VIPEPEO WEUSI: MKAKATI NAMBA 0034
EPISODE 17
Maneno ya Kaburu yalinishitua sana. Kwanza nilishtushwa na taarifa ya Vincent Mallya kuhusika na kujishughulisha na The Board. Vinncent Mallya alikuwa ni moja ya watanzania wanaoheshimika zaidi hasa kutokana na umahiri wake katika sekta ya kibenki, ambapo aliweza kuikuza kimtaji benki ya CRBB kutoka kuwa Benki ya kawaida tu mpaka kuwa benki inayoongoza nchini kwa huduma za kifedha.
Pamoja na hilo pia, mtihani wa kumtorosha Kaburu kutoka gerezani sio tu kwamba ulikuwa hauwezekani bali pia ulikuwa kama mpango wa ukichaa. Inawezekana vipi mtu kutoroka sehemu inayolindwa kiasi hiki? Hata gereza lenyewe likivyojengwa lilizingatia kwa kiwango kikubwa mtu asiweze kutoroka. Kuta zilikuwa kubwa na ndefu na zenye nyaya za miiba juu yake.
Nikamuangalia tena Kaburu ambaye muda wote alikuwa amesimama tu mbele yangu akiniangalia ninavyoumiza kichwa kuchambua kile alichonieleza.
"..ok! Tuseme kwa mfano nikapata namna ya kukutorosha humu, then what?" Nikamuuliza.
"Nikikanyaga tu salama nje ya hii ngome, nakupa hiyo taarifa na kila mtu anaelekea njia yake!" Akanijibu.
"Nitakuwaje na uhakika kwamba utatimiza hii ahadi unayosema?"
"Well, hakuna namna unaweza kuwa na uhakika, lakini nitatimiza"
"Ok! Let me think about this.." Nikamjibu.
"Na si hilo tu, kuna kitu kingine nahitaji pia"Akaongea huku hata yeye mwenyewe anajishtukia.
"Oooh God, what else? Usije ukasema unataka mikupeleke peponi" nikaongea kwa mzaha wa kumkejeli.
"Kuna nyaraka zangu muhimu nahitaji nizipate mpaka kufikia kesho jioni" akaongea kwa kumaanisha.
"Nyaraka gani? Kutoka wapi?"
"Nahitaji uwasiliane na mtu unayemuamini huko nje, kuna document iko kwenye e-mail nataka 'aiprint' kisha adelete kule kwenye e-mail na hizo nakala atakazo print nizipate kesho jioni"
"Hivi tuseme kwa mfano nikapata namna ya kukutorosha humu! Kwanini usisubiri mpaka ukiwa huko nje ili ufanye hiyo kazi mwenyewe?" Nikamuuliza kwa hasira kidogo.
"Nina maana kuzihitaji kesho!" Akanijibu.
"Maana gani?"
"Its non of your business! Au labda tu kwa kifupi nikudokeze, nahitaji hizo nyaraka kabla ya jumatatu kuanza ratiba aliyoisema mkuu wa gereza kwamba nianze kupelekwa shamba"
"Ok! Na hiyo email ni ipi?" Nikamuuliza.
"
guy13@gmail.com"
"Password?"
"veronica123100%"
"Wow! Mahaba niweke password hahaha" nikamuinjoi.
"Hahah umekariri?"
"Yeah got it! guy thirteen at gmail dot com, na password ni veronica one, two, three, one hundred percent..!" Nikamjibu huku natabasamu.
"Genius!" Akanisifia kwa kuniinjoi.
"Fu*ck you" nikajisikia tu kumtukana.
"Kesho nahitaji hizo documents Ray! Sio kesho kutwa, sio mtondogoo… Nazihitaji kesho" akaongea kwa msisitizo mkubwa.
"I will do my best" nikamjibu huku nageuka kuondoka eneo hilo.
Kengere ya chakula cha mchana ilikuwa inalia kwahiyo ndani ya dakika chache watu watajaa upande huu wa gereza ili waweze kwenda jikoni kuchukua chakula.
Nikatembea mpaka pale kwenye mlango mkubwa ukutani ambapo kuna mlango wa kwenda yard namba moja na kusubiri.
Kama dakika mbili baadae wafungwa na mahabusu wakaanza kumiminika wakipita hapo kuelekea jikoni.
"We fala ulikuwa wapi muda wote huu nakutafuta?" Godi akaniukiza baada ya kufika hapo mlangoni na kunikuta akiwa anaelekea jikoni.
