Viongozi kuzuia mazao ya chakula yasitoke nje ya maeneo yanapozalishwa wanawatendea haki wakulima?

fundik

Member
Apr 22, 2013
59
38
Hawa hawajui ugumu wa kulima, wanazuia mazao yasitoke ili soko liwe gumu wasiolima wanunue kwa bei rahisi. Kutokana na hasara/ faida ndogo wakulima hawawezi kupanua kilimo na wasiolima hawawezi kuvutika kutafuta mashamba, matokeo uzalishaji hauongezeki na umaskini unatamalaki.
 
hao viongozi ni wapuuzi hivi nani anawapangia namna ya kutumia mshahara wao isitoshe si sehemu zote wanalima mfano dar es salaam hamna mashamba ya kulisha watu wa jiji hili
 
Unaongelea viongozi gani? Na wapi unadai hili limetokea?

Unapoteza muda mwingi kujadili post za siasa za majitaka kiasi kwamba hujui mambo kama haya tunayokutana nayo wakulima. Kwa taarifa yako ni tabia ya kawaida kwa viongozi wa nchi hii kutuzuia wakulima kuuza mazao yetu tunapotaka nje ya nchi kwenye maslahi mazuri. Kibaya zaidi unakuta viongozi hao hawana msaada wowote kwa mkulima wakati anapoanza kuandaa shamba, kuotesha hadi kuvuna achia mbali msaada wa pembejeo, lakini wakati wa kuuza unakuta kiongozi aliyekaa ofisini muda wote anakugomea kuuza nje ya nchi.
 
Sasa ndio umenijibu nini, kama ndivyo unaongea na hao viongozi husiotaka hata kutoa mfano wa unapoongelea basi kaa ujisaidie mwenyewe kuyamaliza.

Unanirukia na hasira huku unaandika gazeti kwa kuni quote ili iweje? Unafikiri watu tumo humu JF kuotea habari kama akina nani. Ukileta uzi andika, ukiulizwa ondoa hasira esp kama ni wa kulalamika. Na hasira zako nenda nazo hukooooo tutasoma wengine wakileta habari kama hii... ungekuwa na majina au eneo na umeumia haswa usingeficha tangu mwanzo bali ungeandika ukweli....as hukuandika acha kutunga yako na kuogopesha wananchi wengine.
 
Mkuu, wakulima ni Uti wa mgongo wacha watumike. Kwanza hao ndio wateja wa CCM
 
Sio siri hii inakera sana! Kulima nilime mimi matumizi unipangie wewe....
 
Back
Top Bottom