Viongozi wa dini wana haki ya kukemea kosa la viongozi wa serikali ?

BAOBAO

BAOBAO

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2012
Messages
1,789
Points
1,250
BAOBAO

BAOBAO

JF-Expert Member
Joined Oct 12, 2012
1,789 1,250

  1. [*=1]Wakuu,mimi naona ni haki yao viongozi wa dini kuwakemea viongozi wa serikali katika ngazi yeyote ile.Pale,Viongozi wa dini wanapoacha au kushindwa kusimamia viongozi wa serikali;tangu katika mimbari za miskiti au madhabahu za makanisa wanayoongoza kwa kushindwa kukemea dhambi au makosa ya viongozi wa serikali;kumeleta mmomonyoko wa maadili kwa baadhi yao.Na viongozi wa serikali wakikosa watu wa kuwaonya na kuwakemea;wanaweza kutenda yasio haki na kuleta machukizo kwa jamii[MITHALI 16;12]. Lawama zangu ni kwa viongozi wa dini kabla ya viongozi wa serikali. Mtawala yeyote anaweza kutenda dhambi au kosa pasipo kukusudia jambo ambalo Mungu amezuilia,kwani si ajabu kama tujuavyo sote [MAMBO YA WALAWI 4:22,26;5:17].Nabii Nathani alimwambia wazi mtawala wa nchi kuwa ametenda dhambi ya kuua kwa siri,Mume wa mtu na kumchukua mkewe na kuzaa naye mtoto.[2 SAMWELI 12:1-15].Mfalme alikiri na kutubu dhambi yake;na kuwapa mfano viongozi wetu wa kukubali kukumewa na watumishi wa Mungu. 3.Na Yesu Kristo aliomba msamaha kwa kosa ambalo alifanya msaidizi wake Simon Petro;la kumkata mtu sikio {LUKA 22:49-51}Je,si vema viongozi wa dini nao kuiga mfano wa Yesu;kuomba msamaha kwa makosa ya waumini wao waliofanya kwenye jamii?Je,leo kuna viongozi wa dini nchini waliojaa ujasiri kukemea uovu bila kujali chanzo cha kosa kama nabii Nathani na wengine huko duniani ?Nawakilisha.
 
Mwanahisa

Mwanahisa

JF-Expert Member
Joined
Jun 29, 2012
Messages
1,395
Points
1,195
Mwanahisa

Mwanahisa

JF-Expert Member
Joined Jun 29, 2012
1,395 1,195
Mkuu, BAOBAO
Kuna ujumbe hapa nauona ila ww umekataa kuuweka wazi kwa sababu ulizo nazo.
Ni vizuri kuomba msamaha kwa niaba ya mtu, pia ni vizuri kukemea na kuonya pale tunapoona hapakwenda sawa, ila jukumu la kuonya au kukemea linabebwa na usafi wa huyo anaenyoosha kidole kwa mwenzie. Kama sio msafi yatakua yaleyale ya ALIYE MSAFI KATI YENU NA AWE wAKWANZA KUMPIGA MAWE MWANAMKE HUYU KAHABA. Hata viongozi wa Dini zetu hawataweza kukemea pale usafi wao utakapotiliwa mashaka.
 
BAOBAO

BAOBAO

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2012
Messages
1,789
Points
1,250
BAOBAO

BAOBAO

JF-Expert Member
Joined Oct 12, 2012
1,789 1,250
Mkuu, BAOBAO
Kuna ujumbe hapa nauona ila ww umekataa kuuweka wazi kwa sababu ulizo nazo.
Ni vizuri kuomba msamaha kwa niaba ya mtu, pia ni vizuri kukemea na kuonya pale tunapoona hapakwenda sawa, ila jukumu la kuonya au kukemea linabebwa na usafi wa huyo anaenyoosha kidole kwa mwenzie. Kama sio msafi yatakua yaleyale ya ALIYE MSAFI KATI YENU NA AWE wAKWANZA KUMPIGA MAWE MWANAMKE HUYU KAHABA. Hata viongozi wa Dini zetu hawataweza kukemea pale usafi wao utakapotiliwa mashaka.
Ni kweli kabisa,Mwanahisa.Kama kiongozi wa dini ana boriti machoni pake;hawezi kumwambia; kiongozi wa serikali aondoe kibanzi;kwa kuogopa kukemea ili nao wasijekemewa ! Uenda tatizo ni kubwa zaidi la maadili,kwa viongozi wa dini kuliko viongozi wa serikali ambao ni waumini wao.
 
M

mwembemdogo

JF-Expert Member
Joined
Feb 28, 2016
Messages
2,288
Points
2,000
M

mwembemdogo

JF-Expert Member
Joined Feb 28, 2016
2,288 2,000
Ahaaaa mie napita tu viongozi wa dini wa kwetu sidhani kama wanaweza kwani wao hawaoni makosa ya serikali
 
H1N1

H1N1

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2009
Messages
4,205
Points
2,000
H1N1

H1N1

JF-Expert Member
Joined May 29, 2009
4,205 2,000
Naona kama baraza la Maaskofu Katoliki huwa linajitahidi kukemea viongoxi wa serikali wasio WAKATOLIKI kwa kuwa huyu MKATOLIKI hagusiki kabisaa
Udini unaweza kuwa ni kweli kwa kuangalia namna na ukimya wa TEC katika matamko wazi na ya hatali yatolewayo na viongoxi
 
BAOBAO

BAOBAO

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2012
Messages
1,789
Points
1,250
BAOBAO

BAOBAO

JF-Expert Member
Joined Oct 12, 2012
1,789 1,250
Naona kama baraza la Maaskofu Katoliki huwa linajitahidi kukemea viongoxi wa serikali wasio WAKATOLIKI kwa kuwa huyu MKATOLIKI hagusiki kabisaa
Udini unaweza kuwa ni kweli kwa kuangalia namna na ukimya wa TEC katika matamko wazi na ya hatali yatolewayo na viongoxi
Ulikuwa hajui katoliki ni serikali ya kimataifa ? Balozi kila nchi!
 
SAUTI YAKO

SAUTI YAKO

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2014
Messages
2,364
Points
2,000
SAUTI YAKO

SAUTI YAKO

JF-Expert Member
Joined Jan 25, 2014
2,364 2,000
Nimemsikia mzee Wa upako Leo pale channel ten ameongea Kwa kuzunguka lakin nimemuelewa amesisitiza sana Amani ..nadhani wiki hii masheikh na viongoz Wa dini zengine watumie wiki hii kuwausia ukuta na wenye mamlaka kuafikiana mezan kuliko kuja kupambana hiyo trh moja
 
Forum statistics

Threads 1,283,763
Members 493,810
Posts 30,800,063
Top