"Nilivyotoka kuonana na Cheupe nikaenda moja kwa moja kuongea na Kaburu" nikamjibu huku tukiongozana kuelekea jikoni.
"Vipi Kaburu amefunguka hizo info?" Akaukiza kwa shauku.
"Kiasi tu! Kama asilimia hamisini bado asilimia hamsini hajaniambia"
"Na hizo info zilizobakia anakwambia lini?"
"Hata leo hii anaweza kunambia nioitimiza tulichokubaliana"
"Usinambie kuwa anataka umpe tigo hahahahah!!" Akaongea kwa mzaha na kuanza kucheka.
"Mseng* wewe!! Bora hata angetaka tigo ninhekuja kukushawishi umpe.. Anachokitaka hata hakiwezekani!!" Nikamjibu pia kwa mizaha.
"Anataka nini?" Akaniuliza akiwa ameacha kucheka sasa.
Nikamsogelea karibu na kumnong'oneza, "anataka nimsaidie kutoroka humu gerezani."
Godi akapiga mluzi wa mshangao kwa sauti ya chini, "mamaeeeeee! Kazi unayo.. Nasubiri nione huo muujiza wa karne ya ishirini na moja"
Tukapanga foleni na kisha kuelekea jikoni kuchukua chakula.
Zilikuwa ni siku sita pekee tangu miingie humu gerezani lakini moja ya mateso makubwa ilikuwa ni chakula.
Sio kwamba ulikuwa unapewa chakula kidogo au hakuna chakula, hapana bali ilikuwa ni aina ya chakula chenyewe ma ratiba ya kula.
Ratiba ilikuwa kwamba mnakunywa uji saa moja au moja na nusu asubuhi. Baada ya hapo chakula cha mchana mnakula saa nane mchana. Basi siku ndio imeisha. Milo miwili tu. Uji saa moja asibuhi na chakula mchana saa nane.
Pia chakula chenyewe kilikuwa ni mtihani mwingine. Lilikuwa ni dona lakini ni dona ambalo sikuwahi kuliona maishani mwangu mwote na wala sikufikiria kuna dona la dizaini hii.
Dona lilikuwa na rangi fulani hivi kama njano lakini imechanganyika na rangi nyeusi. Mwanzoni nilipoingia gerezani niliuliza labda yawezekana wanatumia mahindi ya njano ambayo wazee wetu wanatusimulia kuwa yalikuwa yanagaiwa kipindi cha njaa enzi za nyerere? Nikaambiwa sio mahindi ya njano, nj mahindi ya kawaida tu ila ni jinsi hilo dona linavyoandaliwa ndio linafanya kuwa na rangi hiyo.
Nikaelezwa kwamba. Katika usagaji wa hilo dona, yanachukukiwa mfano magunia matatu ya mahindi ambayo hayajakobolewa, kisha yanachanganywa na gunia moja la vibunzi tupu. Yaani vibunzi ambavyo vimeoukuchuliwa hazina mahindi. Kisha vinasagwa pamoja. Ndio unaoatikana ungwa wa dona linalopikwa magereza.
Kinachochosha zaidi ni kwamba dona hili kulila ni kila siku. Kila siku ni dona hili la ajabu na maharage. Na hayo maharage yenyewe yalikuwa ni kiroja kingine.
Unapoenda pale jikoni kuchukua chakula, kuna madirisha makubwa matatu.
Dirisha la kwanza unakabidhiwa "berenge"! Hili ni bakuli kubwa la bati ambalo nahisi kipimo chake unaweza kujaza chakula sahani tatu kutoka kwenye sahani za kawaida.
Ukishachukua berenge, unahamia dirisha la pili ambapo unampa mpishi lile berenge na anakujazia dona mpaka juu.
Kisha unahamia dirisha la tatu ambalo unapewa kikombe cha bati kilichojazwa mboga. Maharagwe.
Kikombe kinakuwa kimejaa "mchuzi" mpaka juu lakini unaweza kuzamisha kiganja kizima cha mkono kuyatafuta maharage na usiyaone. Kuna siku nilipopewa hiki kikombe cha maharage na kurudi yard kula, nikafanya uchizi kidogo! Nikamimina mchuzi wote chini ili niyaone hayo maharage.
Nikayakuta yametuama chini kabisa. Nikayahesabu nikapata punje 12 za maharage. Hiyo ndiyo mboga unayotakiwa kukia dona ulilojaziwa kwenye berenge.
