Viongoziwa dini mmepatwa na nini?

Viongoziwa dini mmepatwa na nini?

Retired

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2016
Posts
53,047
Reaction score
104,575
Pamoja na kuwa na lengo lenye nia njema ya kumtendea haki Mbowe, sikubaliani na kauli ya kuwa Samia ampe Mbowe msamaha. Msamaha kwa kosa lipi? Inajulikana wazi kuwa Mbowe kabambikiwa kesi kwa sababu za kisiasa.

Sasa Samia ampe msamaha kwa angle ipi? Wangemwomba Samia afute kesi kwa sababu ni ya kubambikiwa. Najua si rahisi kuyasema hayo hadharani, Basi wangeyasema "in camera" na si kuja hadharani kuwa Samia amsamehe Mbowe.

Heshima yenu ni kubwa, yachunge Sana matamshi yenu na matendo yenu.

Amen.
 
Baada ya kuwa mtu mzima na mwenye timamu [above average] nikagundua kuwa si kila kiongozi ni akili kubwa, nimepuuza viongozi wengi mno wakiwemo hao wa dini, hapo kabla niliamini ni mabalozi wa Mungu hapa duniani.

Hii imenisaidia kwenye mambo mengi sana, punguza tu matarajio mkuu.
 
Pamoja na kuwa na lengo lenye Nia njema ya kumtendea haki Mbowe, sikubaliani na kauli ya kuwa Samia ampe Mbowe msamaha. Msamaha kwa kosa lipi? Inajulikana wazi kuwa Mbowe kabambikiwa kesi kwa sababu za kisiasa. Sasa Samia ampe msamaha kwa angle ipi? Wangemwomba Samia afute kesi kwa sababu Ni ya kubambikiwa. Najua si rahisi kuyasema hayo hadharani, Basi wangeyasema "in camera" na si kuja hadharani kuwa Samia amsamehe Mbowe.
Heshima yenu ni kubwa, yachunge Sana matamshi yenu na matendo yenu.
Amen.
Wamekosea sana. Kama kweli mbowe ni gaidi sasa asamehewe ili aje kulipua vituo vya mafuta na kuweka magogo barabarani? Ama kweli maajabu hayatakaa yaishe. Wiongozi wa dini hawapaswi kuwa wanafiki, wangempa makavu kwamba "Mbowe sio gaidi"
 
Nimejaribu kutafuta kwenye mtandao mkutano wote sijapata nakuta vipande vipande tu. Naomba mwenye "link" yote ya huo mkutano wa Mheshimiwa Raisi na viongozi wa dini ani pm jamani. Maana mikutano yote ikifanyika hata ikinipita nikienda tu "youtube " naikuta huko. Au ulikuwa mkutano wa ndani?
 
Wamekosea sana. Kama kweli mbowe ni gaidi sasa asamehewe ili aje kulipua vituo vya mafuta na kuweka magogo barabarani? Ama kweli maajabu hayatakaa yaishe. Wiongozi wa dini hawapaswi kuwa wanafiki, wangempa makavu kwamba "Mbowe sio gaidi"
Umemaliza kazi. Makavu kabisa kuwa Mbowe siyo gaidi
 
Wameongea kwa hekima na busara, ila ujumbe wao ndiyo huo huo kwamba kesi ni ya mchongo
Busara itendeke na ionekane imetendeka. Busara inawezekana imetendeka, LAKINI kwa kauli Yao waliyoitoa hadharani, Busara haijaonekana imetendeka
 
Hivi ulikuwa mkutano wa ndani au ulikuwa "live". Kama ulikuwa "live " naomba tena mwenye "link " anipatie.
 
Wameongea kwa hekima na busara, ila ujumbe wao ndiyo huo huo kwamba kesi ni ya mchongo
Sidhani kama kumwombea msamaha Mbowe na kumwomba Raisi afute kesi ya mchongo kama ni mambo yanayofanana.Busara ingekuwa labda kumwamia rais kuwa kesi haina maslahi kwa taifa,bali inaongeza chuki tu.
 
Pamoja na kuwa na lengo lenye Nia njema ya kumtendea haki Mbowe, sikubaliani na kauli ya kuwa Samia ampe Mbowe msamaha. Msamaha kwa kosa lipi? Inajulikana wazi kuwa Mbowe kabambikiwa kesi kwa sababu za kisiasa. Sasa Samia ampe msamaha kwa angle ipi? Wangemwomba Samia afute kesi kwa sababu Ni ya kubambikiwa. Najua si rahisi kuyasema hayo hadharani, Basi wangeyasema "in camera" na si kuja hadharani kuwa Samia amsamehe Mbowe.
Heshima yenu ni kubwa, yachunge Sana matamshi yenu na matendo yenu.
Amen.
Hao sio viongozi wa dini bali ni wajasiriamali wa dini
 
Busara itendeke na ionekane imetendeka. Busara inawezekana imetendeka, LAKINI kwa kauli Yao waliyoitoa hadharani, Busara haijaonekana imetendeka
Kipimo cha busara ni nini na ni nani anaye endorse? Kuna mkuu wa nchi yuko upande mmoja wa mazungumzo na wananchi ambao ni viongozi wa dini upande mwingine. Je busara ni kutoa lugha kali,tata, gombeshi,chongeshi na karipishi au lugha za kiungwana zenya kujenga? Viongozi wadini wana malengo mahususi, kupatanisha, kuleta maridhiano na kuponya. Malengo hayo hayawezi kufikiwa kama watafuata ushauri wako potofu.
 
Wewe utakuwa CCM, kwaheri! Enjoy your day!
 
Pamoja na kuwa na lengo lenye Nia njema ya kumtendea haki Mbowe, sikubaliani na kauli ya kuwa Samia ampe Mbowe msamaha. Msamaha kwa kosa lipi? Inajulikana wazi kuwa Mbowe kabambikiwa kesi kwa sababu za kisiasa. Sasa Samia ampe msamaha kwa angle ipi? Wangemwomba Samia afute kesi kwa sababu Ni ya kubambikiwa. Najua si rahisi kuyasema hayo hadharani, Basi wangeyasema "in camera" na si kuja hadharani kuwa Samia amsamehe Mbowe.
Heshima yenu ni kubwa, yachunge Sana matamshi yenu na matendo yenu.
Amen.
Duh
 
Back
Top Bottom