Viongozi kwenye msafara wa Kikwete wapotea!!!

vivian

JF-Expert Member
Nov 2, 2009
1,749
1,000
baadhi ya magari yaliyokuwa katika msafara wa rais Kikwete leo yakielekea uwanja wa ndege Nduli
Magari yaliyopotea kwenda Ikulu yakiwa uwanja wa Ndege Nduli
WIKI ya maji yamalizika kwa kituko cha mwaka mkoani Iringa baada ya viongozi waliokuwa katika msafara wa Rais Jakaya Kikwete kupotea mjini Iringa.

Tukio hilo limetokea Leo majira ya 9.30 alasiri baada ya viongozi hao kutoka katika chakula cha mchana na Rais Kikwete katika ukumbi wa St Dominic ulipo eneo la RETCO kata ya Gangilonga.

Viongozi hao wakiwemo viongozi wa Manispaa ya Iringa pamoja na wale wa kitaifa waliofika katika maadhimisho ya wiki ya maji kitaifa ,Sherehe zilizofanyika mkoani Iringa walijikuta wakipotea badala ya kuelekea Ikulu wao walielekea uwanja wa Ndege Nduli nankulazimika kugeuza .

Mbali ya viongozi hao kupotea pia askari polisi wa FFU na wanahabari waliokuwemo msafara huo nao walijikuta wakipotezwa na viongozi hao baada ya kuelekea uwanja wa Ndege Nduli na kugeuza eneo la FM Abri na kuelekea Ikulu.

Mmoja kati ya viongozi waliokuwemo katika msafara huo alisema kuwa kupotezana kwa viongozi hao katika msafara huo ni kutokana na magari kugawanyika kwa yale ya Manispaa ya Iringa kuelekea uwanja wa Nduli na msafara wa Kikwete kuelekea Ikulu na askari aliyekuwepo eneo hilo kushindwa kujua magari yanayokwenda Ikulu ni yapi na yanayokwenda uwanja wa Ndege kabla ya Rais ni yapi.

Mwandishi wa habari hizi ambaye pia alikuwemo katika msafara huo alishuhudia kupotezana huko kwa magari hayo yaliyokuwemo katika msafara wa Rais Kikwete huku baada ya magari yakilazimika kupita njia za vichochoroni ili kutokea Ikulu kuungana na msafara wa Rais Kikwete ambaye alikwenda Ikulu ndogo ya mkoa wa Iringa kwa mapumziko mafupi.


kwa hisani ya Francis Godwin.
 
Hawakuwa na mawasiliano?

siyo mara ya kwanza misafara yake kupotezana. Unakumbuka habari ya trafiki aliyejinyonga baada ya kuupoteza msafara wake mwanzoni wa uongozi wake? Ndo maana anajitetea yeye siyo dhaifu.
 
Mmh kwa yule trafic alojiua ni kwsbb ya kupoteza msafara mzima wa Rais na wakat Iringa ni baadhi tu ya magari yalounga msafara ndiyo yalopotea kwa maelezo ya mtoa taarifa; sasa hapa ni tatizo la madereva na mabosi wao hawakufanya mawasiliano vyema kwamba wakati msafara unaelekea Ikulu wao watatangulia Airport; sasa katika hili sio Rais wala wasaidizi wake, wala Police(Trafiki) au FFU wanahusika, sema kwa FFU walopotea wao huo ni uzembe wa dereva na mkuu wake kwa maana mkuu wao wa msafara huwapa uelekeo"
 
siyo mara ya kwanza misafara yake kupotezana. Unakumbuka habari ya trafiki aliyejinyonga baada ya kuupoteza msafara wake mwanzoni wa uongozi wake? Ndo maana anajitetea yeye siyo dhaifu.

Tunakumbuka sana tena ilikuwa huko katika mkoa wa Mara. Kikubwa ni kuwa nchi yenyewe ndiyo iliyopoteza njia, hayo ya msafara wa rais ni cha mtoto.
 
Magari yote hayo yanawekwa mafuta kuwapeleka watu kwenda kumuaga rais au sijui kupata chakula au yako kwenye msafara
viongozi wote wa mkoa na wilaya wameacha kazi zao kuzunguka na rais kokote aendako
Na hapo mnazungumzia tija na ufanisi na uzalishaji
Watazalisha muda upi wakati wako busy kuzunguka na mheshimiwa
 
Nilikua yamepata ajari!
Kama kupotea tuu sio issue kwa Tz ya sasa
 
Wangepotelea kuzimu kabisa hao maharamia wa jasho letu jk labda mungu angempenda zaidi
 
Yalirudia fm abri ili yajaungane na mhe pale ikulu, mara tena yamejipanga uwanja wa ndege, tushike lipi ss
 
Back
Top Bottom