Viongozi wa ccm wanasiri gani rohoni mwao?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Viongozi wa ccm wanasiri gani rohoni mwao??

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Taifa_Kwanza, May 16, 2011.

 1. T

  Taifa_Kwanza JF-Expert Member

  #1
  May 16, 2011
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 443
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Jamani

  CHADEMA inazunguka nchi nzima kutafuta wanachama kwa maandamano, kwa kulipua mabomu,
  kuichafua CCM, kuamusha UMA, kuwatoa wananchi uoga, kudai katiba, kushinikiza n.k

  Maeneo wanayokwenda hawa jamaa sasa hakuna ambaye alitegemea siku moja chama kisicho CCM
  kitakwenda kwenye maeneo hayo na kupata wasikilizaji kama inavyoonekana sasa.

  wanakwenda vijijini sana, wanakwenda maeneo ambayo ni sawa kabisa na roho ya CCM, Vinapata
  wasikilizaji wengi sana, ikiwa ni dalili ya kukubarika.

  Wakati haya yote yanafanyika viongozi wa CCM hata hawajali, hakuna anayesituka, ndio kwanza
  wanaitisha semina za kisanii, wanachama wao wanapungua, wanalishwa sumu kali sana na
  hatimaye wanawachukia, wao hawajali.

  Hili linanitisha sana, CCM kimekuwa ni kama mtu asiyeogopa kifo, ni kama mtu mgonjwa sana,
  yuko hoi kitandani kwa maradhi lakini hataki kunywa dawa, ni sawa na Muhalifu aliyezingirwa na
  askali wenye siraha kali anaambiwa ajisalimishe lakini hataki na anawaambia wafanye chochote
  lakini hatajisalimisha.

  Ninapatwa na uoga sana, Kinachowapa nguvu za kujiamini namna hii ni nini?
  Nahisi wanasiri OVU sana moyoni mwao. Wanaweza wakawa wameishaweka nadhiri kwamba
  ni bora damu imwagike kuliko kuachia dora...
   
 2. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #2
  May 16, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Mbo ni Simpo sana juu ya siri yenyewe??????????

  Pale CCM hadi hivi sasa siri kubwa walionayo rohoni mwao huko CCM ni juu ya tarehe chama hiki kitakapo anguka chini PWAAAAAAAA na wengine huku uraiani tukaanza kuimba nyimbo za ' TUMPELEKE KIJANA HUYU CCM ...' huku tukielekea mazikoni pale Makaburi ya Kisutu kulikozikwa pia makada wake wengine akina Mzee Moses Nauye na Abbasi Gulamli (mzaliwa wa kijiji cha Ifakara, Morogoro).
   
 3. s

  seniorita JF-Expert Member

  #3
  May 16, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 674
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Hawana siri yeyote on the contrary it is a sign that they are weak and defeated
   
 4. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #4
  May 17, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,986
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  Siri waliyo nayo ni kupanga jinsi ya kuja na sera za uongo, kama kiongozi mmoja alivyo sema kuwa uongo ukiusisitiza unageuka kuwa ukweli!!!!!!
  Kila linalosemwa na CDM ni la ukweli sasa watasimama wapi kupinga ukweli, lazima wapinge ukweli kwa kusema uongo. Lakini siku hizi hata huko vijijini watu wamesha choka kudanganywa!!!!!!! Its a matter of time kila jambo litakuwa wazi!!!!!!!
   
Loading...