIDI NIANDIKE TENA UPYA YOTE, NENO KWA NENO.!! NA KWA HASIRA SASA LEO NAPOST EPISODE 3 ALAFU KESHO EPISODE 4.!! YANI BAMPA TO BAMPA KUWAKOMESHA THE BOARD

NDANI YA DAKIKA 10 EPISODE 3 INAKUWA HEWANI..

MNIWIE RADHI WAKU..!
Mimi nikajua Tanesco wamekata umeme lol
 
DAAAHH WAKUU SIJUI NISEMEJE.!! NAHISI THE BOARD WAMEDUKUA PC YANGU.! YANI NIMEANDIKA EPISODE YOTE, MIDA YA SAA KUMI NA MOJA NATAKA KUPOST SIJUI NIMEGUSA WAPI IKAYEYUKA YOTE KATIKA MAZINGIRA YA KUTATANISHA

USHUJAA NILIOUFANYA NASTAHILI HATA KIEPE YAI WALAHI.!! IMEBIDI NIANDIKE TENA UPYA YOTE, NENO KWA NENO.!! NA KWA HASIRA SASA LEO NAPOST EPISODE 3 ALAFU KESHO EPISODE 4.!! YANI BAMPA TO BAMPA KUWAKOMESHA THE BOARD

NDANI YA DAKIKA 10 EPISODE 3 INAKUWA HEWANI..

MNIWIE RADHI WAKU..!
Ah hahahahahahaaaa hongera mkuu,
Ila ungetengeneza pdf tununue kupitia link
 
DAAAHH WAKUU SIJUI NISEMEJE.!! NAHISI THE BOARD WAMEDUKUA PC YANGU.! YANI NIMEANDIKA EPISODE YOTE, MIDA YA SAA KUMI NA MOJA NATAKA KUPOST SIJUI NIMEGUSA WAPI IKAYEYUKA YOTE KATIKA MAZINGIRA YA KUTATANISHA

USHUJAA NILIOUFANYA NASTAHILI HATA KIEPE YAI WALAHI.!! IMEBIDI NIANDIKE TENA UPYA YOTE, NENO KWA NENO.!! NA KWA HASIRA SASA LEO NAPOST EPISODE 3 ALAFU KESHO EPISODE 4.!! YANI BAMPA TO BAMPA KUWAKOMESHA THE BOARD

NDANI YA DAKIKA 10 EPISODE 3 INAKUWA HEWANI..

MNIWIE RADHI WAKU..!
Nimekaa na simu yangu mithili ya mtu anayesubir hela kwa njia ya Mpesa kila meseji notification ikiingia anashika simu kumbe ni meseji ya deni la Mpawa
 
Ilipoishia Episode 2

Ray anaitwa na Dr. Shirima katika kikao cha 13 (D.S. 13) katika Hoteli ya Nashera. Anapewa maelekezo ya kuwaombea tenda vijana kadhaa waliopo chini ya taasisi yake ya SOTE HUB.
Tenda hizo zinatangazwa na serikali na makampuni binafsi kwa kuzingatia sera iliyopendekezwa na mbunge Zephania.
Lakini wiki tatau baadae yanatokea mauaji ya waziri wa Nishati na baba yake Hasnat anahusishwa na kifo hicho.
Ray anaanza kupata hisia juu ya mkakati unaopangwa na The Board na anajilaumu kwa hakuwahi kumueleza Hasnat kuhusu ushirika wake katika mipango ya The Board.


------------------------



EPISODE 3


Kwa karibia dakika tano Hasnat alinitazama kwa mshangao akiwa amepigwa na bumbuwazi.
"What's going on Ray?" Hatimaye akaniuliza tena akiwa amenikazia macho.
Niliwaza haraka haraka nianze vipi kumueleza nilichokuwa nimepanga kumuambia. "Hey, calm down ma love! Please kaa chini nikueleze kwa utaratibu." Nikamueleza bila kujiamini na nikaanza kuona jinsi alivyokuwa anapandwa na hasira huku machozi yanamtoka.

