Vipande vya fedha dhidi ya uhai wangu

Vipande vya fedha dhidi ya uhai wangu

dawa yenu

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2014
Posts
2,829
Reaction score
3,733
Maisha ni safari yenye mambo mengi. Ni kama kitabu cha simulizi kilichosheheni kurasa nyingi zenye visa na mikasa ya kila aina. Ni safari yenye vituo vingi na huwezi kuviacha kwa kuwa hivyo ndivyo hutengeneza historia za Maisha yetu. Ukiwa na furaha kinyume chake ni huzuni, kwenye upendo jirani yake ni chuki, kuna ujinga na werevu. Sasa sijui ni ujinga, ushamba au tamaa iliyonifanya nikaweka rehani uhai wangu kwa ajili ya shilingi elfu mbili, yaani Tsh 2000/= taslimu!

Likizo ilikuwa imeisha, nilitakiwa kurudi shule na kama kawaida nilikuwa nishavuta wiki moja bila sababu ya msingi. Sisi ambao tulikuwa tumejiunga na "makundi" badala ya marafiki shuleni tuliamini kuwahi shule ni tabia za Wasafwa kutoka Mbozi. Iyunga boys enzi za Headmaster Kisusange, uwe Msafwa halafu unatokea Mbozi ilikuwa ni technical error!

Bi mkubwa alikuwa ananipenda sana japo hatukuwahi kukaa nusu saa bila kupishana kauli, basi akanikaangia kuku mzima akaniwekea kwenye boksi pamoja na dagaa wa kukaanga, Chill source, juice bila kusahau blueband na vikorombwezo kibao ili mwanae nisiwe na stress nisije bure nikafeli NECTA maana nilikuwa kidato cha pili! Kumbe huko shule mwenzake sina marafiki nina makundi. Mshua akanipa simu yake aina ya Panasonic niende nayo shule halafu akanishikisha kitita cha shilingi laki mbili.

Just imagine, ada sh 35,000, nauli sh 8,000 hadi Mbeya, njiani ninakula chipsi mayai, mishkaki na soda jumla sh 3000, halafu sh 200 nitampa mtu anibebee mizigo stendi, nauli ya daladala kutoka stendi Hadi shule sh 50. Shuleni lazima nifike na 150,000/= hiyo ni yangu binafsi, kuhusu chakula shule inatulisha tena jumatatu, jumatano na ijumaa tunakula nyali (wali) Mungu anipe nini? Mimi ni tajiri wa fedha na mali, Panasonic!

Nilifika hadi shule! Bahati mbaya makundi yangu yalikuwa hayajaripoti. Nikaweka tranka vizuri, nikachukua laki moja nikaingia zangu Mwanjelwa kununua viatu "four angle", huwezi kuwa mjanja halafu unavaa viatu vya shule, lazima uvae four angle zilizopigwa marufuku! Laki moja mfukoni, Panasonic mkononi, kwenye tranka Nina kuku mzima na blueband! Mimi ndio Mimi utaniambia nini?

Nimetegesha alarm kwenye simu kila nusu saa lazima nipigiwe, ninakata alarm naweka simu sikioni halafu naitoa halafu nalalamika "Aah kumbe anadip! Uza simu acha kudip" Nilikuwa zaidi ya Don. Nikanunua four angle, safari ya kurudi shule ikaanza na ndio hapo shetani akajiinua machoni kwangu.

Katikati ya Mwanjelwa kuna jamaa akanipiga begani! Nikageuka kwa chuki na hasira, jamaa mwenyewe kumbe mshamba tu! Ana lafudhi ya kisafwa, technical error! Akaniuliza ilipo shule ya msingi Umoja! Nikamwambia siijui! Kabla sijaondoka akapita jamaa mwingine na yeye akaulizwa swali hilo hilo akasema hiyo shule ipo hapo chini sio mbali.

Msafwa akaomba yule jamaa ampeleke hapo shuleni ila jamaa akagoma akasema ana madili mengi sana anayawahi! Msafwa akamwambia asijari atampa buku mbili ya usumbufu, mzee wa madili ikabidi akubali. Msafwa akaniambia mimi kwa sauti ya chini eti niwasindikize atanipa na mimi buku mbili maana yeye mgeni hapa mjini hamuamini mzee wa madili, ananiamini mimi! Sikumshangaa Msafwa kuniamini Don mwenye Panasonic yangu na kuku mzima kwenye tranka!

