VIONGOZI WA CHADEMA KULIKONI

mwengeso

JF-Expert Member
Nov 27, 2014
9,219
6,650
Inasikitisha dhamira ya viongozi wa CHADEMA ya maandamano kutekeleza Tamko lao la UKUTA.

Maneno yanayotamkwa na viongozi wao, si tu yana ukakasi, pia yanatia kinyaa yanapotoka midomoni mwa watu wenye heshima zao katika jamii.

Itafika hiyo tarehe 1/9 iliyopangwa kufanyika kwa maandamani, ati ya kudai kuvunjwa kwa Katiba, wakapambana na vyombo vya Dola, kama viongozi hao watukufu hawatajifikiria upya usahihi wa dhamira yao.

Wakumbuke kwamba wao ndo wanaovunja Katiba kwa kuwa njia sahihi ya kufikisha hilo swala ni mahakamani.

Kifungu cha 30 (1)cha hiyo Katiba, inaodaiwa kuvunjwa na kuilamu Polisi, kinatamka "Haki na Uhuru wa binadamu ambavyo misingi yake imeorodheshwa katika Katiba hii havitatumiwa na mtu mmoja kwa maana ambayo itasababisha kuingiliwa kati au kukatizwa kwa haki na uhuru wa watu wengine au maslahi ya umma".

Naamini viongozi wa CHADEMA wanalijua hilo wanapong'ang'ania kuwepo kwa maandamano, ambayo yamekwisha zuia na mamlaka zilizopo kikatiba. Kuendelea kung'ang'ania kuwepo kwa maandamano ni sababu tosha inayothibitisha kuwa si ya amani.

Njia sahihi si maandamano ila mahakamani kama ilivyoainishwa kwenye Katiba inayodaiwa kuwa inavunjwa:

Kifungu cha 30(3): "Mtu yeyote anayedai kuwa sharti lolote katika Sehemu hii ya Sura (ni Sura ya Tatu: Haki na Wajibu Muhimu)au katika sheria yoyote inayohusu haki yake au wajibu kwake, limevunjwa, linavunjwa au inaelekea litavunjwa na mtu yeyote popote katika Jamhuri ya Muungano, anaweza kufungua shauri katika Mahakama kuu."

TUJIULIZE:

INAKUWAJE VIONGOZI WA CHADEMA HAWATAKI KUTUMIA HII NJIA YA KIKATIBA KUDAI KUVUNJWA KWA KATIBA!

TAFAKARI CHUKUA HATUA
 
Back
Top Bottom