"Ray, naomba unieleze kinachoendelea!" Cheupe akaongea bila kukaa chini kama nilivyomuomba na alikuwa amefura kwa hasira.
"Ok! Hasnat, nina sababu za kuamini kuwa watu walionitafutia wafadhili kwa ajili ya Sote Hub ndio wanaohusika na mauaji ya Waziri Kipanju na nina amini wanahusika na kukamatwa mzee wako!" Nikamueleza kwa hofu kubwa huku nikijaribu kuchunguza reaction yake usoni. Hasira nilizokuwa naziona zikabadilika na kuwa 'confusion'. Akafumba macho kwa sekunde chache akijaribu kuelewa nilichokuwa najaribu kumueleza.

"What the fu*k are you talking about? Ninavyofahamu ni Dr. Shirima mwalimu wako ndio amekusaidia kupata wafadhili." Akaniuliza bado akiwa na mshangao mkubwa usoni.
"It's much bigger than that?" Nikamjibu na kufumba macho kwa kujisikia aibu kwa nilichotaka kumuekeza. "Dr. Shirima ni sehemu ya watu wanaojiita The Board, sifahamu hasa wana malengo gani, lakini wao ndio wamenisaidia kupata wafadhili!" Nikajikuta nimeinamia chini nikiwa namueleza mambo hayo. Nilijisikia aibu kumueleza mambo haya leo.

"And..?" Hasnat akauliza kwa kifupi tu na nilihisi hasira iliyokuwa kwenye sauti yake.
"Well, wamekuwa wananipa maelekezo tu mambo ya kufanya, vijana gani niwaingie kwenye projects Sote Hub, project gani waanze nazo na mambo kama hayo" nikamueleze nikiwa najitahidi nirelax lakini ndani nikiwa na hofu kubwa kwani nilianza kuona hasira inarejea usoni kwa Hasnat.

"And hukuona umuhimu wa kunieleza yote haya miaka miatatu yote hii." Hasnat akauliza sauti ikiwa na hasira kweli kweli.
"Am so sory! Sikuona umuhimu wowote wa kukueleza mambo ambayo hata mimi mwenyewe siyaelewi vizuri. Na sikuwahi kuhisi yana ubaya wowote ule mpaka leo hii. Natamani nirudishe siku nyuma nifanye kitu sahihi. Am so sorry"

"Ray, I don't give a fu*k wewe na hao wenzako wa Freemason, sijui The Board mnafanya nini! I don't give a fu*k of what you do! Please muacheni mzee wangu, please please sitaki mzee wangu apotee please Ray! Kwanini umenifanyia hivi Ray." Hasnat akaongea kwa hasira ambayo sikuwahi kumuona nayo tangu nimemfahamu. Alikuwa anaongea huku amenifuata mpaka niliposimama na kuanza kunipiga vingumi. Uzuri vilikuwa vingumi vya kike, yes nilikuwa nimemkosea sana lakini pia vingumi hivi vilikuwa vya kudeka. Katika wakati mgumu kama huu nilijua ni kiasi gani alikuwa ananihitaji. Ni kiasi gani natakiwa kuwa imara kwa ajili yake.

Nikamvuta karibu yangu, akijitahidi kujitoa katika mikono yangu lakini nikamshinda nguvu! Nikamvuta kwa nguvu na kumkumbatia, akajitahidi kukukuruka atoke mikononi lakini nilizidi kumkumbatia kwa nguvu mpaka akatulia na kitu pekee alichoweza kukifanya ni kulala kifuani kwangu na kuanza kulia. Sidhani kama nimewahi kujisikia uchungu kiasi kile katika maisha yangu, nikajikuta nataka kutamka maneno lakini nikashindwa na kitu pekee nilichomudu kukifanya ni kumkumbatia zaidi.
"Am sorry honey! Am so sorry." Ndio maneno pekee nilifanikiwa kuyatamka na nikajikuta nayatamka tena na tena.

