Viongozi mjisahihihe; Kuongoza siyo kupiga marufuku bali ni kuleta suluhisho

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,284
21,403
Chuki hupandwa, huchipua na hukua na huenea!

Chuki ni kama harufu mbaya ambapo bila kutoa uozo harufu inaendelea kuwepo!

Viongozi wengi hasa awamu hii wamekosa maono, wamegeuka wanyampala! Viobgozi wengi siku hizi Wanazani kuongoza na udanganya, kuficha, kupiga marufuku au kuzalilisha!

Huwezi kuongoza kwa kupiga marufuku! Kama kiongozi hauna suluhisho ni afadhali kukaa kimya ofisini!

Mfano!
Kiongozi Huwezi kufunga njia kisa kwako kuna msiba ili kushinikiza wapita njia wahudhurie msiba wako!

Kufanya hivyo ni unyampala na ukatili kwasababu lazima ufikilie kuna watu wamekodi usafili watahitaji kupita, kuna wagonjwa watahitaji kupita, kuna malighafi zinahitaji kupita;

Sasa kisa wewe una msiba unataka hayo yote yasifanyike! Hivi tangu lini Kulia au kucheka ikawa ni jambo la lazima?!

Viongozi Hizo marufuku zenu ziangalieni mnagusa maisha ya watu, Marufuku zizingatie uhalisia, Ratiba na uchumi wa watu!

Mtu anakuwa kashagharamia halafu ghafla kiongozi anapiga marufuku bila kutaja ni kifungu gani cha sheria kinalazimisha marufuku yake!

Kiongozi msiwe wanyampala, tumieni akili na utu kabla ya kuamua msije kuharibu!
 
Acheni jamani Jiwe azikwe,yeye ndie alikuwa mkandarasi wa mambo yote ya hovyo hovyo na anakwenda nayo huko kwenye uongozi wake wa malaika waasi
 
hivi yule konda mkuu wa "MAKONDA" yupo wapi??...kweli nyota ing'aayo hupotea gafula......tusipende kujijengea maadui...wacha maadui waje wenyewe....
 
kuna mtu kapiga marufukun sherehe zote mkoani kwake , kwakuwa anajua kuna wanaosherehekea mara mbili hahaaaa za kwao na za tukio
 
Usiwakumbushe mkuu,sisi wakileta unyampala Kama awamu ilopita sisi tutawashtakia kwa Mungu wetu......
Hakika hawatapona WATAKUFA.
 
Acheni jamani Jiwe azikwe,yeye ndie alikuwa mkandarasi wa mambo yote ya hovyo hovyo na anakwenda nayo huko kwenye uongozi wake wa malaika waasi
Katiba ingebadilishwa Rais akifa aende zake pamoja na baraza la mawaziri, DC, wakurugenzi na walinzi wake kama ilivyokuwa misri ya zamani yani wanakuwa mummified ili waendelee na utopolo wao huko kuzimu
 
Katiba ingebadilishwa Rais akifa aende zake pamoja na baraza la mawaziri, DC, wakurugenzi na walinzi wake kama ilivyokuwa misri yani wanakuwa mummified ili waendelee na utopolo wao huko kuzimu
mkuu umenichekesha sana nimekumbuka kisa kimoja cha mtumwa alikuja kombolewa na ndugu zake akakataa kata kata kuondoka kwa yule bwana et sababu alikua anatendewa wema,
Ndugu wakamsihi sana sana aondoke nao kwani familia yake ndo mtoto pekee wa kiume aliyebaki lakini jamaa akakaza msimamo kua bwana wake anamfanyia hisani kubwa kwahiyo hawezi ondoka,
Basi ndugu wakaondoka zao baada ya miaka miwili mbele yule bwana akafa na mila za pale mkuu akifa anazikwa na mjakazi wake aliempenda jamaa si ndio akachaguliwa weeeee

Alijaribu kukataa wapi,lia sanaa pale haikusaidia,jamaa akawakumbuka wale ndugu walikuja mkomboa lakini akawa kashachelewa ndo akazikwa mzima pamoja na bosi wake,

Kwahiyo na wewe mkuu ulitamani kina musiba wazikwe na kiongozi wa malaika wallah nimecheka haaaaaaahaaaaahaa
 
Yaani ni shida. Wameshindwa tu kutulazimisha kulia. Waache vitu viendee naturally, wenye kulia walie, na wenye kushereheka pia waendelee.

Na makatazo yenyewe ni so vague. Sherehe zipi? Yaani mie niache kuoa na kufurahia siku yangu ya ndoa? Mwanangu ana birthday yake, tusifungue champagne na kufurahi nyumbani kwetu?

Kama Rais alipendwa na wananchi wake hakuna haja ya makatazo. Tutamlilia tu bila kulazimishwa.
 
Ka
Yaani ni shida. Wameshindwa tu kutulazimisha kulia. Waache vitu viendee naturally, wenye kulia walie, na wenye kushereheka pia waendelee.

Na makatazo yenyewe ni so vague. Sherehe zipi? Yaani mie niache kuoa na kufurahia siku yangu ya ndoa? Mwanangu ana birthday yake, tusifungue champagne na kufurahi nyumbani kwetu?

Kama Rais alipendwa na wananchi wake hakuna haja ya makatazo. Tutamlilia tu bila kulazimishwa.
Kabisa
 
Back
Top Bottom