DR. MWAKABANJE
JF-Expert Member
- Nov 7, 2012
- 1,976
- 3,127
Baadhi yenu matendo na kauli zenu sio tu zinakera lakini pia zinaleta maswali juu ya uhalali wenu wa kuongoza kondoo wa mungu kuelekea njia iliyonyoofu.
Siku hizi hakuna tena kukemea akina sizonje, kila wanachofanya nyie ni ama kimya au kuwapigia makofi, inamaana malalamiko ya kondoo huku malishoni hamyasikii? Yaani hata mmoja mwenye ujasiri wa kusema katika hili hapana hakuna si bure itakuwa na nyie wachafu kiasi kwamba hamna nguvu ya kukemea ama kuonya.
Ona viongozi wenzenu hapo kenya wameweza kuiambia serikali kuwa hii sheria ya uchaguzi hapana, nenda DRC wameinusuru nchi wa ulafi wa viongozi katika madaraka, huku akina sizonje wanasema, wanafanya, wananena watakavyo na sakramenti wakipokea kwa unyenyekevu wakitoka hapo kauli zao Mungu anawaona.
Haiwezekena kiongozi wa dini huyu utasikia kaiba mke wa mtu, huyu kalewa na kutukana majirani badaye kuwatabiria vifo wengine, hawa wanasemwa kubeba sandarusi za fedha haramu mara huyu kagoma kuachia madaraka n.k. imetosha jitokezeni kukemea, kuonya na kuelekeza sio mnawaza sadaka zetu tu simameni katika kweli na haki nasi tukiwaombea na Mungu atawabariki na taifa kwa ujumla.