Nikamchukua Cheupe, nikaenda nae mpaka kwenye Sofa pembeni na nikampakata kama katoto kadogo. Mda wote huu alikuwa analia tu bila kusema chochote na mimi sikutaka kumzui kulia, nilijua kiwango cha uchungu ambacho atakuwa alikuwa nacho moyoni, nikaache atoe uchungu huo kwa machozi. Takribani dakika ishirini alilia na hatimae akanyamaza. Zilipita karibuni dakika kumi nzima baada ya kunyamaza lakini hakuna aliyesema chochote. Alilala tu kifuani, na mimi nilikuwa nimemkumbatia tu.

Kwa mara ya kwanza kwenye maisha yangu niliogopa kuanzisha maongezi na Cheupe wangu. Na yafaa zaidi kusema nilitamani tusiongee chochote kile. Tubakie hivi hivi milele. Alale kifuani kwangu, nimkumbatie namna hii milele. Tusiseme chochote, mioyo yetu tu isemeshane katika ulimwengu tusiouona. Niliogopa neno lolote, au sentesi yoyote nitakayo tamka inaweza kuanza kumliza tena Cheupe, na hakuna maumivu makubwa kama kushuhudia mpenzi wako wa maisha analia kwa uchungu na sababu ni wewe umemkosea.

Mara Hasnat akainua kichwa na kunitazama "so, you are one of them? The Board?" Akaniuliza huku akizungusha macho alipoitaja 'The Board.'
"No I'm not! Sio mwenzao mimi." Nikamjibu nikionyesha kukereka kwa kufikiria tu kwamba na mimi ni mwanachama wa The Board.
"Ray, unawezaje kukataa sio mwenzao wakati unashirikiana nao mwaka wa Tatu huu sasa?"
"Its complicated" nikamjibu kwa kifupi tu.
"So Mzee wangu anahusikaje kwenye……" Nikamkatisha kabla hajamaliza kuongea nikihisi muda si mrefu atapaniki tena.
"Ssshhh.! Please naomba tusiongee haya mambo sasa hivi. Please hasnat naomba pumzika. Tutaongea kila kitu asubuhi. Najua unaweza kuwa huniamini sasa lakini najua huwezi kutilia shaka kuwa nakupenda kuliko kitu chochote kile. So please naomba ulale, kutakucha asubuhi na nakuahidi kila kitu kitakuwa sawa! I promise you." Nikaongea kwa hisia za hali ya juu. Hasnat hakusema chochote kile, akaniangalia machoni kwa karibia dakika nzima kisha akashusha kichwa na kukilaza tena kifuani. Nikamkumbatia. Nikambusu paji la uso. Dakika chache baadae wote tukapitiwa na usingizi.


****************************


Japokuwa tulichelewa sana kulala, lakini saa kumi na moja na nusu nilikuwa nimeamka.
Tulikuwa tumelala pale pale kwenye sofa mimi na cheupe na alikuwa amelala juu yangu kifuani kama tukivyolala Jana usiku. Kwa hiyo nikajitahidi kuamka taratibu nisimshitue cheupe na nikamuacha aendelee kulala.
Nikaingia bafuni na kuoga haraka haraka kisha nikaingia chumbani na kuanza kupanga vitu kwenye begi dogo la mgongoni. Wakati nikiendelea kuweka vitu kwenye begi nikahisi mtu amesimama nyuma yangu mlangoni.
"Unataka kunitoroka?" Hasnat akaniuliza macho yakiwa bado yamelegea kutokana na usingizi kwasababu ya kulala mda mfupi.
"No najiandaa inabidi twende Dar, so ni vizuri uanze kujiaandaa pia" nikamueleza na hakunijibu nikamuona amegeuka tu na kuelekea bafuni.

