Viongozi wa dini wamtetea Dk Slaa. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Viongozi wa dini wamtetea Dk Slaa.

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Ujengelele, Oct 3, 2010.

 1. U

  Ujengelele JF-Expert Member

  #1
  Oct 3, 2010
  Joined: Jan 14, 2008
  Messages: 1,256
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Viongozi wa dini wamtetea Dk Slaa.


  [​IMG]Thursday, 30 September 2010 04:10
  *Askofu Ruzoka ashauri zijadiliwe hoja si maisha binafsi
  *Askofu Laizer: Tukitazama maisha binafsi hakuna atakayepona

  ?Na Reuben Kagaruki

  VIONGOZI wa dini nchini wamekosoa tabia ya watu kujadili maisha binafsi ya wagombea kama kigezo cha uongozi bora katika uchaguzi mkuu, kuwa hiyo sio ya sahihi kwa kuwa kinachotakiwa kusikilizwa ni hoja za wagombea na kitu gani wataifanyia nchi.

  Kauli hiyo ilitolewa Dar es Salaam jana na Taasisi ya Juhudi za Viongozi wa Dini ya Kutafuta Haki na Amani nchini, inayoundwa na Baraza la Waislamu Tanzania (BAKWATA), Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) na Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC).

  Wakizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana viongozi wa taasisi hiyo walisisitiza kuwa endapo kila mwananchi ataandamwa kwa masuala binafsi, hakuna atakayebaki salama.

  Viongozi hao walitoa kauli hiyo wakati wakijibu maswali ya waandishi wa habari mara baada ya kumaliza mazungumzo yao viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) jijini Dar es Salaam. Mazungumzo hayo ambayo vyombo vya habari havikushiriki yalihusisha viongozi 12 wa dini .

  Mwenyekiti wa taasisi hiyo, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Tabora, Paul Ruzoka alisema kinachotafutwa ni hoja za wagombea kuhusu kile watakachoifanyia nchi.

  Hoja ya Askofu Ruzoka iliungwa mkono na Askofu Thomas Laizer wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) kutoka CCT

  Askofu Laizer alihoji; "Kila mmoja akiandamwa kwa masuala binafsi nani atabaki salama? Kinachotafutwa ni sera na sio masuala binafsi."

  Aliongeza kusema kuwa; "Na ninyi waandishi wa habari kila mmoja akiandamwa kwa masuala binafsi hakuna atakayebaki salama."

  Pamoja na kwamba hawakumtaja jina kiongozi anayehusika, kwa nyakati tofauti mgombea urais kwa tiketi ya CHADEMA, Dkt. Willibrod Slaa amekuwa akishambuliwa na wanasiasa kuwa hafai kuwa kiongozi kwa madai kuwa ametangaza uchumba na Bi. Josephine Mushumbusi ambaye ni mke wa mtu.

  Kutokana na tuhuma hizo, anayejitangaza kuwa mume wa Josephine, Bw. Aminiel Mahimbo alijitokeza na kufungua kesi ya madai mahakamani, lakini Dkt. Slaa amesema watakutana huko huko, huku akihoji, 'huyo mwanamume alipoibiwa mke alikuwa wapi?'

  Viongozi hao wa dini walipoulizwa wana maoni gani kuhusu kauli ambazo zinaweza kuwapa hofu Watanzania kuhusu utabiri unaotolewa kwamba kuna mgombea urais atafariki hivi karibuni, Askofu Ruzoka alijibu;

  "Muda wowote watu wanafariki hata wakati wa uchaguzi wanakufa...kwa bahati hatujui tarehe ya kufa," alisema bila kufafanua zaidi.

  Mara kwa mara, Mnadhimu wa nyota nchini, Shekhe Yahya Hussein amekuwa akisema kuwa utabiri wake wa kinyota unaonesha kuwa kuna mgombea urais atafariki.

  Akizungumzia sababu ya viongozi hao kwenda kuzungumza na viongozi wa CHADEMA, Askofu Ruzoka alisema lengo lao ni kuzunguka katika vyama mbalimbali na kuzungumza na wagombea wote ili kuwasihi waendeshe shughuli zao za kugombea uongozi kwa misingi ya haki, mshikamano na amani.

  "Tunafanya hivyo muda wote tunatembelea kila chama ili ujumbe wetu ufike," alisema.

  Kwa upande wake Dkt. Slaa alisema wamefarijika kwa viongozi hao kuona jukumu la kutembelea vyama vya siasa na alitumia nafasi hiyo kumshitaki mgombea urais wa CCM, Rais Jakaya Kikwete kwa kile alichodai anavunja kanuni na maadili ya uchaguzi.

  Alisema waliwaaambia viongozi hao kuwa Rais Kikwete licha ya kuwa mlinzi wa kusimamia maadili na taratibu zote za uchaguzi, anakiuka taratibu kwa kufanya mikutano yake ya kampeni hadi saa moja usiku.

  "Tumewaambia (viongozi wa dini) kuwa ndani ya vyama vya siasa hatulingani, kuna chama tawala kinavunja taratibu, sheria na kanuni," alisema Dkt. Slaa na kuongeza; "Haki isipotendeka sio rahisi sisi kukaa kimya."

  Alisema mara nyingi vurugu katika uchaguzi zinatokana na matokeo kutokuwa ya haki. "Viongozi wa dini wametuambia tuwe tayari kukubali matokeo...lakini na wao ni lazima wachukue hatua za kuhakikisha taratibu za haki zinafuatwa," alisema.

  Dkt. Slaa alisema aliwaambia viongozi wa dini kuwa kuna waraka wa serikali umesambazwa wa kuwatishia wakurugenzi nchi nzima unaoelekeza kuhakikisha CCM inashinda. "Hii ni dhahiri matokeo yatakuwa yamepangwa," alisisitiza Dkt. Slaa.

  Mbali na kusambazwa kwa waraka huo, Dkt. Slaa alisema imetumwa tume ya kwenda kuonana na viongozi wa dini na wengine wanatishwa.

  Kwa upande wake Mwenyekiti wa CHADEMA, Bw. Freeman Mbowe alisema vikundi vya CCM maarufu kama Green Gurd vinafundishwa mafunzo ya kijeshi huku Jeshi la Polisi likiwa halichukui hatua zozote.

  "Vyama vya siasa sio vyombo vya kijeshi...Green Gurd wanaachwa wanavunja sheria wakati wa uchaguzi, itafikia hatua uvumilivu utashindikana," alisema na kusisitiza kuwa Green Gurd watakuwa chanzo cha kuchafua uchaguzi wa mwaka huu.
   
 2. M

  Magobe T JF-Expert Member

  #2
  Oct 3, 2010
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 357
  Trophy Points: 180
  Kama kuwa kiongozi Tanzania ni lazima kuchunguza hali ya ndoa (maisha binafsi ya mtu) basi tufanye hivyo kwa wagombea wote na siyo kumlenga mtu mmoja tu kwani kuna minong'ono huku mitaani kuhusu wagombea wengine pia. Kwa bahati mbaya, ni rahisi kujadili maisha ya ndoa ya baadhi na kuogopa ya wengine. Hapa ndipo linapokuja tatizo. Kama kuna tija tufanye hivyo kwa wote na kama wengine tunawaogopa basi tusifanye kwe yeyote, otherwise tunakuwa hatutendi haki kabisa! Nami naunga mkono ushauri wa viongozi wa dini. Kama ni kuchokonoa, tuchokonoe viongozi wote!
   
 3. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #3
  Oct 3, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,895
  Likes Received: 416,603
  Trophy Points: 280
  Dr. Slaa aondoe wasiwasi kwani kwenye maandiko matakatifu imeeandikwa:-


  Matakwa ya Mwenyezi Mungu ni shubiri ya wale wote ambao wanamkaidi kwa fikra na matendo yao!

  Ukisoma

   
Loading...