Viongozi wa China waendelea kuonyesha mfano katika juhudi za kuhifadhi mazingira nchini China

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,034
f31fbe096b63f62472d3765e1f4bf7f21b4ca3fe.jpeg

Fadhili Mpunji

Wiki hii Rais Xi Jinping wa China aliendelea na desturi yake ya miaka 10 ya kushiriki kwenye harakati ya kupanda miti inayofanyika kila majira ya spring yanapoanza mjini Beijing. Rais Xi Jinping aliambatana na viongozi wengine waandamizi wa China katika shughuli hiyo, na kujumuika na watu wengine wanaojitolea kupanda miti kati sehemu moja ya kusini mjini Beijing.

Kwa wakazi wa mji wa Beijing ambao bado tunakumbuka siku zilizokuwa na uchafuzi mkali wa hewa ya moshi wa magari na viwanda (smog), na dhoruba la vumbi la mchanga la mwaka hadi mwaka kutoka jangwani (sandstorm). Katika hali ya kukata tamaa kuna watu waliokuwa wanasema itachukua hata miaka 30 kwa mji wa Beijing kuondokana na hali hiyo, lakini sasa wakazi wa Beijing na hata miji mingine ya China tunafurahia hewa safi karibu kwa mwaka mzima, tofauti na zamani ambapo tulihesabu siku chache tu zenye hewa safi. Kumwona Rais Xi na viongozi wengine kwenye shughuli hii ya kupanda miti, kunatufanya tutambue kuwa hewa safi, anga ya bluu na mazingira mazuri tunayoyaona sasa, hayawezi kutenganishwa na juhudi binafsi kutoka kwa viongozi wa China.

Kwa wanaofuatilia changamoto ya mabadiliko ya tabia nchi duniani, bila shaka wanatambua kila nchi sasa inakabiliwa na changamoto mbalimbali zinazotokana na mabadiliko ya tabia nchi. Kuna hatua ambazo dunia nzima inatakiwa kuchukua kwa pamoja, kuna hatua ambazo kila nchi inatakiwa kuzichukua, na kuna hatua ambazo mtu mmoja mmoja anachukua.

Katika kipindi cha miaka 30 iliyopita China imekuwa moja kati ya nchi zilizofanya vizuri katika upandaji wa miti inayofyonza hewa ya Carbon. Katika kipindi hicho eneo misitu limefikia hekta milioni 220, ongezeko lake likiwa ni la tarakimu mbili kila mwaka.

Juhudi hizi za China pia zimeenda sambamba na hatua nyingine za kuhakikisha hewa inakuwa safi, kama vile kubadilisha muundo wa matumizi ya nishati, kama vile matumizi ya nishati endelevu kama ya upepo, jua na maji, na kutumia vyombo vya usafiri kama magari na pikipiki zinazotumia betri. Mwezi Sepetemba mwaka 2021, Rais Xi Jinping aliishangaza dunia baada ya kutoa ahadi kuwa itakapofikia mwaka 2030 China itafikia kilele cha utoaji wa hewa carbon, na kuanzia hapo na kuendelea utoaji huo utapungua na kutarajiwa kufikia 0 mwaka 2060.

Rais Xi Jinping mwenyewe ameonyesha kuwa mstari wa mbele katika juhudi za kuhifadhi mazingira nchini China, na suala la kuthamini mazingira liko kwenye damu yake. Sio tu linaweza kuonekana kwenye kujitokeza kwake kwa miaka kumi mfululizo kwenye harakati ya upandaji miti mjini Beijing, lakini pia linaonekana kwenye historia ya utendaji kazi wake. Kauli moja inayokumbukwa sana ni ile aliyowahi kutoa alipokuwa katibu wa chama wa wilaya ya Ningde, Mkoani Fujian kuwa “milima ya kijani, na mito safi, ni sawa na dhahabu”. Rais Xi alisema hivyo akisisitiza kuwa kujitafutia maendeleo na faida, hakutakiwi kuwa kisingizio cha kuharibu mazingira. Kwani mazingira safi yana thamani sawa na mazingira ya neema.

Lakini pia Rais Xi ameonyesha kutambua kuwa juhudi za kufanya mazingira yawe mazuri, sio za kizazi kimoja na mara zote ameonyesha imani yake kwa vijana. Mwaka huu pia amesisitiza pia kuwa mbegu ya kuhifadhi mazingira ya asili inatakiwa kupandwa mioyoni mwa vijana, ili juhudi za kulinda mazingira ya asili ziwe endelevu.
 
Back
Top Bottom