Nikachukua dona langua na tukaondoka na godi kwenda yard kula.
************************
SIKU YA TANO
Ilikuwa jumapili, siku nyingine ya wafungwa na mahabusu kuja kutembelewa na ndugu zao, jamaa na marafiki.
Nilishukuri kwa jinsi Cheupe na Issack walivyokuwa wanakuja mapema sana kuniona. Kama nilivyosema hii ilitupa mwanya wa kuwa peke yetu kwenye chumba cha wageni.
Jina langu lilikuwa limeitwa na sasa ndio nilikuwa nimeingia ndani ya hiki chumba nankukaa chini nikisubiri wageni wangu wakiwa wanakamilisha taratibu za kujiandikisha huko nje ili wapewe ruhusa ya kuingia.
Nilikuwa namsubiri kwa hamu kubwa Cheupe wangu! Walau kumuona tu roho yangu ilikuwa inapata faraja na kunipa nguvu ya kupambana zaidi.
Mara mlango ukafunguliwa na wageni wangu wakaingia! Lakini ajabu ni kwamba hawakuwa wageni, Bali alikuwa ni mgeni.
Nikishikwa na butwaa na mshtuko kwani sikutegemea hili. Dr. Shirima ndiye aliyeingia kwenye hiki chumba.
"Hujambo Ray?" Akanisalimia kwa tabasamu kama kawaida huku anaketi kwenye kiti.
Nilishindwa kumuitikia, nikabaki nimemkodolea macho tu.
"Ulipata Ujumbe wangu?" Akaniuliza baada ya kuketi kwenye kiti.
"Ujumbe gani?" Nikajikuta nimemjibu pasipo mwenyewe kutaka kimjibu.
"Ujumbe wangu kuhush kikao cha kumi na nne, tukutane kwenye makazi ya askofu? Uliupata?" Akaniuliza tena.
"Yes niliupata!" Nikamjibu kwa mkato.
"Kwanini haukutokea?"
"Well, labda kama hujagundua hapa sio Kempiski!! Niko gerezani na siwezi kutoka tu kama naenda sokoni" nikamjibu huku nimekereka kweli kweli.
"Hahaha! Ray, upo gerezani kwa kuwa umetaka kuwa gerezani" akanijibu huku anatabasamu tena. Hili tabasamu lilinikera kweli kweli.
"What do you want??" Nikamuuliza kwa hasira.
"Hahaha! What do i want?? Lets see, haujawahi kukosa kuhudhuria hata kimoja nilichokuita.. Lakini kikao hiki cha 14 haukuja.. So nikahisi labda umechoka kuja ninapokuita.. So nimeona labda itakuwa vyema mimi nikija ulipo" akaongwa kwa kejeli huku anatabasamu.
"Bulksh*t!! What the fu*k do you want?" Nikamuuliza kwa hasira.
"What do I want?? Hahaha, what the fu*k you think you are doing?" Akaniuliza pia kwa hasira. Akaendelea "chochote kile ambacho watu wa Usalama walichokushawishi mpaka ukakubali uwanyie kazi jua kwamba wanakudanganya na kukurubuni"
"I'm not working for anyone! Not you motherfu*ckers, not them" nikajibu kwa hasira mpaka nikasimama kutoka kwenye kiti.
"Then get the hell out! Unanisikia Ray, chochote ulichokipanga kichwani kwako nakupa nafasi kwa mara ya kwanza na ya mwisho.. Get out of here, na ukitoka moja kwa moja nataka uje nilipokuelekeza katika ujembe wa kikao namba 14" akaongea kwa hasira pia huku anasimama.
"Only in you dream dr. I'm done with you guys!" Nikaongea huku naanza kugeuka ili nitoke kwenye hiki chumba.
"Jumatatu italetwa hati ya dharura hapa kwa ajili yako ili upelekwe mahakamani! Ukifika mahakamani kesi itafutwa.. Baada ya hapo nataka uje moja kwa moja ulipoelekezwa kwenye ile karatasi.. Usijifanye shujaa.. Fikiria mara mbili mbili before its too late, huwezi kupambana na The Board!! Watakupoteza.. So acha kuwa mjinga na mbinafsi, Fanya ninachokuambia kwa ajili yako, kama sio kwa ajili yako Fanya kwa ajili ya cheupe, na kama sio Cheupe fanya kwa ajili ya mtoto aliye tumboni kwake"
Nilishikwa na mshtuko, moyo ulinipasuka nusura nidondoke chini.
