Wangari Maathai
JF-Expert Member
- Aug 13, 2018
- 34,959
- 70,694
Mwanjelwa ni balaa, pamechangamka Sana kuibiwa nje nje! Hahaha ubora wa familia ulikuwa unapimwa kwa kutazama tranka lako limesheheni vitu gani unapotoka likizo! Kuna jamaa akaja na maandazi halafu usiku anakula gizani, tunasikia tu harufu ya maandazi tunamvumilia. Siku ya Jumapili kaenda kanisani huku nyuma tukatekenya kufuli la tranka lake likafunguka, tukakuta hela na maandazi kibao na asali! Tukachukua maandazi na asali tukala! Aliporudi akasema, "Ninachoshukuru hamjachukua hela yangu ya ada, Asanteni Sana!!"
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣! Kuna kidenti kilitoka USA kikaja shule yetu..kikawa kina makormbwezo kibao Ila kichoyo balaa...wakanipa kazi hiyo Mimi...maana mm walishanizushia nimechanjiwa🤣🤣! Nilikua nna uwezo wa kuiba popote bila kustukiwa😆😆! Jikoni naongea na chefcooker huku mkono mwingine unasomba maandazi..bas Yule demu nikasema. Ntakufunza adabu...nilikua mjuzi Sana wa kucheza na kufuli na zip yoyote Ile ..tukafungua tranka Ina kila kitu cha kula .kula balaa maziwa na mijuice fulan ilikua maarufu miaka Ile ..dogo alirudi hostel kufuli liko vile vile .dah Yale maisha yalikua Hakuna stress...
Orchard ya shule nyanya zikikomaa tu had boys wananifata..oya nyanya zimekomaa ..natambaa umbali mrefu balaa nimebeba nyanya mgongoni nisionekane.. mnatengeneza kachumbari na wali saaafi kbs.shenzi Sana Yale maisha





