Viongozi wa dini Tambueni, Tume Huru itapatikana ktk Katiba Mpya. Sisitizeni Katiba Mpya kabla ya 2025

Chagu wa Malunde

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
8,708
5,711
Tupate Katiba Mpya ambayo itaweka wazi kuwa viongozi wa Tume ya Uchaguzi kuanzia mwenyekiti wa taifa mpaka wasimamizi wa uchaguzi wawe watu huru wasiofungamana na upande wowote na wasiwe na vinasaba vya kufungamana na chama chochote.

Huu ndio utakuwa msingi wa kisheria wa kuwa na tume huru isiyokuwa na upendeleo.

Naona mnakomalia habari ya Tume Huru huku mkisahau kuwa Tume Huru itapatikana kama Katiba itaseme tume iwe Huru.

Simamieni taifa letu lipate Katiba Mpya. Maana hali ni tete.

Viongozi wa dini wasisitiza Tume Huru ya Uchaguzi.
 
Huyo kwenye gazeti la Mwananchi ni Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu ya Bakwata, Sheikh Hamis Mataka..

Wanasemaga Bakwata ni taasisi ya ccm. Kama ni kweli unatarajia maajabu yoyote?
 
Watu wanadhani katiba ndio inaongoza nchi wakati katiba hiyo hiyo inatengenezwa na kusimamiwa na watu hasa wanasiasa, kama taifa inatakiwa tutengeneze wanasiasa wazalendo na raia wazalendo na wenye weledi mkubwa, lakini tukiendelea kuwa na wanasiasa ambao leo wanasema hivi mara kesho vile, leo wanaamini hichi kesho wanageuka, leo wanasema fulani fisadi kesho wanasema msafi, hata tuwe na katiba nzuri kiasi gani hatutasonga mbele.
 
Tupate Katiba Mpya ambayo itaweka wazi kuwa viongozi wa Tume ya Uchaguzi kuanzia mwenyekiti wa taifa mpaka wasimamizi wa uchaguzi wawe watu huru wasiofungamana na upande wowote na wasiwe na vinasaba vya kufungamana na chama chochote.

Huu ndio utakuwa msingi wa kisheria wa kuwa na tume huru isiyokuwa na upendeleo.

Naona mnakomalia habari ya Tume Huru huku mkisahau kuwa Tume Huru itapatikana kama Katiba itaseme tume iwe Huru.

Simamieni taifa letu lipate Katiba Mpya. Maana hali ni tete.

Viongozi wa dini wasisitiza Tume Huru ya Uchaguzi.
Ni makanisa matatu tu ndiyo yana viongozi wa dini, ya walokole ni majanga tu.
Katiba hadaiwa na wananchi, wananchi hawatakiwi kuwa watazamaji nchini mwao wanatakiwa wawe mstari wa mbele kudai haki zao, nchi zote zinazofanikiwa kwenye demokrasia huwa ni juhudi za wananchi kusimamia haki zso bila kujali itikadi zao.
 
Back
Top Bottom