Viongozi wa dini wakatishwa tamaa na JK

Mzito Kabwela

JF-Expert Member
Nov 28, 2009
18,857
7,617
Miaka ya nyuma kunapotokea tatizo la ukame tena ambalo halina madhara kama la hivi sasa viongozi wa kikristo na wasio wakrsto hukutana kwa nyakati tofauti kuombea mvua.
Wengine husoma albadiri ili anga litoe matone ya mvua.
Sina hakika na outcome ya albadiri lakini kwa maombi ya wakristo mara zote walizoomba mvua ilinyesha.
Matatizo haya ya umeme na njaa ambayo ni matokeo ya ukame hayajawafanya viongozi wa dini kushtuka na kuombea mvua ambayo inawaathiri waumini wao na hivyo kuathiri hata sadaka.
Matukio ya hivi karibuni yafanywayo na serikali yaliyoambatana na majibu ya kebehi na dharau kutoka kwa Rais yamekatisha tamaa wengi na ninaamini hata viongozi wa dini pia wamekutana na hali hiyo.
RAI YANGU: Viongozi wa dini mnafundisha kusamehe wasameheni hao walafi wa raslimali zetu. Nyie ndio mnapaswa kutuongoza ili tufikie lengo la Mungu aliye juu Mbinguni kwamba tuishi kwa amani na raha duniani na Mbinguni pia
 
Ndio maana tumemsamehe Jk bure na kusamehe kunaendana na matendo. Tutawafundisha waumini wetu kufunga mikanda inapobidi kama sasa. Mbona vita ya Amini watu tulifunga mikanda? Tatizo la kizazi hiki mayai ni kula kula hovyo. Hata hilo tutamwomba Mungu atusamehe.
 
Miaka ya nyuma kunapotokea tatizo la ukame tena ambalo halina madhara kama la hivi sasa viongozi wa kikristo na wasio wakrsto hukutana kwa nyakati tofauti kuombea mvua.
Wengine husoma albadiri ili anga litoe matone ya mvua.
Sina hakika na outcome ya albadiri lakini kwa maombi ya wakristo mara zote walizoomba mvua ilinyesha.
Matatizo haya ya umeme na njaa ambayo ni matokeo ya ukame hayajawafanya viongozi wa dini kushtuka na kuombea mvua ambayo inawaathiri waumini wao na hivyo kuathiri hata sadaka.
Matukio ya hivi karibuni yafanywayo na serikali yaliyoambatana na majibu ya kebehi na dharau kutoka kwa Rais yamekatisha tamaa wengi na ninaamini hata viongozi wa dini pia wamekutana na hali hiyo.
RAI YANGU: Viongozi wa dini mnafundisha kusamehe wasameheni hao walafi wa raslimali zetu. Nyie ndio mnapaswa kutuongoza ili tufikie lengo la Mungu aliye juu Mbinguni kwamba tuishi kwa amani na raha duniani na Mbinguni pia

Kiongozi wetu anasema hawezi kumuomba mungu anyeshe Mvua ili Umeme upatikane!!!
 
Back
Top Bottom