Viongozi waheshimuni Walimu la sivyo mtalaaniwa

Viongozi waheshimuni Walimu la sivyo mtalaaniwa

Mawematatu

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2021
Posts
468
Reaction score
608
Niende kwenye hoja moja kwa moja.

Kuna baadhi ya viongozi tena wa juu kabisa hawawapi heshima walimu na sababu ya wazi kwao kuwatendea uhalifu tena wakiwa nao ni walimu ni madaraka. Siku zote madaraka ni upofu.

Madaraka yamekuwa yakiwatoa ufahamu viongozi wa juu mawizarani na kuwaona watumishi Hawa wa Mungu kama dekio, kwa wanajua dekio wataelewa.

Mh. Rais na Mh wazuri Mkuu.

Waraka huu mfupi usaidie kufumbua jicho la tatu wamulikwe ni wanyanyasaji, waoneaji, wababe, miungu watu, wafalme na wengine kufanya mambo ya hovyo kabisa huko waliko. Hawa ni watumishi walioaminiwa cha kushangaza wanakosa hekma na busara za utu na kibinadamu.

Walimu ni watu wa kuwaheshimu tutake tusitake, Kwa Mola Mwenyezi, walimu wamesaidia watu wengi wanaojipatia riziki huko walipo.

Kama kiongozi ukishindwa kutambua hilo utaambulia laana. Ni lazima waheshimiwe.
 
Waongeze salary, madaraja,ela za likizo hatulipwi miaka adi 3,muundo haubadiliki,ukipata muundo Basi unatumikia miaka 3 bila nyongeza ya mshahara?
 
Back
Top Bottom