Viongozi wengi wanaoteuliwa ni ''zao'' la UDSM, hizi siyo fikra potovu?

sirluta

JF-Expert Member
Nov 28, 2012
6,325
2,487
Kuna kaushahidi ka mbaali kuwa viongozi wengi wanaoteuliwa katika nafasi mbalimbali serikalini, walisoma ama wamefanya kazi katika Chuo Kikuu Cha Dar es salam (UDSM)!!!

Swali ni je, hadi leo vyuo vingine haviwezi kupatikana hao viongozi na badala yake kuchukuliwa UDSM pekee?

Navyohisi ni kwamba kuna maeneo mengine kuna watu wana sifa zaidi ya UDSM peke yake tu.
 
USICHOELEWA NINI WEWE. TANZANIA KUNA UDSM, SOKOINE NA MUHIMBILI UNIVERSITY TU. VINGINE NI BRANDING YA VYUO VIKUU AMBAVYO HAVINA VIWANGO. MZUMBE BADO NI INSTITUTE ILIYOPACHIKWA JINA LA UNIVERSITY LAKINI HAIJAFIKA KIWANGO CHA UNIVERSITY.
 
Kwasababu wenye position na nguvu za kuteua wengi walisoma UDSM , ila kiutendaji tunajua miaka 15 ijayo product za vyuo vyengine vitaonekana tu.
 
Sababu wako karibu na mjini....wako Dar...wako ikulu...a.k.a wana daresalamu...kwi kwi kwi...
Ila ukweli ni kwamba UD wanapenda sana siasa...na bila kuwa mwanasiasa kupata cheo ni kuokota embe chini ya mwarobaini...
Mzumbe wanapiga kimya kimya...ma RAS, wakurugenzi wa mawizara hasa HR wengi ni product za Mzumbe...wao wanachukua vyeo ambavyo ni professional...Unajua kuwa hata Balozi Sefue ni Product ya Mzumbe????
Ulishawai sikia Mzumbe wanagoma?...hawana siasa hao
Wao ni KAZI TU
 
Kuna kaushahidi ka mbaali kuwa viongozi wengi wanaoteuliwa katika nafasi mbalimbali serikalini, walisoma ama wamefanya kazi katika Chuo Kikuu Cha Dar es salam (UDSM)!!!

Swali ni je, hadi leo vyuo vingine haviwezi kupatikana hao viongozi na badala yake kuchukuliwa UDSM pekee?

Navyohisi ni kwamba kuna maeneo mengine kuna watu wana sifa zaidi ya UDSM peke yake tu.

Dunia nzima kuna vyuo vinavyojulikana kwa kuzalisha viongozi.Uliza vyuo vingine toka vianzishawe vimezalisha viongozi wa ndani na nje ya nchi wangapi ambao ni wakuu?

Chuo kikuu cha Dar es salaam kimezalisha maraisi sio wa Tanzania tu bali na nchi za nje kibao

pia angalia walimu.CHUO KIKUU cha Dar es salaam mwalimu ni wenye PHD na PROFFESSORS
Vyuo vingine wanavumiliwa tu.

Chuo kikuu kama cha Dar es salaam TUTORIAL ASSISTANT kazi yake wala si kufundisha ni kubeba na kufunga projector kwa ajili ya lecturer na proffessor kushusha nondo zao wakati vyuo vingine utakuta ni mwalimu anafundisha wanafunzi wa mwaka wa mwisho wa digrii.

Pass mark za kuingia CHUO KIKUU CHA Dar es salaam ni za juu kuliko chuo chochote.Ina maana ni chuo kama cha watu vipaji maalum

Hakuna chuo chenye maprofesa wengi na ma-Doctor wengi kama chuo kikuu cha Dar es salaam.Na wamewekwa waandae viongozi.Nenda vyuo vya HAVARD,OXFORD,YALE,MIT vyote kazi yao kuandaa viongozi tena wengine wa dunia nzima
 
USICHOELEWA NINI WEWE. TANZANIA KUNA UDSM, SOKOINE NA MUHIMBILI UNIVERSITY TU. VINGINE NI BRANDING YA VYUO VIKUU AMBAVYO HAVINA VIWANGO. MZUMBE BADO NI INSTITUTE ILIYOPACHIKWA JINA LA UNIVERSITY LAKINI HAIJAFIKA KIWANGO CHA UNIVERSITY.
Mimi nafikiri hicho Chuo ndicho kilichotufikisha hapa kwa ajili ya upigaji serikalini na Taasisi mbalimbali! Hivyo vingine kama SAUT, Mzumbe na vinginevyo ndivyo vyenye maadili!
 
Umeona eehhh. Mafisadi wote waulize wamesoma api???!!! te te te...nadhani nchi ijaribu kwingine ione matokeo
 
Kwa kifupi UDSM ipo pale kuandaa future leaders.sasa chuo kama Kampala jamani,nisiendelee tu.
 
Ukweli utabaki pale pale kuwa UDSM ndio chuo kikuu kwa Tanzania,hivyo vingine ni kwa ajili ya takwimu tu.Kwa maana ya idadi na ongezeko la vyuo.
 
Huu usawa mwingine mnaupigania siyo kabisa.. Hivi kweli kwa sasa hivi unawezaje kufananisha product za UDSM na vyuo vya juzi na vya machakani? Mfano tu jamani chuo kama CBE au TIA dakika 5 tu umetembea chuo kizima. Akati UDSM unaweza toka Yombo mpaka COET unakimbia kuwahi kipindi na bado unachelewa kama dakika 20. Acheni bwana
 
Ukweli utabaki pale pale kuwa UDSM ndio chuo kikuu kwa Tanzania,hivyo vingine ni kwa ajili ya takwimu tu.Kwa maana ya idadi na ongezeko la vyuo.
kejeli kama hizi hazifai. Kwahiyo hivo vingine ni vyoo au?
 
