Mtoto wangu hata awe na kipaji vipi, lazima aende kusoma.
Akisha soma nikajua ana elimu ya kutosha, hapo sasa yeye ndo ataamua kufanya nini, huo ni uchaguzi wake.
Si naye mmoja yeye anaitwa messi hahaha, lakini usiombe mama yake amemzungushia walimu, yani anaenda kucheza tena anapewa time saa flani awe karudi.lakini vipaji vingine vinatakiwa
kuendelezwa tangia utotoni
mfano mpira
unasemaje hapo?
The Boss bado sana hatujajua namna ya kuhandle issue za watoto ambao wana hivyo vipaji wakiwa wadogo
Bado hatujaweza kuviendeleza na hakuna shule maalum za kufanya hayo mambo na kuwaweka katika misingi ya kuwa pamoja na kipaji chako elimu nyingine iendelee
At least kungekuw ana namna ya kuwafanya watoto waendeleze vipaji vyao na huku wakiwa wanaendelea na elimu ya kawaida hapo sawa
huku unaweza kumwachia aendelee na kipaji chake ukajikuta hata muda wa kupata elimu ya kawaida hakuna na anaishia kupata umaarufu ambao utamcost baadae bila kujua kuwa kipaji chake kinatakiw akuendana na elimu
The Boss na wana jf wote mliochangia hii hoja nzuri sana nami nimejifunza mambo muhimu, kwangu mm nadhani elimu ni msingi wa kila jambo ktk dunia ya leo, ni bora adumaze hicho kipaji ili apate elimu kwani naadhani itakuwa ni namna pia ya kukiendeleza hicho kipaji kwa manufaa/mafanikio makubwa zaidi, na bila elimu anaweza kuneemesha wengine bila yeye kutabua...
Unaweza ukamruhusu mtoto ku-EXPLORE ki/vipaji vyake
huku ukim-limit kwa kiasi fulani badala ya kumu-EXPOSE all the way.
Ulaya (naongea from experience) . . .watoto huwa wanaenda shule kama kawaida huku pembeni (muda wa ziada) wakijifunza/hangaika na hivyo tunavyoweza kuita vipaji. Kama ni kupiga chombo cha mziki, kucheza michezo ya athletic, kuimba, kucheza mziki vinakua ni "SIDE" things mpaka baadae mtoto anapokomaa. Binafsi niliruhusiwa kujifunza kila nilichoonekana napenda/naweza (kuimba, kupiga kinanda, kupika, kufuma, kushona, kuandika,michezo kidogo n.k) bila ya kuvipa hivyo vitu kipaumbele. Darasa lilitangulia ndo na hayo yakafuata. Sasa hivi nikiamua kujikita kwenye kuimba sijui kuandika siwezi angukia pua maana sikusukumizwa huko kwenye umaarafu ila niliruhusiwa kujiweka sawa ili nikomae.
Tatizo linatokea pale mzazi anapoamua kumtumia mtoto kama kitega uchumi hata pale ambapo mtoto anakua bado sana. Kwahiyo ni vizuri kugundua na kuendeleza vipaji vya watoto wangali wadogo ila sio kuvitumia wakati bado hawajakomaa vyakutosha.