Bome-e
JF-Expert Member
- Jan 3, 2014
- 17,104
- 26,070
Wanabodi,mambo ambayo yametokea katika awamu ya 5 yamenifanya nione umhumi wa kutenganisha kofia hizi mbili ili kuleta matokeo chanya zaidi katika utawala bora usiohodhisha madaraka kwa mtu mmoja!
Chama cha siasa kilichotoa Rais kinapaswa kufanya tathimini ya utekelezaji wa sera na ilani yake unaofanywa na serikali!
Sasa kwenye vikao hivyo unakuta wale wale viongozi wa serikali ndio wanakuwa viomgozi wa chama,hapo ndio unajiuliza nani anafuatilia utendaji wa mwenzake!Yaani kwa lugha nyepesi ni kama unajifanyia tathimini mwenyewe na hapo ndio kunaibuka mgongano wa maslahi!
Nitoe mifano michache,
-2015 kikosi kazi na think tank ya CCM ilikaa na kuja na ilani!Katika mambo ambayo walijadili kama chama na kuyaweka katika ilani ni pamoja na kipengele kinachoeleza kuwa watawapa fursa ya kuendelea na masomo watoto wote ambao watapata ujauzito mara baada ya kujifungua!Vichwa makini ndani ya CCM viliona jambo hilo ni muhimu,Rais akazunguka kuinadi ilani hiyo nchi nzima!
Alipochaguliwa moja kwa moja akabadili muelekeo na kusema kwenye utawala wake marufuku mtoto atakayepata mimba/kujifungua kurudi katika mfumo rasmi !Katika hilo nilitegemea CCM iisimamie serikali kutekeleza ilani waliyokubaliana,ndio hapo unakuta Mwenyekiti ni huyo huyo ambaye ametenda kinyume na ilani ya chama!Hapo tunaona kuwa kofia hizi mbili zikivaliwa na mtu mmoja,dhana nzima ya chama kusimamia serikali katika utekelezaji wa ilani inakwama!
Tunachoona hapa ni viongozi wengine,wajumbe wa NEC na kamati kuu kunywea maana Boss ni yule yule pande zote,serikalini na chamani!
-Pia tumeona kauli zisizo nzuri zikitolewa na mkuu wa nchi mara watz wanapokutwa na Majanga,lakini hakuna wa kumwambia kutoka kwenye chama kuwa unakosea maana yeye mwenyewe ndiye mwenyekiti!
-Tumeona namna ambavyo tofauti zake na viongozi wastaafu amelazimisha chama kizibebe!Hajaridhishwa na maongezi yalivyofanyika dhidi ya Membe,kinana na Makamba hivyo ameamua kuiamuru kamati ya maadili kufikisha report ili ajiridhishe na kilichotokea,ameona kama kamati ilikuwa soft kwa wahojiwa!Hapa tunaona mgongano wa maslahi kwenye kofia hizi mbili!
-Tunaona Rais anavyoagiza wizara ya ardhi irudishe ardhi kwa halmashauri,lakini anawashauri halmashauri wajenge hata ofisi ya chama wakirejeshewa ardhi hiyo!Sasa hapo ndio unaona anashindwa kujua kuwa sio kazi ya halmashauri kujenga ofisi za chama chochote cha siasa!
-Kofia hizo mbili zimewafanya wanaccm wengi kuwa ndio mzee,maana hawana namna kwani wanaona kwa vitendo kuwa siyo afya kuwa na mawazo tofauti na Mwenyekiti ambaye ndiye Rais!
Niishie hapo!