Viongozi wapya wa CCM vyuo vikuu lazima waonyeshe taswira mpya ya CCM mpya

DOFFA

JF-Expert Member
Jul 31, 2016
425
233
Hivi karibuni CCM vyuo vikuu ilifanya chaguzi zake na kupata viongozi wapya kabisa ambao pamoja na kazi iliyowapeleka vyuoni watafanya majukumu mengine ya chama ikiwa ni pamoja na kuitambulisha,na kuikuza kwenye shughuli za kijamii.

CCM ni vijana na Mh. Rais ameonyesha kwa vitendo kwa vijana kwa wengi wao kuchukuliwa kuwa watendaji ndani ya chama na serikali hivyo viongozi hao lazima wajitambue kuhusu hitaji la chama ili vijana wachukue hatamu ya chama.

Nimeanza na hili kuwakumbusha wasomaji na wadadisi wa mambo ya kisiasa kuwa CCM ni chama kongwe na chama dola kwa hiyo wale wote waliokuwa na mikakati ya kuidoofisha wamekwama na chama kinarudi kwenye ung'aro wake wa kijana inayotia moyo na matumaini.

CCM------------IMANI YAKE
a)
Binadamu wote ni sawa.
b)Kila mtu anastahili heshima ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake.
c)Ujamaa na kujitegemea ndiyo njia pekee ya kujenga jamii ya watu walio sawa na huru.
d)Kila mtu aliyekuwa mwanachama wa TANU au wa ASP mara kabla ya kuvunjwa kwa Vyama hivyo, na aliyekuwa anatimiza masharti ya
Uanachama wake, atakuwa mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi, isipokuwa kama atakataa mwenyewe.
e) Raia yeyote wa Tanzania mwenye umri usiopungua miaka 18, anaweza kuwa. Mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi iwapo anakubali Imani, Malengo na Madhumuni ya CCM.
f) Mtu atakayekubaliwa kuingia katika CCM, au kuendelea kuwa Mwanachama, ni yule anayetimiza Masharti yafuatayo:-

(1) Kuwa mtu anayeheshimu watu.
(2) Kuwa mtu anayefanya juhudi ya kuielewa, kuieleza, kuitetea na
kuitekeleza Itikadi na Siasa ya CCM.
(3) Kuwa mtu mwenye kuamini kuwa kazi ni kipimo cha Utu, na kuitekeleza imani hiyo kwa vitendo.
(4) Kuwa mtu anayependa kushirikiana na wenzake.
(5) Kuwa mtu ambaye siku zote yuko mstari wa mbele katika utekelezaji wa
mambo yote ya Umma, kulingana na Miongozo ya CCM.
(6) Kuwa wakati wote ni mfano wa tabia nzuri kwa vitendo vyake na kauli yake, kuwa mwaminifu na kutokuwa mlevi au mzururaji.
(7) Kuwa ama Mkulima, Mfanyakazi, au mwenye shughuli nyingine yoyo
yoyote halali ya kujitegemea.
9. Mtu atakayetaka kuwa Mwanachama atajaza fomu ya maombi na kuipeleka kwa Katibu wa Tawi anapoishi.
10. Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya CCM ya Tawi itafikiria na kutoa uamuzi wa mwisho kuhusu maombi ya Uanachama.
11. CCM itakuwa na Mpango wa kutoa Mafunzo kwa wanachama wake juu ya Imani, Malengo na Madhumuni ya Siasa ya CCM kwa jumla.

Wanachama
12.
(1) Mtu akikubali kuwa Mwanachama itabidi atekeleze haya yafuatayo:-
(a) Atatoa kiingilio cha Uanachama.
(b) Atalipa ada ya Uanachama kila mwezi isipokuwa kama akipenda anaweza kulipa ada ya mwaka mzima mara moja.
(c) Atatoa michango yoyote itakayoamuliwa.

(2)
Viwango vya kiingilio, ada na michango vitawekwa na Halmashauri Kuu ya Taifa.

13. (1) Uanachama wa mwanachama utakwisha kwa:-
(a) Kufariki.
(b) Kujiuzulu mwenyewe.
(c) Kuachishwa kwa mujibu wa Katiba.
(d) Kufukuzwa kwa mujibu wa Katiba.
(e) Kutotimiza masharti ya uanachama.
(f) Kujiunga na Chama kingine chochote cha siasa.

Katika muktada huu kiongozi lazima atimize wajibu wake kwa chama na kwa taifa lake,isiwe chama kama daraja la kupiga hela au kulinda rasilimali zako/ccm maslahi.
CCM NI CHAMA CHA KUTOA HUDUMA KWA JAMII.
 
CCM nakumbuka juzi tu mlisema siasa vyuoni ni mwiko.
kauli hii ilitolewa na Mtukufu Rais Magufuli akihutubia pale Udsm na pia makamanda wa polisi waliopinga mahafali ya chadema vyuoni walisema siasa vyuoni ni mwiko.
leo imekuaje tena??
Siasa siyo lazima kutoa hotuba majukwaani,siyo lazima ufanye siasa ukiwa ndani ya taasisi ya elimu japo hata hii lazima wanafunzi wa practice politics ndiyo kazi ya political science.
katazo ni malumbano yasiyo na tija ya vyama vya siasa!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
kauli ya Rais ilisema ni mwiko siasa vyuoni.
 
Siasa siyo lazima kutoa hotuba majukwaani,siyo lazima ufanye siasa ukiwa ndani ya taasisi ya elimu japo hata hii lazima wanafunzi wa practice politics ndiyo kazi ya political science.
katazo ni malumbano yasiyo na tija ya vyama vya siasa!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Maana ya katazo la siasa ni kuwa hakuna kuwa na tawi wala kijana kujipambanua yupo chama gani, kimya kimyaa kama una taka siasa. Sasa wewe kusema amepiga marufuku mikutano majjukwaani na malumbano unaonekana una uelewa mdogo sana, jiulize kwanza SIASA NI NINI NA MAANA YA NENO MARUFUKU.
 
Usikariri,funguka usijifunge ndani ya chupa!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom