Hapa Tanzania tuna makundi mawili ya viongozi wanaopatikana Makanisani na Misikitini. Kuna viongozi wa DINI na viongozi wa DILI.
Viongozi wa DINI ni wale ambao wanapokuta dhuluma katika Nchi zinazidi sana hususani wakati wa uchaguzi hupaza sauti zao waziwazi ili kukemea udhalimu huo lakini viongozi wa DILI wao hata kama dhuluma zitashamiri namna gani katika Nchi, wao hukaa kimya huku wakiendelea kuneemeka na DILI (sadaka, zaka, fungu la kumi, michango mbalimbali nk.).
Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Kutokana na hali mbaya ya Demokrasia, mpaka sasa tumeshawaona viongozi hao wa DINI na wale wa DILI.
Rai yangu kwa viongozi wa DILI ni kwamba waache mara moja kutafuta DILI tu Makanisani na Misikitini badala yake waongoke na kuwa viongozi wa DINI.
Kiongozi wa DINI huwa tayari kwa lolote pale madhulumu yanapozidi katika Nchi.
Nyie viongozi wa DILI mkiendelea kukaa kimya wakati Nchi inaendelea kutafunwa na Genge la watu wachache mjue saa ikifika tutafika kudai sadaka, zaka, fungu la kumi na michango mbalimbali tuliyowahi kuwapeni huko nyuma.