Takribani dakika kumi tu baadae tulikuwa tunafunga mlango wa nyumba yetu na tunaekekea kwenye gari. Ajabu ni kwamba ilikuwa ni saa kumi na mbili kasoro kama dakika kumi hivi lakini tulimkuta baba bite yuko nje kibarazani kwao anabrush viatu. Nikajiuliza sana kama nimewahi kumuona mwenye duka yeyote duniani anabrush viatu asubuhi kama mwalimu au polisi anataka kuwahi ofisini. Nikahisi alikaa tu pale nje atuone tunavyotoka. Nikaona wacha nimfanyie mind game.

"Za asubuhi Mkuu!" Nikamsalimia kwa bashasha. Nikamuona kama ameshtuka hivi kwa kuniona niko kawaida. Nika note kitu kichwani.
"Salama kabisa Ray, shemeji za asubuhi?" Akanijibu na kumsalimia Hasnat.
"Nzuri shemeji, shikamoo" Hasnat akamjibu. Uzuri wa cheupe wangu huwa anajua kusoma akili yangu. Ingawa sikumwambia chochote ila usalimiaji wangu ule wa bashasha akahisi 'kuna jambo'. Hivyo na yeye akijitahidi kuwa kawaida na kusalimia kwa uchangamfu.

"Daaahh mkuu habari ya Waziri imekuwa kubwa kweli kweli, vipi hujasikia tetesi zozote kuhusu muhusika wa tukio?" Nikamuuliza.
"Hapana Mkuu sijajua bado" alijibu kwa kugugumizi kwa mbali na nikamuona amemuangalia Cheupe kwa kama nusu sekunde hivi. Nikanote kitu ningine kichwani.

"Daaahh yatapita bhana, and… Aaah sorry naelekea dar sahizi naweza kupitia gazeti la Mwananchi kuna tangazo la ofisi naweza kupeleka pale watuchapie kwenye gazeti lao, so ukinisaidia namba ya yule jamaa yako anayefanya kazi pale utakuwa umenisaidia sana, si unajua watanzania bhana tunaishi kwa kujuana hahahhah" nikamtega na kucheka kinafiki.

"Aaah daaahh Mkuu simu imezima chaji kabisa, itabidi nikutumie labda baadae" baba bite akajibu na nikimuona kabisa ameanza kuwa uncomfortable.

"Ooohh haina shaka Mkuu nipe tu hata jina lake." Nikamtega tena.

"Aaaahh anaitwa… aahh John! Yeah anitwa John.! John Joseph." Baba bite akanijibu akiwa totally uncomfortable.

"Nashukuru sana Mkuu" nikamjibu huku nabonyeza bonyeza simu nikijifanya kusevu nilichoambiwa.

Tukapanda kwenye gari na kuondoka. Tulipotoka tu nje ya geti Cheupe akaniangalia huku ana tabasamu.
"What the fu*k was that?"
"Hahahaha usijali, nikielewa nitakwambia maana hata mwenyewe bado sijaelewa mpaka sasa" nikamjibu na kucheka.
"Damn jamaa hajui hata kusema uongo" Cheupe akajibu huku akipokea simu.

Nikafarijika kuwa na cheupe ameona kuwa Baba Bite alikuwa anadanganya. Nikaanza kufikiria tena maongezi yangu na Baba Bite.
Nimemsalimia kwa bashasha lakini akashtuka. Kwahiyo alitegemea habari ya kifo cha waziri inishtue! Kwanini?
Nimemuuliza kama anajua kuhusu muhusika wa mauaji, akanijibu kwa wasiwasi huku anamkata jicho Cheupe! Yawezekana alifahamu kuhusu kukamatwa kwa Babake Hasnat, swali amefahamu vipi wakati habari hiyo bado haijawekwa wazi kwa vyombo vya habari.?
Pia nimemuomba namba na majina ya rafiki yake wa gazeti la Mwananchi na amenidanganya! Kwanini jana anidanganye kuwa taarifa ameipata kutoka kwa rafiki yake wa Mwananchi? Kwanini anifiche source yake? Anafahamu vipi mambo haya?

Nikamuweka kiporo.



