Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,458
- 5,134
Viongozi wa Umoja wa Ulaya leo wanakutana mjini Brussels katika mkutano wao wa mwisho wa kilele kwa mwaka huu, ambapo ajenda zitakazotawala katika mkutano huo wa siku mbili zikiwa ni kuhusu vita dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi na bajeti ijayo ya muda mrefu ya umoja huo.
Kwa mara ya pili mwaka huu, viongozi hao wanatakiwa kujizatiti kupunguza gesi chafu ya kaboni ifikapo mwaka 2050. Poland, Hungary na Jamhuri ya Czech zinalipinga lengo hilo ambalo linajumuisha upunguzaji wa matumizi wa gesi chafu ya kaboni.
Rais mpya wa Baraza la Ulaya, Charles Michel na Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya, Ursula von der Leyen, wanashinikiza ajenda ya mabadiliko ya tabia nchi.
Mada nyingine ya mkutano huo ni vikwazo vya Urusi kutokana na kuivamia Ukraine, mkataba wa mipaka baharini uliofikiwa na Uturuki na Libya na majadiliano ya Brexit.