"Umesemaje??" Niligeuka kutoka mlangoni nilikokuwa naelekea na kumtazama Dr. Shirima usoni na kumuuliza kwa hasira na mshangao.
"Umenisikia vyema tu naamini! Think about it" Dr. Shirima akaongea huku anaondoka kutoka kwenye chumba cha wageni.
Nilibaki nimesimama nimeganda kwa mshangao akili ikizunguka. Ile sentesi ikawa inajirudia kichwani, "fanya kwa ajili ya mtoto aliye tumboni kwake". Sikuamini masikio na macho yangu. Moyo ulienda mbio kijasho chembemba nikaanza kukisikia kinaanza kunitoka.
"Rweyemamu usitoke una wageni wengine" nikamsikia askari wa mapokezi anaitilia.
Nikaketi chini kwenye kiti. Akili bado ilikuwa inanizunguka. Ile sentesi ya Dr. Shirimanilikuwa inajirudia tena na tena kichwani mwangu. "fanya kwa ajili ya mtoto aliye tumboni mwake".
Mlango ukafunguliwa na Cheupe na Isaack wakaingia.
"Niaje kichwa?" Issack akanisamia mara baada ya kuingia kwenye chumba cha wageni.
Tukasalimiana na Issack. Kisha nikasalimia na Cheupe.
Baada ya hapo Issack kuna kitu akaanza kunielezea nadhani kuhusu ile akaunti ya Foundation kutoka Australia. Lakini akili yangu yote ilikuwa haifanyi kazi, nilikuwa nafikiria tu ile kauli ya De. Shirima, "fanya kwa ajili ya mtoto aliye tumboni mwake".
Cheupe alikuwa amekaa lakini kwa namna Fulani hivi nilimuona hakuwa na raha na uchangamfu kama kawaida yake. Na kila nilipomuangalia machoni alikuwa anakwepesha macho.
"Umepanga uniambie lini?" Nikauliza huku namuangalia Cheupe.
"Whaaaatt???" Issack akakatisha alichokuwa anaelezea na kuduwaa.
"Is it true?" Nikauliza tena huku namuangalia Cheupe.
"What is it Ray?" Cheupe akaniuliza huku ameshangaa.
"Are you pregnant?" Nikamuuliza.
Wote wawili wakashtuka ghafla. Wakatoa macho.
"Umejuaje?" Issack akaropoka.
"Haijalishi nimejuaje!! Is it true?" Nikauliza nikiwa na hasira kidogo iliyochanganyika na furaha.
"Aaahh wiki nzima hii Hasnat alikuwa anaumwa umwa na juzi hapa akaanza kutapika tapika na hali ikazidi kidogo.. So usiku tukaenda town hapo hospitali ya Agha Khan na baada ya vipimo vipimo.. ndio ikabainika kuwa ni mjamzito" Issack akaongea huku ana tabasamu.
Nilishikwa na furaha ya ajabu nikatamani niruke nioenye kwenye zile nyavu na kumkumbatia Cheupe.
"Kwanini hamkuniambia toka jana" nikafoka kwa furaha huku nimesimama kutoka kwenye kiti.
"Well, niliona na wewe kuwepo humu gerezani alafu nikupe taarifa za ujauzito naweza kukuchanganya hata mipango unayoipanga akili ikashindwa kutulia nankuifanya" cheupe akaongea kwa woga kiasi Fulani lakini akiwa na furaha.
"Haijalishi niko wapi au nina hali gani, that's my son lazima unipe taarifa" nikafoka tena kwa furaha..
"Your 'son'?? Macho yako yana ultra sound au?? How do you know its a boy??" Cheupe akaongea huku anacheka kwa furaha.
"Ok ok ok guys mtapata muda wa kusheherekea.. Let's get down to business.. Hivi huyo tuliyepishana naye hapo nje si ni Dr. Shirima??" Isaack akauliza kwa mshangao.
"Yes ni yeye! Akikuja kunipiga mikwara" nikamjibu huku nikaa tena kwenye kiti baada ya kuinula kwa furaha.
"Amesemaje?" Cheupe akauliza.
"Akichosema sio muhimu ni mikwara tu" nikamjibu huku najitahidi kuficha uongo wangu wasigundue kuwa nawadanganya. "Kuna jambo la muhimu nataka mlifanye." Nikaongea kwa utulivu huku nawatazama.
