Viongozi wa dini kulikoni?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Viongozi wa dini kulikoni??

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kadogoo, Mar 20, 2011.

 1. K

  Kadogoo JF-Expert Member

  #1
  Mar 20, 2011
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,072
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka jana Rais Kikwete aliwaalika viongozi wa dini mbalimbali ktk Ikulu ya Mbeya kula futari kwa heshima ya Mwezi mtukufu wa Ramadhani lakini viongozi wa Makanisa walimsusia kwa kutokuhudhuria karamu hiyo ingawaje miaka yote huko nyuma walikuwa wakihudhuria!

  Hatua hiyo haikunishangaza sana kwa sababu huo ulikuwa ni uamuzi wao ila nachoshindwa kuelewa imekuaje tena viongozi hao hao leo baada ya uchaguzi kwisha wanamualika Rais huyo huyo ktk hafla za Kanisa kuwa mgeni rasmi? jee, kikwete huyu wa leo anatofauti gani na yule wa Mwaka jana? na imekuaje viongozi hawa wa Dini wamebadilika ghafla hivi?

  Gonga hapa:http://www.ippmedia.com/frontend/index.php?l=27224
   
 2. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #2
  Mar 20, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Hawa makuwa!
   
 3. L

  LAT JF-Expert Member

  #3
  Mar 20, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  sijakuelewa kabisaaaa...!
   
 4. K

  Kadogoo JF-Expert Member

  #4
  Mar 20, 2011
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,072
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Bila shaka lugha niliyotumia kufikisha maoni yangu ni Lugha ya Kiswahili sasa kama hujanielewa mbona hujafafanua kuwa hujaelewa nini?
   
 5. nsimba

  nsimba JF-Expert Member

  #5
  Mar 20, 2011
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 785
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33

  Unashangaza unaposhindwa kutofautisha na kuchanganua hoja yako!!!!!!!!! Huelewi nini kipindi akiwataka wakale futali wote mbeya ilikuwa kipindi cha kampeni za uchaguzi; na wao kama viongozi wa dini hawatakiwa kuonesha wanaegemea upande au chama fulani-ndo maana haikuwa busara wao kula naye (ingehesabika ni kampeni). Kumbuka waumini wa dini hizo ni wafuasi wa vyama mbalimbali hivyo kufanya hivyo ni kuleta mvurugano makanisani miongoni mwa waumini. Kwa sasa is not a big deal- wanaweza muita na kuwa naye pamoja kama rais wa nchi-wala si mgombea urais!!! Tofautisha hayo mawili!!!!
   
 6. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #6
  Mar 20, 2011
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  GO9G0027.JPG
  JK na Askofu Joh Nyaisonga
   
 7. Mupirocin

  Mupirocin JF-Expert Member

  #7
  Mar 20, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,596
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Naomba nikusahishe, JK hakuwa mgen rasmi, ni kawaida RC kuwaalika viongozi wa serikali ktk sherehe na mazishi mbalimbali hawajaanza leo. Kule bunda na mwanza alialikwa akatuma wawakilishi utakumbuka wasira na pinda waliwakilisha kwa nyakati tofauti. Afu kumbuka mwaka jana aliwaalika kipindi cha kampeni kipindi hicho jk hakuwa rais ila alikuwa mgombea na yeye mwenyewe alianza kulalamika kwamba kuna udini. Kanisa katoliki haliwezi kuhongwa kwa futali au fedha yeyote ile wewe umeona juzi tu kule sumbawanga kanisa limekataa msaada kutoka kwa mbunge kwani style aliyotumia ilionekana kama ni hongo fulan na kanisa likashtukia. Jua kuwa kanisa linaalika ofisi si mtu. Kama angekuwapo Rais dr Slaa angekuja pia na ndo maana hakuja slaa akaja JK kwa sababu ndo aliyeko ofisin. Nafikiri nimeeleweka naomba kuwasilisha.
   
 8. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #8
  Mar 20, 2011
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Sasa hapo unamlalamikia Raisi kuwa na yeye angesusa ama unawalalamika viongozi wa kanisa kumwalika Raisi. Kwa taarifa yako hivi vitu havifanyiki kiholela. Huwa vinakuwa na sababu za msingi za mtu kualikwa. Walikuambia sababu yao ya kutohudhuria ambayo walimwambia raisi akaridhika na hata yeye kuhudhuria mwaliko huu wa sasa? Kwanini hawakumwalika Shekhe Mkuu ama viongozi wakuu wa madhehebu mengine?
   
 9. k

  kayumba JF-Expert Member

  #9
  Mar 20, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 654
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Mmmmmh, sasa wakulaumiwa nani? aliye alika au aliyealikwa na kukubali kwenda?
   
Loading...