Mimi nafikiri hicho Chuo ndicho kilichotufikisha hapa kwa ajili ya upigaji serikalini na Taasisi mbalimbali! Hivyo vingine kama SAUT, Mzumbe na vinginevyo ndivyo vyenye maadili!
nakubaliana na wewe kabisa. Hata wale waliokuwa wanaongoza migomo na fujo ndo viongozi wetu leo ambao ndo mafisadi
 
Huu ni mtizamo hasi sana.Si dhani kama kuna nia ya makusudi ya kufanya hivyo.Remember one thing,University of Dar es Salaam imeanza siku nyingi kwa hiyo ina wahitimu wengi.Hii ina maana kwamba probability ya kuchagua kutoka kwenye sample ya UDSM ni kubwa zaidi kuliko kutoka kwenye samples zingine kama St.Augustine nk.kwa kuwa ni ndogo.I think it is as simple as that.Hakuna upendeleo wowote.
Kuna kaushahidi ka mbaali kuwa viongozi wengi wanaoteuliwa katika nafasi mbalimbali serikalini, walisoma ama wamefanya kazi katika Chuo Kikuu Cha Dar es salam (UDSM)!!!

Swali ni je, hadi leo vyuo vingine haviwezi kupatikana hao viongozi na badala yake kuchukuliwa UDSM pekee?

Navyohisi ni kwamba kuna maeneo mengine kuna watu wana sifa zaidi ya UDSM peke yake tu.
 
Watu hutoa mengi sana ukianza kuuliza chuo kikuu kizuri Tanzania. Lakini huwa najiuliza elimu ya chuo ulichosomea imebadili kwa kiasi gani maisha yako?? Naamini tunakwenda shule kwa ajili ya mambo matatu muhimu.
1.Kuondoa ujinga/kubadili mitizamo
2.Kuweza Kupambana na Mazingira yanotuzunguka(umaskini na maradhi)
3.Kuongeza Maarifa Zaidi
....kikubwa zaidi kubadili maisha yetu.....kwa maana ya kuwa na maisha mazuri zaidi......
Sasa kama Mtaendelea na perception kwamba UDSM is better than any other, Itakuja UDBS is better than CoET...Dhambi ileile itaendelea. Nawashauri kuachana na hii dhana ya which university is best kwa sababu tunajua what is going on in each university. So tujengane, hivi tunavyofanya tunawavunja Moyo wadogo zetu walipo huko ktk vyuo vingine. this is not fair.
 
Ni suala la muda tu, UDSM ilianza muda mrefu hivi vingine vimeanza hata miaka kumi bado havijafikisha, si rahisi kua na wahitimu ambao wamefanya kazi serikalini muda mrefu, chuo kingine ambacho kina viongozi serikalini hasa ktk sekta ya kilimo, misitu na ufugaji ni SUA. Naamini baada ya miaka 10 ijayo tutakua na mchanganyiko wa viongozi kutoka vyuo mbalimbali
 
Sababu wako karibu na mjini....wako Dar...wako ikulu...a.k.a wana daresalamu...kwi kwi kwi...
Ila ukweli ni kwamba UD wanapenda sana siasa...na bila kuwa mwanasiasa kupata cheo ni kuokota embe chini ya mwarobaini...
Mzumbe wanapiga kimya kimya...ma RAS, wakurugenzi wa mawizara hasa HR wengi ni product za Mzumbe...wao wanachukua vyeo ambavyo ni professional...Unajua kuwa hata Balozi Sefue ni Product ya Mzumbe????
Ulishawai sikia Mzumbe wanagoma?...hawana siasa hao
Wao ni KAZI TU
Hivi ule wimbo wa jipe moyo aliimba nani?
 
Dunia nzima kuna vyuo vinavyojulikana kwa kuzalisha viongozi.Uliza vyuo vingine toka vianzishawe vimezalisha viongozi wa ndani na nje ya nchi wangapi ambao ni wakuu?

Chuo kikuu cha Dar es salaam kimezalisha maraisi sio wa Tanzania tu bali na nchi za nje kibao

pia angalia walimu.CHUO KIKUU cha Dar es salaam mwalimu ni wenye PHD na PROFFESSORS
Vyuo vingine wanavumiliwa tu.

Chuo kikuu kama cha Dar es salaam TUTORIAL ASSISTANT kazi yake wala si kufundisha ni kubeba na kufunga projector kwa ajili ya lecturer na proffessor kushusha nondo zao wakati vyuo vingine utakuta ni mwalimu anafundisha wanafunzi wa mwaka wa mwisho wa digrii.

Pass mark za kuingia CHUO KIKUU CHA Dar es salaam ni za juu kuliko chuo chochote.Ina maana ni chuo kama cha watu vipaji maalum

Hakuna chuo chenye maprofesa wengi na ma-Doctor wengi kama chuo kikuu cha Dar es salaam.Na wamewekwa waandae viongozi.Nenda vyuo vya HAVARD,OXFORD,YALE,MIT vyote kazi yao kuandaa viongozi tena wengine wa dunia nzima[/QUO

Badala ya kutumi idadi ya PhDs na Professors, jaribu kutmuia uwiano kati ya wanafunzi na hao PhD/Professors. Harafu mazingira ya kusomea, kama maabara na madarasa. Weka uwiano wa maabara (ahasa vifaa kama darubini nk) na wanafunzi wanapsawa kutumia.

Kwa taarifa rahisi, UDSM ina walimu wasio na PhD wengi kuliko walio na PhD.
 
Back
Top Bottom