"Tunaweza kuongea sasa kuhusu kinachoendelea?" Cheupe aliniuliza na kunizindua kutoka katika kumuwaza Baba bite.
"Yeah! Nikueleze tu juu juu maana na mwenyewe sifahamu kwa undani sana" nikaanza kumuelezea cheupe kila kitu. Kuhusu siku ya kwanza wakivyokuja nyumbani mwembe chai. Kuhusu nilivyotolewa damu. Kuhusu kikao chao mikocheni B. Na kuhusu karatasi za mkakati namba 0034.

"Oohh my god! So huo mkakati unahusu nini hasa?" Hasnat aliniuliza kwa mshangao baada ya kumueleza yote haya.

"Actually sifahamu sana! Nilipewa karatasi kama kumi hivi lakini sehemu kubwa zilikuwa kama zimefutwa hivi. Si unaonaga vile kwenye televisheni zile karatasi za top secret zinavyokuwa zimefutwa futwa na wino mweusi na kuacha mistari michache? Yes, zilikuwa namna hiyo. Kitu pekee ambacho nilikiona ni mkakati wa kuwezesha vijana, pia kuna karatasi ilihusu Sote Hub, kuna karatasi ilihusu sera mpya ya kuwezesha vijana, nahisi ndio hii iliyowasilishwa bungeni na Mhe. Zephania. Na karatasi ya mwisho ilikuwa na figures tu zinainyesha kiwango cha gesi na mafuta vilivyogunduliwa mpaka sasa na vitalu vyote vilivyopo pamoja na makampuni yanayomiliki vitalu hivyo.!"

"Aiseeeee! So unadhani hii inahusiana vipi na kuuwawa waziri kipanju na mzee wangu kuchaguliwa bodi ya TPDC na kukamatwa kwake".

"Siku ile Dr. Shirima alivyonieleza niwaombee vijana tenders, nilijiuliza sana why wametarget idara hizo za serikali na kampuni ya swala Energy. So nikaanza kufatilia kampuni ya Swala Energy, hawa jamaa wamepewa licence na serikali kufanya utafutaji wa mafuta kwenye bonde la ufa eneo la kilosa na kilombero toka mwaka 2008! Katika kufukunyua kwangu nikakuta kuwa thamani za hisa zao zimeporomoka sana kwenye masoko ya hisa miaka hii miwili. Pia mwaka huu walitakiwa wafanye drill ya kisima kipya kwenye eneo lao huko kilosa lakini ikahairishwa. Sasa licence yao ya kufatuta mafuta walipewa na serikali mwaka 2008 na inaisha mwakani 2017. Kwa mwenendo huu lazima serikali itakataa kuwapa licence mpya ya miaka minane mingine. Kwahiyo ninachokihisi ni kwamba The Board wanajaribu kushinikiza TPDC kubariki taarifa za uongo kuhusu maendeleo ya utafutaji mafuta huko kilosa na kilombero ili Swala Energy wasipoteze wawekezaji na serikali wasijue hali mbaya waliyo nayo ili iwape tena licence mwakani. Kwa hiyo ninachohisi mzee wako aliwekwa TPDC ili kusaidia kushawishi kukubalika kwa taarifa hizo za kupika! Ninachojiuliza je alikubali kutumiwa na The Board? Pia nahisi Waziri Kipanju aligundua hii ishu au akupewa taarifa nyeti kuhusu hili suala na alikuwa anazipeleka sehemu au alikuwa anataka kuzifanyia kazi mara moja ndio maana wakamzimisha fasta fasta! Maana wangeweza kutumia njia nyingine kumuondoa, lakini assasination ya dizaini hii inaonyesha suala la kumuondoa lilikuwa urgent kuzuia asifanye alichokusudia kukifanya kwa haraka. Pia bado sijaelewa kusudi la kunambia niwaimbee tends Morani Warriors kulinda Swala Energy."

Nilimueleza Cheupe kwa kina kile ninachokihisi. Aliganda kwa dakika kadhaa akitafakari kile nilichomueleza.