"Jambo gani?" Akaniukiza cheupe.
Nikawaeleza kuhusu ile email ambayo wanatakiwa wakaprint document iliyopo na kisha kudelete hiyo document kwenye email. Na pia nikawaeleza kuwa wanatakiwa document hiyo ifike hapa gerezani leo jioni kabla hatujaenda kulala. Hivyo nilichowaelekeza ni kwamba wakiileta hiyo document hapa magereza wakamkabidhi askari anayeitwa 'Obama' na yeye Obama atajua namna gani ya kunifikishia hiyo document kwa siri.
"Kitu kingine ni kwamba nahitaji jumatatu mje mahakamani! Niatapelekwa mahakamani na kuachiwa huru"
"What? Kesi yako si ni tarehe 8 wiki ijayao" akauliza cheupe.
"Yeah, italetwa hati ya dharura kunipeleka mahakamani.. Nahitaji muwepo.. Msiumizw kichwa nini kinaendelea, I just want you to be there! Sawa?"
Nikamuangalia Cheupe.
"Honey, nahitaji use strong mama'ngu.. We are very close kulimakiza hili.. Tafadhali sana mama be strong for me and for our baby" nikaongea kwa hisia Kali huku nimemkazia macho Cheupe.
"Najitahidi baba! But am really scared" Cheupe akaongea huku vimachozi vinamlenga lenga kwa mbali.
"Cheupe unakumbuka ile stori niliyokwambia kipindi tuko sekondari mzew wako alipotaka kukufukuza kwasababu ya kuwa na uhusiano na mimi?" Nikauliza kwa hisia.
"Yes nakumbuka" Cheupe akaongea huku machozi yanamtoka taratibu.
"Tell me that story"
"Ray noooo! Pleaseee" Cheupe akalia zaidi.
"Please naomba unambie ile srori" nikajikuta kwa mbali machozi yananikaribia kutoka.
Cheupe akafumba macho kwa hisia na kuyafumbua kisha akaanza kusimulia.
"Uliniambia kuwa kulikuwa na panya wawili wametumbukia kwenye glasi ya maziwa.. Baada ya kutumbukia wakaanza kutapa tapa kwa kupiga piga miguu ili wasizame chini.. Wakafanya hivyo kwa karibia dakika kumi nzima.. Panya mmoja akamwambia mwenzake kuwa hakuna point ya kupiga piga miguu hivyo kwasababu mwisho wa siku watachoka na watazama na kufa.. Hivyo ni bora tu wafe kwa amani bila kutapa tapa.. Yule panya mmoja akaacha kupiga piga miguu na akazama kwenye glasi na kufa.. Lakini yule panya mwingine akaendelea kupiga piga miguu na kutapa tapa ili asizame… Akafanya hivyo kwa dakika kumi nyingine kwa maumivu makubwa kwa kuwa alikuwa amechoka sana..
ingawa yule panya alikuwa hajui ila ni kwamba maziwa yakikaa yametulia muda mrefu na ukaanza kuyatingisha kwa nguvu ghafla yanatengeneza margarine.. Yani mabonge mabonge ya siagi.. Kwa hiyo baada ya muda kadiri yule panya alivyo tapa tapa na kupiga piga miguu, maziwa yalitengeneza mabonge mabonge ya margarine na hatimaye yule panya akayatumia kuyakanyaga juu yake na kutoka kwenye glasi na kuendelea na maisha, akiwa hai na salama"
Cheupe akieleza kwa ufasaha kabisa hadithi ya kumtia moyo niliyomweleza miaka mingi sana iliyopita tukiwa wanafunzi wa sekondari.
"That's the spirit honey! We don't ever give up.. Please stay strong for me.. Karibia tunalimaza hili.. Stay strong please"
Nikaongea kwa hisia kubwa na Cheupe wangu.
"Yes! Honey I will do that.. for us and and for this baby" Cheupe akaongea huku anapapasa tumbo lake.
Baada ya hapo tukaagana na wakaondoka. Nikatoka mle ndani nikiwa na nguvu mpya na usongo zaidi. Kwamba sasa napaswa kupambana si kwa ajili ya baba yake Cheupe tu, au kwa ajili ya Cheupe tu bali napaswa kupambana kwa ajili ya mwanangu.
Itaendelea Ijumaa Episode 18…