Viongozi wa dini, wawaunga mkono UKAWA

rosemarie

JF-Expert Member
Mar 22, 2011
6,841
2,000
Viongozi wa dini nchini, wamesema kuwa watasimama kidete kuhakikisha wanaunga mkono umoja wa katiba ya wananchi (ukawa) kwa ajili ya kuhakikisha inapatikana katiba mpya.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Mbinga mkoani Ruvuma, Mwenyekiti wa taasisi za dini za Kiislaamu nchini, Rajab Katimba, amesema viongozi wa dini kwa pamoja wamewapa baraka viongozi wa UKAWA, ili kuhakikisha inapatikana katiba ya muundo wa serikali tatu, kama wananchi walivyopendekeza, katika rasimu iliyowasilishwa bungeni na Tume ya Jaji Joseph Warioba.
10301513_709983802373452_5506094571147617657_n.jpg
 
Sideeq

JF-Expert Member
Dec 12, 2009
2,422
0
Haswaa!siyo yule shehena Jongo laana tullah
Yule amepotoka hivyo mpe nasaha, atakapozielewa na kuzikataa hapo ndipo hukmu yake itakapopita kama ni kulaaniwa au kukufurishwa.

Ila kumlaani kabla ya kumpa nasaha basi nakunasihi usifanye hivyo maana yake Kiislamu utakuwa humtendei haki.
 
OSOKONI

JF-Expert Member
Oct 20, 2011
10,977
2,000
Na sisi wananchi wa kawaida tuwaunge mkono UKAWA kwani wanatetea maoni yetu yajadiliwe kutengeneza katiba mpya sio maoni ya mkoloni mweusi(ccm)
 
Buchanan

JF-Expert Member
May 19, 2009
13,202
2,000
Na sisi wananchi wa kawaida tuwaunge mkono UKAWA kwani wanatetea maoni yetu yajadiliwe kutengeneza katiba mpya sio maoni ya mkoloni mweusi(ccm)

Tueleze mkuu,
Hivi UKAWA ni NGO, SACCOS, au kitu gani? Sio unadai tu tuwaunge mkono kitu tusichokifahamu!
 
Buchanan

JF-Expert Member
May 19, 2009
13,202
2,000
Viongozi wa dini nchini, wamesema kuwa watasimama kidete kuhakikisha wanaunga mkono umoja wa katiba ya wananchi (ukawa) kwa ajili ya kuhakikisha inapatikana katiba mpya.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Mbinga mkoani Ruvuma, Mwenyekiti wa taasisi za dini za Kiislaamu nchini, Rajab Katimba, amesema viongozi wa dini kwa pamoja wamewapa baraka viongozi wa UKAWA, ili kuhakikisha inapatikana katiba ya muundo wa serikali tatu, kama wananchi walivyopendekeza, katika rasimu iliyowasilishwa bungeni na Tume ya Jaji Joseph Warioba.
View attachment 159978

Kwa hiyo huyo Rajab Katimba ndio "Viongozi wa Dini?"
 
BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
102,694
2,000
Uelewa wako ni finyu sana ndio maana hufahamu UKAWA ni kitu gani. Kwa wale tunaoelewa UKAWA ni kitu gani na madhumuni yao wala hatuoni tatizo kuwaunga mkono.

Tueleze mkuu,
Hivi UKAWA ni NGO, SACCOS, au kitu gani? Sio unadai tu tuwaunge mkono kitu tusichokifahamu!
 
Getstart

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
6,660
2,000
Viongozi wa Dini wanaojitambua kama Sheikh Rajabu Katimba ni mfano wa kuigwa na wananchi wote.
Kwa hiyo ngoja draw. Jana kulikuwa na taarifa kuwa CCM wanafanya kampung misikitini kuungwa Serikali mbili na Leo tuna pasta taarifa kuwa UKAWA wanaungwa kmkono na viongozi wa dini Serikali tatu!
 
samaki2011

JF-Expert Member
Dec 17, 2013
1,776
0
Tueleze mkuu,
Hivi UKAWA ni NGO, SACCOS, au kitu gani? Sio unadai tu tuwaunge mkono kitu tusichokifahamu!

Kawaulize viongozi wako wa chama chenu cha mafisadi wanawafahamu sana UKAWA maana sasa hivi hawapati usingizi tena mpaka kifo kitakapowakuta
 
Buchanan

JF-Expert Member
May 19, 2009
13,202
2,000
Uelewa wako ni finyu sana ndio maana hufahamu UKAWA ni kitu gani. Kwa wale tunaoelewa UKAWA ni kitu gani na madhumuni yao wala hatuoni tatizo kuwaunga mkono.

Okay, mwenye "uelewa mpana" tueleze hii kitu iitwayo "UKAWA" ni SACCOS, NGO, VICOBA au ni nini?
 
Buchanan

JF-Expert Member
May 19, 2009
13,202
2,000
Kawaulize viongozi wako wa chama chenu cha mafisadi wanawafahamu sana UKAWA maana sasa hivi hawapati usingizi tena mpaka kifo kitakapowakuta

Spika Makinda alipiga marufuku neno "UKAWA" kutumika Bungeni kwa kuwa halijulikani maana yake!
 
BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
102,694
2,000
Reputation yako hapa ilikuwa kubwa sana, usiendelee kuiharibu zaidi ya ilivyokwishaharibika.
Have a great weekend :):)

Okay, mwenye "uelewa mpana" tueleze hii kitu iitwayo "UKAWA" ni SACCOS, NGO, VICOBA au ni nini?
 
msumeno

JF-Expert Member
Aug 3, 2009
2,833
2,000
Serekari tatu hazikwepeki ila urais baado kabisa ..... Kale ka harufu bado kananuka
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom