chidy abidal
Member
- Mar 4, 2015
- 6
- 4
*VIONGOZI MNA MENGI YA KUJIFUNZA KWENYE SOKA*
Soka ni miongoni mwa michezo inayopendwa zaidi duniani hasa kutokana na matokeo yake ya kustaajabisha ambayo mara nyingine huwaliza na kuwafurahisha watazamaji wake. Pia vile vile mchezo wa soka umekuwa ukifananishwa sana na mchezo mmoja maarufu sana pia ila kwa muktadha huu ngoja niuache hamuchelewi kusema kijana sina adabu.
Kama ilivyo michezo mingine ni lazima kuwe na mshindi, Ili mshindi apatikane kwenye soka basi ni lazima mpira uvuke mstari wa goli kihalali kwa kufuata sharia 17 za mpira wa miguu. Wakati natafakari magoli magumu yaliyowahi kufungwa kwenye soka nikajikuta narejea Septemba 18 mwaka 2011 mnamo dakika ya 81 mchezo kati ya Manchester United dhidi Chelsea pale mshambuliaji nguli wa timu hiyo Fernando Torres alipokosa bao la wazi kabisa akiwa ametazamana nyavu daah! soka lina matokeo magumu sana.
Mchezo wa soka unatoa taswira halisi ya Uongozi, Kama ambavyo timu ya soka ina wachezaji 11 uwanjani ndivyo hivyo pia kwenye uongozi kuna safu zinazounda uongozi huo. Fernando Torres wakati anakosa lile bao ule mpira hakuutoa mwenyewe golini kwake bali ilikuwa ni kazi nzuri ya Mbrazil Ramires, Hivi ndivyo viongozi wanaangushana katika safu mbalimbali za uongozi.
Ili apatikane kiongozi bora basi ni lazima michakato halali ya kisheria ifuatwe ili apatikane kiongozi halali anayejua misingi na weledi ya uongozi kama vile kwenye soka waamuzi wanavyosimamia kwa weledi sheria 17 za mchezo huo na sasa wameongeza VAR aaaah hii VAR ya kwenye chaguzi zetu huku sijui inaangalia nini.
Hali inakuwa mbaya Zaidi kwa viongozi wanaopewa nafasi za uongozi kwa undugu,urafiki, ujamaa au aina fulani ya ‘ugenge genge’ hivi. Viongozi wa aina hii hawana ubunifu zaidi ya kuhakikisha wanawafurahisha mabwana zao waliowaweka madarakani. Viongozi wa aina hii hawajui kuwa ili ufanikiwe ni lazima ushirikiane na unaowaongoza na wale mnaoongoza nao kwa pamoja ndo maana mwanzoni nikaanza hadithi ya Fernando Torres ambaye angejua uchungu wa jasho la Ramires asingefanya alichofanya.
Viongozi waliopewa dhamana kwa njia za ‘ndondokela’ hawana utulivu hawajui nini wafanye, hawajui nini washike na kwababu gani. Binafsi siwalaumu kwasababu hata wakati wanapewa hawakufundishwa namna ya kutumia walichopewa lakini naweza kuwa walakini na uwezo wao kufikiri kwa sababu hawana tofauti na mtoto mdogo unayeweza myang’anya shilingi 100/= ukampa shilingi 20/= akafurahi kisa tu ukubwa umbo lake.
Viongozi wa aina hii hawaijui thamani ya uongozi zaidi ya kujitanabaisha kuwa wao ni viongozi tena wanyonge wa hali chini tena huwa waoga wa kukosolewa na mara zote huwashutumu wale wanaowakosoa na kuwapuuza kwa kuamini kuwa wanawachukia, Anayetanguliza silaha kuhisi anachukiwa mara zote chuki huwa moyoni mwake. Usishangae ‘wamezoea vya kunyonga vijana wa ndondokela’.
Hakuna haja ya kutafuta mchawi muarobaini wa hayo yote ni kuacha uchu na tamaa ya madaraka, kupunguza ubinafsi, kuongeza uwezo wa kufikiri Zaidi ya yote ni kumuogopa Mungu kwa ys, Tuishi tukiamini kuwa kuna siku yaja tutahukumiwa kwa yale tunayoyatenda sasa.
RAJABU RAJABU A.
0715685395
rajabuathumani123@gmail.com