Viongozi wa ccm watuhumiwa kutorosha trilion 16.6.

Dec 11, 2010
3,321
6,328
VIONGOZI na wafanyabiashara nchini, wameelezwa kutorosha na kuhifadhi fedha nje ya nchi kiasi cha Sh trilioni 16.6
fedha ambazo zinazidi bajeti ya Serikali kwa
mwaka 2012/13.

Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina (CCM) alisema hayo
bungeni wakati
akichangia hotuba ya
Makadirio ya Matumizi ya
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Tume ya Mipango kwa mwaka 2012/13 na kuituhumu Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kuwa inajua fedha zote zilizofichwa na
Watanzania nje ya nchi.

Mpina mbali na kuituhumu BoT kufahamu fedha hizo
zilipo, alisema Benki Kuu ya Uswisi imekiri sehemu ya fedha hizo kuhifadhiwa katika benki za nchi hiyo na
Watanzania sita.

“Taasisi ya Global Financial ilibainisha kuwa Sh trilioni
16.6 zimefichwa nje ya nchi na viongozi na
wafanyabiashara wa nchini na Benki Kuu ya Uswisi imesema Sh bilioni 315 ziko
nchini mwao zimefichwa na
watu sita.
“Benki Kuu ya Tanzania (BoT) inajua fedha za Watanzania zilizo nje ya nchi, lakini hadi leo
hawajatwambia ni za nani, ziliibwa lini na zitarejeshwa
lini! Mbali na kufichwa kwa
fedha hizo, Mpina alisema pia kwamba Tanzania inapoteza Sh bilioni 478 kila
mwaka, zaidi ya nusu ya Bajeti ya Zanzibar kutokana na fedha hizo kufichwa
katika benki za nje ya nchi.

Marejeo: Habarileo 04 July, 2012.
 
Mkuu Mtoi, ondoa hofu;

kila kitu wanachokifanya kinajulikana na it is just a matter of time, hapo 2016 thama ya shilingi yetu itaimarika zaidi baada ya kupigwa mnada majengo mbalimbali ndani na nje ya nchi yaliopatikana kwa njia zisizo halali na viburungutu vya mi-dola kurejeshwa toka Uswisi.

Just wait and you will come to see all these come to pass. Vipi yule Marehemu Mtoi au 'Mr White' mnene aliyekua PPF ni ndugu yako?
 
Hasira zinazidi kunipanda, Naomba ndovu moto na viroba vitatu
 
CCM mbona hivi; fedha zote hizo za nini Ughaibuni mbona mnalitesa taifa hivi kwa kuendekeza maslahi binafsi kila mahali hivi?
 
Back
Top Bottom