johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 96,225
- 168,794
Nilishangazwa na matukio mawili yaliyotokea karibuni, kwanza la Nape na pili la katibu mkuu Nishati.Wakati Rais ameshalizungumzia suala la Makonda pale ubungo sikuona sababu ya Waziri kuendelea tena na swala lile akijua wazi mamlaka ya juu imeshatoa msimamo.Lakini pia sikuona sababu ya KM Nishati kuongozana na Spika bandarini huku akijua wazi Rais ameshalitolea msimamo jambo hilo na Spika anaujua msimamo wa serikali.Spika alipaswa kuongozana na viongozi wa bandari ila kama ziara ya Rais ingekuwa haijafanyika ndipo umuhimu wa uwepo wa KM Nishati ungeonekana.So niwashauri tu viongozi wetu wawe wanazingatia protocal, Rais ni mamlaka ya juu kabisa ktk uongozi wa nchi.Ahsante na karibu tujadili