Mfukoni nilikuwa nina Kama sh 80,000 hivi, ongezea hiyo buku mbili inakuwa 82,000 taslimu. Hakika mwenye nacho huongezewa, nikakubali kuwasindikiza! Tukaanza kukatiza mitaa na vichochoro huku Msafwa anaongea Kama chiriku! Mzee wa madili na mimi Don tumekausha tu!

Kumbe Msafwa ni mganga bwana! Akasema kwenye hiyo shule kuna mwalimu mjamzito ila ni mwaka Sasa hajajifungua, tumboni kuna jini ndio anampelekea dawa ili Hilo jini litoke halafu ajifungue! Mganga alitoa Siri za mgonjwa! Mzee wa madili akawa mbishi eti anasema hizo story tu!

Mganga akasema hata wewe najua umekuja hapa Mbeya umekimbia kijijini kwenu Kuna mwanafunzi umempa mimba unaogopa kufungwa! Nikuambie tu umewekewa tego miaka miwili ijayo utakuwa kichaa! Mzee wa madili akapagawa! "Daah aisee kweli bwana, daah kumbe wameniwekea tego daaah... Aisee duuh" Mimi kusikia hivyo nusu nijikwae, jasho likanitoka, pumzi zikabadilika! Kumbe Msafwa ni gwiji!! Aisee.

Basi gwiji akaniangalia akasema mwanafunzi unaitwa Nani? Khaa!! Amejuaje Mimi mwanafunzi? Nikajitambulisha! Akasema, "kijana wangu, una moyo mzuri Sana! Unaonekana ulipokuwa mtoto uliwahi kuumwa." Hii ni kweli, nani hajawahi kuumwa alipokuwa mtoto? Nikatikisa kichwa kuafikiana nae basi Gwiji akaendelea, "ulirogwa na jirani yako, ni mama mtu mzima, nywele zake zina mvi!" Shabashhh... Mama Helena (RIP) ana mvi! Ni yeye! Ni yeye!

Gwiji akasema huyo mama ameniwekea nywele za maiti ya bubu kifuani kwangu, ipo siku nitapata ajali ya gari nitakuwa mlemavu maisha yangu yote! Daah nimemkosea nini mama Helena!? Gwiji ana roho nzuri akaniambia atanipa dawa ya kuondoa hizo nywele maana nimemsaidia sana! Hapo hapo mzee wa madili na yeye akataka apewe dawa, gwiji akasema tutafute sehemu tukae ili atutengenezee dawa! Mzee wa madili akasema kuna sehemu anaijua twende tukakae!

Tukaenda kwenye jumba bovu, lina vipisi vya sigara kibao, rizla za kutosha, karata kila sehemu, yaani tulienda makao makuu ya wahuni nyanda za juu kusini! Na njia ya kurudia siijui! Chap chap Gwiji akaniambia nitoe karatasi, nikatoa karatasi niliyokuwa nimefungia viatu nikampa! Akaiviriga ikawa Kama goroli, akanipa akasema niimung'unye!

Basi nikaanza kuimung'unya ikawa inajivirigua mdomoni, Heeh! Kumbe zilivirigwa nywele, nikadata! Gwiji akasema tema, nikatema nywele na karatasi! Akasema nwele za kifuani zimeishatoka. Ghafla akashika kichwa akasema mwanafunzi una matatizo mengi Sana! Nikataka kulia!

Ghafla wakatokea jamaa wawili warefu, wameshika fimbo! Bila maelezo wakamkamata gwiji na mzee wa madili wakaanza kuwachapa fimbo za nguvu! Walipigwa hovyo hovyo hadi damu, Mimi nipo tu pembeni nafanya sala ya toba! Unapata wapi ujasiri wa kumpiga Gwiji?
Kilikuwa kichapo heavy. Tukachukuliwa wote watatu hadi kituo cha polisi. Kumbe wale jamaa ni askari! Wakaanza kuwahoji Gwiji na mwenzake!

