Viongozi wapewe semina elekezi watambue umuhimu wa viapo vyao

malang0

JF-Expert Member
Apr 7, 2021
440
518
Kati ya matatizo tunayoyaona leo kwa wateule wanaopewa nafasi za uongozi nchini mwetu ni kushidwa kuelewa majukumu ya kazi zao mpya, maadili na nini maana ya viapo vyao kabla ya kuingia ofisini. Kiongozi yeyote anapoapa atambue hiyo nafasi si yake tena, bali hiyo ni nafasi ya Mwenyezi Mungu naye anafanya kazi chini ya mwongozo wake kuwatumikia wanadamu.

Hivyo basi, majukumu hayo si mepesi kama tunavyodhani bali wanatakiwa waombe hekima kuwatumikia watu kama mfalme Sulemani alivyomwomba Mungu. Nasema hivi kwa sababu makosa aliyofanyika miaka mitano ya Mwendazake yasijirudie tena, wapewe semina elekezi kama kipindi awamu ya nne ya Mh.Jakaya Kikwete.

Mambo ya kupiga watu, utekaji, uvamizi wa vyombo vya habari, kuminya haki za watu, kuendesha magenge ya uhalifu. kudhulumu haki za raia kuishi,kutukana watu, kuchapa viboko wafanyabiashara na wanafunzi siyo kazi zao hizo. Hatutaki kuona Marekani wanatutetea tena kuwa Tanzania ina viongozi wanaodhulumu haki za raia kuishi.
 
Back
Top Bottom