"Ooohh my gorsh! This is insane" Cheupe akaongea huku anafumba macho kwa uchungu.

"Be strong cheupe" nikamtia moyo.

Niliendesha kwa fujo kiasi kwamba ndani ya masaa mawili tu tulikuwa tumefika ubungo. Moja kwa moja tukaelekea ubungo plaza. Nilikuwa nimempigia simu school mate wangu Issack niliyesoma naye sekondari. Huyu alikuwa mtundu mtundu wa kompyuta. Hakuwa mchawi kiasi kile cha wale wa kwenye televisheni lakini alikuwa na utundu wa kutosha tu na uzuri chuoni alichukua shahada ya masuala ya kompyuta.

Tulipofika tu baada ya salamu nikamueleza nilichomuitia.

"Issack hii simu kuna mtu alinipa, naomba ufanye utundu wako nipate taarifa ya chochote utakachofanikiwa kukipata kuhusu simu hii" nilimkabidhi Issack simu niliyopewa na Dr. Shirima miaka mitatu iliyopita.

"Pia hii ni namba ya akaunti ya shirika linaitwa Alice Cartz Foundation, lipo Australia naomba pia taarifa zao zote ambazo utafanikiwa kuzipata hasa hasa donors wao na bodi ya wakurugenzi"
Nikamkabidhi kikaratasi kilichoandikwa namba ya akaunti ya wafadhili wangu wa SOTE HUB shirika la Alice Cartz Foundation pamoja na anuani yao ya ofisi.


Baada ya maongezi hayo kwa haraka tukaondoka kuelekea kituo cha polisi Oysterbay ambapo tuliambiwa baba yake Hasnat alipelekwa baada ya kukamatwa. Nje tulimkuta mama Hasnat na ndugu wengine na wakatueleza kuwa askari waliowakuta hapo wamekataa kuwajibu chochote mpaka pale mkuu wa kituo akifika.
Hatukuwa na jinsi tukasubiri mpaka majira ya saa nne mkuu wa kituo akawasili. Akatuomba radhi kwa kuchelewa kwani alikuwa na majukumu mengine. Baada ya kumueleza shida yetu kuwa tumefika kumuona ndugu yetu Mhandisi Jaffar Kumbea, akatujibu kwa mkato tu kuwa hayupo hapo kituoni kwao alishakuja kuchukuliwa na afahamu amepelekwa wapi.

Tulipomuuliza ni nani aliyemchukua? Akatujibu tu "watu wa serikali" wamemchukua. Wengine hawakuelewa ila binafsi nilimuelewa. Nilielewa "watu wa serikali" ni akina nani.

Tulitoka nje na kuanza kujadili nini tufanye. Wengine wakashauri tufanye press conference kushinikiza serikali iseme walipompeleka Mhandisi Jaffar Kumbea, wengine wakashauri tuende Wizara ya Mambo ya ndani tukaombe maelezo zaidi. Kama ilivyo ada kukiwa na tatizo alafu kikaitishwa kikao cha ndugu, kila mtu anakuwa mjuaji zaidi, hivyo Mjadala ulikuwa mkali haswa. Mpaka saa nane mchana bado tulikuwa kwenye mgahawa karibu na kituo cha Oysterbay 'tunajadili'.

Mara simu yangu ikaita, alikuwa ni Issack! "Give me some good newz!" Nilimjibu Issack baada ya kupokea simu na kusogea pembeni.

"Oohh yeah nina habari njema haswaaa! Hii simu bado nahaingaika nayo ila ile akaunti nimepata vitu verrrryyy interesting." Aliongea Issack kwa sifa kama kawaida yake.

"Really?" Nikamuuliza
"Yeah, nadhani vizuri uje hii sio ya kuongea kwenye simu!".

Nikakata simu. Nikamuita Cheupe pembeni, nikamueleza nilichoambiwa na Issack. Kisha nikamuaga na kuwasha gari Kuelekea Upanga kuonana na Isaack.



Issack amegundua nini kwenye akaunti ya Alice Cartz Foundation?? Baba Hasnat amepelekwa wapi na "watu wa serikali"?? Ni kitu gani anachokificha baba bite?? Na swali la Mkakati namba 0034 alijajibiwa.. Bado pia kuna maswali kuhusu kifo cha waziri kipanju..!!


Yote yatajibiwa Kesho Jumatatu kwenye Episode 4!!
 
NEW EPISODE (EPISODE 3) POST # 655



Divine... glory to yhwh Nifah BansenBurner Alisen Papushikashi Magazine Fire miss chagga succinate coA hydrogenase SANCTUS ANACLETUS mngony Excel Mussolin5 Jimena Inferiority Complex gwijimimi wambura marwa Hoshea Shareef Conscious wambeke The Boss deejay Nasmile gkileo Juma chief Mangi flani hivi Ngongo makaveli10 KENZY kadada wa pili Root aretasludovick jonnie_vincy Clkey KAFA.cOm mbewe makedonia Afande Nyati peterchoka Leonard Robert Nchi Kavu STUNTER Chrizo jully van persie Khalidoun Tetramelyz punje haradari Mazigazi Alybaba babu na mjukuu platozoom jimmyfoxxgongo Nicodemas Tambo Mwikozi Ls man Heaven Sent sifongo Infantry Soldier haa mym 20acres MTS MarkHilary compos Tembo2 Erick the future nancy1983 Bulah binsaad Fazzaly The Wolf Firegironsa everhurt Melvine Mgibeon kijana wa leo samsun Coolant Jagood pacesetter apologize payton George Betram kisengeli Kiranga Jiwe Linaloishi Madame B jay john Guasa Amboni Dinazarde Juma chief Analyse Diva Beyonce snowhite Mmanu Expected Value onechromosome Missy rose Innocenthezron Immortal_MH Ficus sunola Robot la Matope mamaafacebook II JEKI likikima Compact scorpio me G'taxi @gambada YNWA @adna yuzo ntamaholo Otorong'ong'o naan ngik-kundie kandukamo1 AFRICA101 mwalidebe Kobe Blaki Womani kalendi savius The Great Emanuel r2ga Ntaluke.N. Transcend Msemachochote Mchumiajuone mwampepec MTOTO WA KUKU Fukara proto cute kawombe zinginary MLALUKO JR Vupu barafu BlackPanther Ntuzu Matola impongo ntamaholo Mkoroshokigoli Deadbody King Easy mahoza Msolo kkenzki deborah1 Mazigazi KIDUDU buffalo44 winlicious RIZIKI ALLYS MUHUNZI Moses2015 nacktary Liuumi dochivele Renzo @barbers hmjamii mbere TATIANA famicho LUCKDUBE mwanadome StraTon MemPhis GhaZar Graph Theory Honey Faith Shunie Slave ddcmanesto zinginary pacesetter Nkanaga haa mym KOMUGISHA mikatabafeki johnsonmgaya lee empire wigo MJINI CHAI Asprin mtzmweusi Blaki Womani erasto kalinga Chrizo kichakaa man kulubule FORTALEZA poleni Mshuza2 shibumi ZE DONE gkileo umande Edger Sr sir joshua sammoo Roram Password Bavaria hambiliki mwanangu Clkey Asili100 Evarist Massawe nice1 Jumong S Rogie babake nasreen uberito baest dustless Kilemachocho Tumosa mtembea kwa miguu Debbs Joe scorpnose musacha shibumi seeker of knowledge Simuchi Veni Vidi Vici T-King gkileo mij TUJITEGEMEE abuu garcia Hon Nkundwe Festo Mwangungulu marion09 mike2k The dream bro kay vandelintz kirikou1 POINT LOAD lusaka city Dirham Rodcones bato MANCNOO multiphill90 George Dalali mwanamalundi90 MwaFreeca Roram
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom