Viongozi wa dini wamnusuru mfanyabiashara kuuawa............... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Viongozi wa dini wamnusuru mfanyabiashara kuuawa...............

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Rutashubanyuma, Jan 17, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Jan 17, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,233
  Trophy Points: 280
  Viongozi wa dini wamnusuru mfanyabiashara


  Na Gladness Mboma

  SERIKALI wilayani Mbarali imewapongeza baadhi ya viongozi wa dini kwa kuzima jaribio la kutaka kuuawa kwa mwekezaji wa shamba la Mpunga lililopo Ubaruku, Bw. Abrahakh Phil Mohamed kwa madai ya kutumia jina la
  Rais Jakaya Kikwete kuwanyanyasa wananchi na kuwaita mbwa.

  Akizungumza na Majira kwa njia ya simu, Mkuu wa Wilaya ya Mbarali, Kanali Cosmas Kayombo alisema kuwa viongozi hao wa dini wakiongozwa na Mchungaji wa Kanisa la Pentecostal Evangelical Church (PEC), Bw. William Mwamalanga walizungumza na wazee na kuzima jaribio hilo.

  Kanali Kayombo alisema kuwa wananchi hao walikuwa wakishinikiza kupatiwa eneo la shamba ambalo wanadai mwekezaji huyo alilichukua kinyume cha sheria, ikiwa ni pamoja na kumkataa.

  "Hata hivyo, Kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa imekaa na viongozi wa vitongoji na vijiji vyenye mgogoro kuona ni nini kifanyike, ambapo walidai kutaka kurudishiwa eneo lao lililomegwa, ikiwa ni pamoja na kutaka mwekezaji huyo kuwapatia maji," alisema.

  Alisema kuwa mwekezaji huyo amekubalina na ombi la wananchi, na amewaachia eneo la shamba ambalo wanalihitaji na kuwapatia maji kwa ajili ya kumwagilia katika mashamba yao.

  Kanali Kayombo alisema kuwa pamoja na wananchi hao kumkataa mwekezaji huyo, katika vurugu hizo walichoma gari la mafuta na kituo cha mafuta cha Igurusi, mali ya Bw. Munus Mohamed.

  Naye Mchungaji Mwamalanga alisema kwamba katika vurugu hizo iliwachukua saa tisa kuwatuliza wananchi hao, akishirikiana na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Bw. Advocate Nyombi.

  Alisema kuwa wananchi hao walichukizwa na kauli ya mwekezaji huyo kuwaeleza kwamba yeye hawezi kuzungumza na mbwa bali anazungumza na mfugaji, ambaye ni Rais Kikwete.

  "Kitendo cha mwekezaji huyu kuwatukana wananchi, ndicho kilichochochea hasira zao na kuamua kufanya vurugu, ambapo walichoma gari na kisima cha mafuta cha ndugu yake na mwekezaji huyo," alisema

  Alisema kuwa kama siyo Kamanda wa Polisi Advocate Nyombi kuwa na busara na kuwatuliza wananchi, mwekezaji huyo angekuwa amechinjwa kutokana na vijana 17 ambao walikuwa wameandaliwa maalumu kwa ajili hiyo.

  Mchungaji Mwamalanga alisema kuwa pamoja na kutulizwa, ikiwa ni pamoja na mwekezaji huyo kuahidi kuwarudishia mashamba pamoja na maji, wananchi bado wamemtaka kuondoka katika shamba hilo kwa kuwa amewatukana wao pamoja na rais.

  "Huyu mwekezaji ametakiwa kuomba msamaha wananchi na pia ametakiwa kumuomba radhi rais kwa kitendo chake cha kuwaita mbwa, pamoja na kutubu," alisema.Naye Kamanda Nyombi alisema kuwa amesikia kwamba wananchi hao wametoa siku tatu kwa mwekezaji huyo kuondoka licha ya kuwatuliza ma kuwasihi wasifanye vurugu zozote juzi.

  "Ndugu Mwandishi hivi ninavyozungumza na wewe niko njiani naelekea Mbarali baada ya kusikia kwamba wananchi wametoa siku tatu kwa mwekezaji huyo kuondoka, tumefanya juhudi kubwa sana kuhakikisha kwamba tunazima vurugu hizo ambazo zilikuwa ni za kumwaga damu," alisema.

  [​IMG]


  1 Maoni:

  [​IMG]
  Anonymous said... Viongozi wetu wanajichafua kwa ufisadi kwani wanapopewa pesa na wawekezaji uchwara kama hao wa kiarabu huwatolea siri kuwa nao ni wabia kwa maneno machafu kama hayo ya wananchi kuitwa mbwa na kwamba wanaongea na mwenye mbwa, nchi yetu inakwenda wapi, mzee wetu Nyerere angetoa masaa 48 ya huyo mwarabu kuondoka nchini.
  January 16, 2011 10:02 PM
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Jan 17, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,233
  Trophy Points: 280
  Asichojua huyu mfanyabiashara ni kuwa kama sisi ni mbwa hata hizo nguzo zake hapo ikulu nazo na mbwa tu..................kama yeye.........................vinginevyo asingelikuja kuhenyea huku kwetu....................angelibaki kwao ambako hakuna mbwa......................
   
 3. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #3
  Jan 17, 2011
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Safi sana wananchi wa Mbarali, kazeni kamba hivohivo msikubali ukoloni huu mpya chini ya Gavana wao Kikwete.
   
 4. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #4
  Jan 17, 2011
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Kule Mbarali kuna Wapakistani toka eneo la Baruch land Pakstan, ni wazamiaji wa miaka mingi, si watu wazuri sana japo wapo wasio na noma.KWa miaka mingi wametumia rangi yao kupata Lion Share. Nadhani hata huyu mwekezaji ni kutoka huko Pakistan.
  Sisi wenyeji tunawaita Maburushi.

  Binafsi nawapongeza kwa dhati wananchi wa Mbarali kumtilia ngumu huyo jamaa mjinga. Huyo jamaa amewaitaye Mbwa nilazima aondoke hapo aende kwao ili akaishi na watu.

  Alichoshindwa kusema wazi ni hiki
  " mimi siongei na ninyi vijibwa vidogo naongea na Jibwa kubwa Jakaya Mrisho Kikwete"

  Anatukana Rangi ya ngozi yetu pamoja na ujinga wetu wa kutumia nguvu zetu zote kugeuza kwetu kuwe kwao.
   
Loading...