Viongozi wa CHADEMA pimeni matamshi yenu, msiwape sababu CCM

Molembe

JF-Expert Member
Dec 25, 2012
9,910
11,767
Baada ya kukamatwa makamu mwenyekiti wa BAVICHA nimeitafuta clip ile na kugundua kuwa kijana yule alikosea kitendo cha kuwataka vijana wapambane na polisi wanaoishi uraiani ni uchochezi, polisi wengi wanafanya vile baada ya kupewa amri toka juu sasa kuwataka vijana wawafanyie fujo polisi ni kuwaonea.

Kauli kama hizi zinawafanya wapinzani wapate sababu ya kuwakamata ni bora kuchunga kauli zenu pindi mnapokuwa majukwaani ili kuepuka kuingia matatizoni.

Mwanachama mtiifu CHAUMA.
 
Baada ya kukamatwa makamu mwenyekiti wa Bavicha nimeitafuta clip ile na kugundua kuwa kijana yule alikosea kitendo cha kuwataka vijana wapambane na polisi wanaoishi uraiani ni uchochezi, polisi wengi wanafanya vile baada ya kupewa amri toka juu sasa kuwataka vijana wawafanyie fujo polisi ni kuwaonea.
Kauli kama hizi zinawafanya wapinzani wapate sababu ya kuwakamata ni bora kuchunga kauli zenu pindi mnapokuwa majukwaani ili kuepuka kuingia matatizoni.

Mwanachama mtiifu chauma.
ta!!
 
kama kafanya fyongo wacha polisi wamshughulikie. hakuna kiongozi yoyote aluyemtuma kutoa ushawishi huo. ajifunze adabu next time ajenge hoja za maana sio kuleta uhuni
 
Yule Dogo alipoona Lowassa anamsikiliza akawa anaropoka tu bila ya kupima maneno yake. Alishauri vijana kila wakiona Polisi mitaani wapambane nao. Bavicha wenzie walisambaza sana zile clip wakidhani wanàlpamba kumbe wanamuharibia.
Sijui kama mpaka muda huu hajapigwa ndoa ya mkeka huko "kusikojulikana".
 
Mnafarijiaaana baada ya kuukosa udc teh teh teh ...kesi za kisiasa ni kesi bc , au nyie wageni na hzo kesi nn ...
 
Kwani kauli hiyo inatofauti gani na ile ya wapigwe tuu? Au kunya anye kuku akinya bata kaharisha? Kupiga polisi ni kosa kama ilivyo kupiga raia. Hivyo viongozi wote wachunge kauli zao na kama ni kuchukuliwa hatua wachukuliwe wote.
Hii tabia tunayojenga ya kubagua makosa kwa itikadi itafika mahali kada wa Ukawa akibaka anafungwa mara moja na wa ccm akibaka mtu tunasema mwacheni huyo ni kada wetu.
 
Kumtetea yule kijana na maneno aliyoyasema inahitaji kujitoa ufahamu kama ufanyavyo. Wewe endelea tu.
 
kama kafanya fyongo wacha polisi wamshughulikie. hakuna kiongozi yoyote aluyemtuma kutoa ushawishi huo. ajifunze adabu next time ajenge hoja za maana sio kuleta uhuni
Wakumfunza adabu sio polisi ni mahakama kwa kutumia sheria. Nyie ndo mnawapa polisi kiburi cha kupiga raia hata kama ni mtuhumiwa
 
Back
Top Bottom