Mlikuwa mnampeleka wapi huyu dogo? Tumewafuatilia mwanzo mwisho washenzi nyinyi! Hayo mahojiano yalikuwa yanasindikizwa na makofi mubashara. Nikaulizwa ilivyokuwa nikasimulia kila kitu, ndio nikaambiwa wale ni matapeli, wangeniibia Hadi nguo nilizovaa! Nikaulizwa kwanini naweka rehani uhai wangu kisa buku mbili? Kule wangeniua ingekuaje? Yaani buku mbili tu, nikajiona bogus pale! Walipojua Mimi ni mwanafunzi kuna askari akanichukua Hadi stendi ya daladala, akanipakiza akaniambia nisiwe natembea peke yangu mjini, nitatapeliwa!

Nikarudi shule nimechoka mwili, roho na akili! Nikala kuku robo huku nikitazama four angle zangu vile nitapendeza jumatatu! Necta nilifanya vizuri Sana na mama alifurahi Sana ambacho hakujua ni kwamba hakuna mtihani uliowahi kuvuja Kama ule tuliofanya sisi! Majibu tulikuwa nayo way back before paper!

Swali linabaki Ulikuwa ni ujinga, ushamba au tamaa!? Kwa buku mbili nikaweka rehani maisha yangu!
 
Ukiacha kutaka kutapeliwa inaonekana unadeka sana sasa kuwa mgumu
 
Mkuu dunia ina mambo, mimi kipindi nipo shule wakati mmoja narudi likizo kuna bwana mmoja tulikaa nae seat1, tuliposhuka stand akanambia tupate chakula mgahawani tukapata...

Cha ajabu wakati tunatoka mgahawan alinishika mkono nikahisi ka nimepgwa shot mkononi dah! nilipga kelele nakukimbia jamaa akabaki anacheka tu, sasa sijui alikua akinifanyia jambo gani hadi leo sijapataga kujua.
 
Nimesoma huku nacheka balaa..sura ya Mwanjelwa ikinijia...mie siuaminigi kbs habari za ushirikina .Ila Kwa Mwanjelwa naamini uchawi upo..Bora we hukuibiwa .mie nilipigwa kweupeee🤣🤣! Enzi hizo form 2! Dadek....umenifurahisha Sana na habari za matrank na kuku na blue and😆😆😆
 
Mkuu dunia ina mambo, mimi kipindi nipo shule wakati mmoja narudi likizo kuna bwana mmoja tulikaa nae seat1, tuliposhuka stand akanambia tupate chakula mgahawani tukapata...

Cha ajabu wakati tunatoka mgahawan alinishika mkono nikahisi ka nimepgwa shot mkononi dah! nilipga kelele nakukimbia jamaa akabaki anacheka tu, sasa sijui alikua akinifanyia jambo gani hadi leo sijapataga kujua.
Bahati yako kelele na mbio zilikukomboa
 
Nimesoma huku nacheka balaa..sura ya Mwanjelwa ikinijia...mie siuaminigi kbs habari za ushirikina .Ila Kwa Mwanjelwa naamini uchawi upo..Bora we hukuibiwa .mie nilipigwa kweupeee🤣🤣! Enzi hizo form 2! Dadek....umenifurahisha Sana na habari za matrank na kuku na blue and😆😆😆
Mwanjelwa ni balaa, pamechangamka Sana kuibiwa nje nje! Hahaha ubora wa familia ulikuwa unapimwa kwa kutazama tranka lako limesheheni vitu gani unapotoka likizo! Kuna jamaa akaja na maandazi halafu usiku anakula gizani, tunasikia tu harufu ya maandazi tunamvumilia. Siku ya Jumapili kaenda kanisani huku nyuma tukatekenya kufuli la tranka lake likafunguka, tukakuta hela na maandazi kibao na asali! Tukachukua maandazi na asali tukala! Aliporudi akasema, "Ninachoshukuru hamjachukua hela yangu ya ada, Asanteni Sana!!"
 
Daaah enzi hizo kwa ishu za shule Mbeya ilikuwa vizuri. Nawamisi wadada wa Loleza, walikuwa wananipenda siku za disco na Iyunga eti Mimi mdogo mdogo siwezi kuwafanya kitu!


🤣🤣🤣Those days...dah..Raha Sana jamani! Wadada wa Loleza enzi zile walikua chakaramu balaa
 
Back
Top Bottom