Kamende
JF-Expert Member
- Mar 1, 2008
- 416
- 45
Habari zilizofika mezani hivi punde kutoka kule Moshi zinasema kuwa viongozi wa ngazi za juu serikalini hasa Mawaziri bila kujali wizara zao wamekuwa wakitembelea Chuo Cha Polisi cha mjini Moshi kuongea na wanafunzi wanaochukua mafunzo ya upolisi mambo nyeti.
Katika mambo wanayoshawishiwa kuyajua askari hao wanafunzi ni umuhimu wa kukilinda Chama Cha Mapinduzi na kuhakikisha kuwa wanawatumika kuvibana vyama vya upinzani ili CCM iweze kushinda chaguzi zinazikuja.
Waziri mmoja aliyekuwa Moshi mapema mwezi huu wa Januari aliwaasa askari hao wanafunzi kuwa wasifanane na hawa askari wa zamani ambao wamebadilika fikra zao zikawa za kiraia. (Maana alifafananua kuwa wapo askari wanaovujisha siri kwa vyama vya upinzani na pia wanaokataa kabisa kuisaidia CCM kushinda chaguzi zinazoikabili. Mfano aliotoa ni uchaguzi mdogo wa Tarime).
Zawadi ambayo askari hao wanafunzi wamehakikishiwa ni kupewa cheti cha askari wa kimataifa. "Hao wenzenu waliowatangulia wana vyeti vya hapa hapa nchini. Nyinyi tutawapa vyeti vya kimataifa"
Depo yote ya sasa na pengine mbili zijazo zitaingizwa FFU kwa lengo hilo hilo la kuimarisha mashambulizi dhidi ya wapinzani.
Jamani bado viongozi wetu hawajafumbuka macho waone kile watanzania wanachoona. Hawataki kuongoza kwa kupendwa. Wanataka kuendelea kutumia nguvu. Hakika ya Zimbabwe yanainyemelea Tanzania.