Ni busara sana kuomba kusamehewa pale ambapo umekosea. Watanzania kulalamikia upatikanaji hafifu wa maji safi kwenye mabomba na kukatika katika kwa umeme naona ni kosa kubwa na hatustahili kuiomba serikali iboreshe huduma hizi muhimu kwa jamii.
Malalamiko haya yamekuwa ni kelele kwenye masikio ya baadhi ya watu. Yatupasa kuwaomba hao watu msamaha kwa kuwapigia kelele.
Kwa upande mwingine, tunaomba mturehemu kwani sisi pia tunahitaji huduma hizo muhimu kuishi, kujitafutia kipato na hivyo kuyafanya maisha yetu kuwa ya furaha.
Najua mnaweza kutoa rehema hizi kwetu na tutawasujudia na kuwaimbia nyimbo za sifa.